Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Aliye Kufundisha Anayo Sifa na Mamlaka ya Kufundisha hilo Ameyapata wapi [emoji53] Yesu alitupa Wafuasi wake Tbs hii [emoji117] View attachment 867725 wewe gavana kujua hii ni HAQI NA HII NI BATILI UNATUMIA TBS GANI [emoji47]
Kila mti hutambulika kwa matunda yake.” (Luka 6:44). Sawa na usemi huu wakati tunampima Bwana Yesu Kristo tunamkuta kwamba ameanguka vibaya sana.
Ingawa sisi tumempenda na tumemuheshimu. Lakini kumpenda kwetu hakumsaidii. Maana Biblia inamuangusha vibaya sana.
Kwa mfano:
(1) “Amini nawaambieni, pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapo muona mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.” (Mathayo 16:28).
Watu ambao walikuwa pamoja naYesu na vizazi vyao zaidi ya hamsini wamekwisha kufa tayari. Hakuna mmoja wao ambaye
ameweza kushuhudia, mwana wa Adamu (Yesu Kristo) akija katika ufalme wake.
Kwahiyo utabiri wa Yesu haujatimia bali imeonekana uwongo.
2. “Yesu akamwambia, amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israel.” (Mathayo 19:28).
Katika aya hii Bwana Yesu Kristo aliwabashiria wanafunzi wake kumi na wawili kuhusu mwisho mwema wa kiimani na kuwa viongozi wa makabila ya Waisraeli.
Lakini mwanafunzi wake mmoja bwana Yuda hakumuasi tu bali alimuuza kwa shilingi thelathini.
Kwa hivi alitoka katika imani na ufalme wa kiroho.
Biblia inasema kwamba: “Wakati huo mmoja wa wale thenashara, jina leke Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani, akisema, ni nini mtakacho nipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelethini vya fedha.” (Mathayo 26:14 -15).
3. Bwana Yesu Kristo alisema kwamba: “(Ewe Petro) nami nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalo lifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.” (Mathayo 16:19).
Katika aya hii Bwana Yesu alim'bashiria Petro kwamba ataendelea vizuri kiimani kwa hali ya juu, lakini hali inaonesha kwamba utabiri huu wa Bwana Yesu ulivurugika vibaya mno. Hata inaonekana aibu kutaja utabiri ule.
Biblia inasema kwamba: “Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, wewe nawe
ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. Akakana mbele ya wote, akisema, sijui usemalo. Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimuona, akawaambia watu walio kuwako huko, huyu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti. Akakana tena kwa kiapo, simjui mtu huyu. Punde kidogo, wale walio hudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, hakika wewe nawe u mmoja wao. Kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha. Ndipo akaanza kulaani na kuapa na kusema, simjui mtu huyu.” (Mathayo 26:69-74).
4. “Yesu akamwambia mwizi mmoja aliyekuwa pamoja naye msalabani: “Amin, nakuambia leo hii utakuwa pamoja nami peponi.” (Luka 23:43).
Aya hii inaonesha kwamba siku ya kusema habari hii Bwana Yesu Kristo na huyu mwizi wangeenda peponi kwa Baba lakini
inaonekana kwamba utabiri huu haukutimia, maana baada ya siku ya tatu Yesu bado alikuwa duniani.
Biblia inasema kwamba Yesu alimwambia, usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.” (Yohana 20:17).
Katika mifano hii ya Biblia nimejaribu kuonesha watu baadhi ya matunda ya tabiri za Yesu, na kila mmoja analalamika kwamba matunda haya ni machungu sana. Kwahiyo mti umetambulika kwa matunda yake.