Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Ahahahahhahahahaahhahahahaha mtu anamuita Mungu mpumbavu halafu unamuita Profesa hizi bange hizi
WAKORINTHO wa kwanza 1:25
";Kwa sababu UPUMBAVU wa Mungu, una hekima zaidi ya wanadamu, na UDHAIFU wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu";

Yaani mtu anatangaza hadharani Mungu ana upumbavu na udhaifu uwe mzuri au mbaya lakini anao udhaifu na Upumbavu ,Ahahaahahaha halafu mtu anatetea upuuzi huo kweli mahaba niue eti Paulo profesa buree kabisa Wewe
Tatizo ni HUJUI KUSOMA Ungekuwa unajua ungekuwa MAUDHUI PROF PAULO AMEONGEA NINI!
 
Hawa Wakristo ambao baba fatúú alio sema [emoji117]
IMG_20180806_124946_626.jpg
[emoji38] [emoji38]
 
Ahahahhqqhaqqahqhqhqhqhqhqhq waislamu tunaongozwa na QURAN na Sunah , hicho kitabu cha KONTRA BALIK umekitoa Vatican ahahahahahhahhahha

Mnazidi kupunguza Imani [emoji38] [emoji38] ndio sababu warabu Wenye deen yao wanawazogodoa na kuwafananiaha na [emoji117]
IMG_20161005_172807.jpg
[emoji12]
 
sijaona katazo la moja kwa moja la kuuliza hapo!!!

Naomba katazo la kuuliza swali la moja kwa moja

mimi nitakupa aya inayotuamrisha tuulize,ikiwa hatujui
weka tukufundishe [emoji4]
 
Ahahahaahaaaahaahaah tabu iko pale pale QURAN iko wazi kabisa Adamu aliposhushwa dunia alikuwa mtu saaafi wala hakuwa na dhambi ( Mungu wetu ni mwenye kupokea toba) , midhambi ya kurisishana kama mali za ukoo huku kwenye uislamu tumekataa
Kaomba wapi Toba [emoji53] [emoji47]
 
Ahahaaaahahahhahhahahq ndio umeandika kitu gani!! Roho atawaongoza watu kwenye kweli haya tuambie UKWELI ni Yesu alivishwa vazi lipi na wale askari dhambarau au jekundu? ahahaahahahaahahhahaha mbona rahisi tu
Nyeusi...[emoji53]
 
Allah kulinda makanisa alijibu swali letu kuwa neno "WAKRISTO" umetoa wapi? WAOVU na WEMA wote ni wa watu waliombwa na Mungu ndio maana wanapata pumzi bila wasiwasi , tena wabaya wanadumu wema wanakufa, Swali liko pale pale neno "WAKRISTO" mpaka yesu anaondoka duniani akuwai kuwaita wafuasi wake hilo jina ww na wenzio mmeanza lini kujiita WAKRISTO? halafu kuhusu Al HAJJ :40 ni kweli mkitenda wema mtapata ujira na mkitenda ubaya pia mtapata ujira wenu a ahaahhahaaahahaaa hapo hakuna hoja mpya MUNGU amesema tumiulize je MMESILIMU ?
QURAN 3:20
" Na pindi WAKIKUHOJI basi sema; mimi NIMEUSALIMISHA uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata, Na waambie WALIOPEWA kitabu na wasio na kisoma; JE MMESILIMU? wakisilimu basi WAMEONGOKA .Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaona waja wake";

ahahaahaaahahahqhaqqqhq wewe piga kelele hoja ziko mbili
1.Nani alianza kumiita nyie WAKRISTO
2.MMESILIMU?
Mwambie walahi hatujisalimishi kwa popo bawa [emoji12]
 
DHAMBI NA KAFARA

Ningebainisha kwanza ya kwamba Wakristo wote hawaamini neno kwa neno yatakayofuata hapa chini.

Hata baadhi ya viongozi wa Kanisa wamekwenda upande na kuachana na msimamo mgumu wa fundisho la imani la Kanisa.

Hata hivyo falsafa ya 'Dhambi na kafara' ni kanuni ya msingi ya imani ya Kikristo inayokubalika kwa jumla.

Sehemu ya kwanza ya maana ya Dhambi na Kafara ni kwamba Mungu ni mwadilifu na anafanya uadilifu wa dhati. Yeye
hasamehe dhambi pasipo kuadhibu; kwani kusamehe tu dhambi hivi hivi kungekuwa kinyume cha uadilifu halisi.

Sifa hiyo ya Mungu inasababisha kafara ilivyoaminiwa na Wakristo kuwa jambo la lazima.

Sehemu ya pili ni kwamba mtu ni mwenye dhambi kwa sababu Adamu na Hawa walitenda dhambi. Matokeo yake ni kwamba
wazao wao wakaanza kurithi dhambi, kana kwamba hiyo dhambi ikaingizwa katika vijine (genes) vyao na tangu hapo watoto wote
wa Adamu huzaliwa wakiwa wenye dhambi.

Sehemu ya tatu ya itikadi hiyo ni kwamba mwenye dhambi hawezi kutoa kafara ya dhambi ya mwingine: mtu asiye na dhambi pekee ndiye anayeweza kutoa kafara ya dhambi za wengine.

Juu ya msingi huu, inakuwa wazi sawa na ufahamu wa Kikristo, ya kwamba Nabii yeyote wa Mungu hata akiwa mwema namna gani ama akiwa karibu sana na ukamilifu hawezi kumtakasa mtu nakumwondolea dhambi na matokeo yake. Akiwa mwana wa Adamu, asingeweza kuepukana na dhambi aliyorithi alipozaliwa.

Huo ndiyo muhtasari wa muradi wa imani nzima ya kafara.
 
Nyeusi...[emoji53]

KAFARA KWA MWANADAMU:

Ili kutatua tatizo lisiloweza kutatulika kidhahiri, Mungu akawaza mpango wa akili sana.

Haijulikani kwamba yeye alishauriana na mwana ama hapana; ama wote wawili wakawaza mpango huu wakati mmoja; au uliwazwa na mwana peke yake lakini ikakubaliwa na Mungu Baba.

Maelezo ya mpango huu yalifafanuliwa katika zama za Yesu kama ifuatavyo. Miaka elfu mbili iliyopita 'Mwana wa Mungu' aliyeshirikiana na Mungu katika umilele barabara, alipata kuzaliwa tumboni mwa mama wa kibinadamu.

Akiwa 'Mwana wa Mungu' yeye akajikusanyia ndani yake sifa kamilifu za kibinadamu na pia za Mungu Baba.

Tena tunaambiwa ya kwamba mama mmoja mwema na mtawa, jina lake Mariamu, akachaguliwa kuwa mzazi wa 'Mwana wa
Mungu'

Mama huyo akashika mimba ya Yesu kwa kushirikiana na Mungu. Ndiyo kusema kwamba Yesu akiwa mwana halisi wa Mungu akazaliwa pasipo kuwa na dhambi, hata hivyo akachukua sifa na sura ya binadamu.

Hivyo akajitolea kwa hiari yake kubeba mzigo wote wa madhambi ya wale watu watakaomwamini na
kumkubali kuwa mwokozi wao.

Kwa njia ya mpango huo wa akili, inadaiwa, Mungu akaepa kuhatarisha sifa yake ya uadilifu halisi.

Kumbukeni ya kwamba sawa na mpango huu pia mtu hatasamehewa dhambi pasipo kuadhibiwa. Bado Mungu ataweza
kumwadhibu mwenye dhambi bila ya kuepa sifa yake ya uadilifu.

Tofauti yenyewe ni kwamba sasa Yesu ataadhibiwa, siyo wale wana na mabinti wa Adamu waliotenda dhambi. Hiyo ni fidia ya Yesu itakayosababisha kuwaondolea dhambi watoto wa Adamu.

Mantiki hiyo hata ikionekana ya ajabu na ya kutatanisha , lakini ndivyo ilivyokubaliwa hasa kwamba ilitendeka.

Yesu akajitolea mweyewe na akaadhibiwa kwa ajili ya dhambi ambazo hakuzitenda kabisa
 
Mwambie walahi hatujisalimishi kwa popo bawa [emoji12]

Kaomba wapi Toba [emoji53] [emoji47]

DHAMBI YA ADAMU NA HAWA:

Hebu tuchunguze upya kisa cha Adamu tangu mwanzo. Sehemu yoyote ya itikadi hiyo hapo juu haiwezi kukubaliwa na dhamiri
ya mtu na mantiki.

Kwanza, tunaambiwa ya kwamba kwa kuwa Adamu na Hawa walitenda dhambi, basi wazao wao wakachafuliwa kwa kudumu na dhambi waliyorithi wakati wa kuzaliwa.

Lakini kinyume chake, sayansi ya tabia zirithishwazo inabainisha ya kwamba mawazo na matendo ya mtu, yakiwa mazuri ama mabaya , hata mtu akiwa nayo kwa kudumu maisha mazima, hayawezi kuhamishwa katika mfumo wa tabia za kurithishwa katika kuzaana.

Muda wa maisha ya mtu ni mdogo sana kwa kuleta mabadiliko hayo makubwa.

Hata maovu ama mema ya taifa, kizazi baada ya kizazi, hayawezi kuingizwa katika wazao yakiwa ni mienendo ya kurithiwa.

Labda mamilioni ya miaka inahitajika kuingiza sifa mpya katika vijine (genes) vya mtu.

Hata kama mtu angekubali kutukia jambo hilo la ajabu la kutatanisha kwa kapanua mawazo yake ya kipuuzi yasiyokubalika
akilini, basi na angekubali kilicho dhidi yake pia kwa kutumia mantiki kama hiyo.

Hiyo itamaanisha ya kwamba kama mtu mwenye dhambi akitubu na akatakasika mwishoni mwa siku, basi hiyo nayo ingerekodiwa katika mfumo wa sifa zile zinazorithishwa na kufutilia mbali kabisa athari ya dhambi ile ya zamani.

Kisayansi hiyo haiwezi kutendeka, lakini kwa yakini kuna mantiki zaidi katika picha hiyo inayoonesha pande mbili kwa
usawa kuliko kufikiria kwamba maelekeo kwa dhambi tu yanaandikwa katika utaratibu wa sifa za kurithishwa lakini
maelekeo ya mema hayaandikwi.
 
Uko kilingeni gavana [emoji47] [emoji4] hayo uliyo cp ni kutoka maabara yako [emoji38] [emoji38]
 
Mnazidi kupunguza Imani [emoji38] [emoji38] ndio sababu warabu Wenye deen yao wanawazogodoa na kuwafananiaha na [emoji117] View attachment 870081 [emoji12]

Pili, kwa kujaribu kutatua tatizo la Adamu kwa kutoa shauri ya kuwa dhambi inahamishwa kwa vizazi vijavyo ambavyo vinairithi
tangu kuzaliwa, msingi wenyewe unabomolewa ambao juu yake imani ya 'Dhambi na kafara' imejengwa.

Kama Mungu ndiye mwadilifu halisi, basi upo wapi uadilifu katika kuwahukumu wazao wote wa Adamu na Hawa kwa dhambi yao waliyotenda mara mmoja tu na kisha wakatubu pia?

Kwa vyovyote, hiyo ilikuwa dhambi ambayo waliadhibiwa vikali kwa sababu yake na wakafukuziliwa mbali katika Pepo kwa
fedheha kubwa .

Ni aina gani ya uadilifu ya kwamba baada ya kuwaadhibu Adamu na Hawa sana sana kupita kiasi kwa sababu ya dhambi yao, bado hamaki ya kujilipiza kisasi haijapoa na akawahukumu wanadamu wote wapate fedheha ya kuzaliwa tayari wamerithi dhambi?

Nafasi gani wanayo wazao wa Adamu kuikwepa dhambi?

Kama wazazi wanafanya kosa, kwa nini watoto wao wasiokosea wasumbuke daima kwa sababu ya kosa la wazazi wao?

Kama ni hivyo, basi batilifu iliyoje maana ya uadilifu anayojidaia Mungu na kuifurahia ikiwa Yeye anawaadhibu watu
waliopangiwa kutenda dhambi hata wakichukia dhambi namna gani?

Dhambi ikafanywa sehemu ya maana sana ya maumbile yao. Hamna kabisa sasa nafasi kwa mtoto wa Adamu kubaki
katika hali ya kutokuwa na dhambi. Kama dhambi ndiyo jinai basi ni jinai ya Mwumbaji siyo ya viumbe.

Basi, uadilifu gani ungetaka kuwaadhibu wasiokosea kwa jinai za wengine?
Tangazo la Kurani Tukufu ni tofauti kabisa na ufahamu wa Kikristo wa dhambi na matokeo yake. Kurani Tukufu inatangaza:

Hakuna mbebaji atakayebeba mzigo wa mwingine. (35: 19)
Mungu haikalifishi nafsi yoyote zaidi ya uwezo wake. (2:287)

Tangazo hilo la Kurani kwa kulinganisha na imani ya Kikristo kuhusu Dhambi na Kafara ndiyo taratibu halisi ya kuituliza roho.

Sasa tugeukie maelezo ya Biblia kuhusu yaliyotendeka hasa wakati Adamu na Hawa walipotenda dhambi, na matokeo
yaliyofuata nyuma ya wao kuadhibiwa.

Sawa na mafunzo ya Mwanzo, Mungu alikubali nusu-nusu udhuru wao na wakapewa adhabu ya kudumu milele inavyoelezwa hapa chini:

Wanadamu walikuwapo muda mrefu sana kabla hawajazaliwa Adamu na Hawa. Wanasayansi wa magharibi wenyewe
waligundua mabaki ya watu wengi waliokuwepo ardhini katika zama za kale sana na wakawapa majina mbali mbali ya
kupambanua. Neanderthal - mtu pengine ndiye anayejulikana zaidi miongoni mwa hao.

Wa-Neanderthal waliishi zaidi katika Yoropa,Mashariki ya Karibu na Asia ya Kati, baina miaka 100,000 na 35, 000 mpaka sasa. Maiti ya mtu mkamilifu imenguduliwa ambaye mtu huyo aliishi ardhini miaka 29,000 kabla Adamu na Hawa hawajaanza safari yao fupi huko Peponi.

Katika zama hizo wanadamu kimaumbile walikuwa kama sisi na waliishi katika Yoropa, Afrika na Asia, na baadaye mnamo zama za Theluji (Ice Age) walienea hadi Marekani pia. Vilevile huko Australia historia thabiti ya utamaduni wa Waaborijini (Aborigines) inaonesha ulianza miaka 40,000 iliyopita kutoka leo. Waaborijini ni watu wa asili ya Australia.

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto, na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo kwa hiyo ulitwaliwa kwa maana u mavumbi wewe nawe mavumbini utarudi (Mwanzo 3:16-19)

Kwa kulinganisha na zama za hivi majuzi, mifupa yote ya mwili ikiwa pamoja, ya mwanamke, imepatikana huko Hedar katika Ethiopia ambayo mifupa hiyo ni ya tangu miaka milioni 2.9. Sasa kwa kulingana na matukio ya historia yalivyoelezwa katika Biblia, Adamu na Hawa waliishi karibu miaka 6,000 tu tangu leo.

Mtu aweza kuangalia nyuma kwa mshangao taarifa ya historia ya wanadamu, ama Homo Sapiens wanavyoitwa katika istilahi
ya Kisayansi
 
KAFARA KWA MWANADAMU:

Ili kutatua tatizo lisiloweza kutatulika kidhahiri, Mungu akawaza mpango wa akili sana.

Haijulikani kwamba yeye alishauriana na mwana ama hapana; ama wote wawili wakawaza mpango huu wakati mmoja; au uliwazwa na mwana peke yake lakini ikakubaliwa na Mungu Baba.

Maelezo ya mpango huu yalifafanuliwa katika zama za Yesu kama ifuatavyo. Miaka elfu mbili iliyopita 'Mwana wa Mungu' aliyeshirikiana na Mungu katika umilele barabara, alipata kuzaliwa tumboni mwa mama wa kibinadamu.

Akiwa 'Mwana wa Mungu' yeye akajikusanyia ndani yake sifa kamilifu za kibinadamu na pia za Mungu Baba.

Tena tunaambiwa ya kwamba mama mmoja mwema na mtawa, jina lake Mariamu, akachaguliwa kuwa mzazi wa 'Mwana wa
Mungu'

Mama huyo akashika mimba ya Yesu kwa kushirikiana na Mungu. Ndiyo kusema kwamba Yesu akiwa mwana halisi wa Mungu akazaliwa pasipo kuwa na dhambi, hata hivyo akachukua sifa na sura ya binadamu.

Hivyo akajitolea kwa hiari yake kubeba mzigo wote wa madhambi ya wale watu watakaomwamini na
kumkubali kuwa mwokozi wao.

Kwa njia ya mpango huo wa akili, inadaiwa, Mungu akaepa kuhatarisha sifa yake ya uadilifu halisi.

Kumbukeni ya kwamba sawa na mpango huu pia mtu hatasamehewa dhambi pasipo kuadhibiwa. Bado Mungu ataweza
kumwadhibu mwenye dhambi bila ya kuepa sifa yake ya uadilifu.

Tofauti yenyewe ni kwamba sasa Yesu ataadhibiwa, siyo wale wana na mabinti wa Adamu waliotenda dhambi. Hiyo ni fidia ya Yesu itakayosababisha kuwaondolea dhambi watoto wa Adamu.

Mantiki hiyo hata ikionekana ya ajabu na ya kutatanisha namna kuelekea kwenye Ubunifu gani, lakini ndivyo ilivyokubaliwa hasa kwamba ilitendeka.

Yesu akajitolea mweyewe na akaadhibiwa kwa ajili ya dhambi ambazo hakuzitenda kabisa
wewe umejiajiri lini KUWA mc Wa Mwenyezi [emoji12] endelea kumuona Mungu kama babu yako mzaa mama-ako [emoji53]
 
DHAMBI NA KAFARA

Ningebainisha kwanza ya kwamba Wakristo wote hawaamini neno kwa neno yatakayofuata hapa chini.

Hata baadhi ya viongozi wa Kanisa wamekwenda upande na kuachana na msimamo mgumu wa fundisho la imani la Kanisa.

Hata hivyo falsafa ya 'Dhambi na kafara' ni kanuni ya msingi ya imani ya Kikristo inayokubalika kwa jumla.

Sehemu ya kwanza ya maana ya Dhambi na Kafara ni kwamba Mungu ni mwadilifu na anafanya uadilifu wa dhati. Yeye
hasamehe dhambi pasipo kuadhibu; kwani kusamehe tu dhambi hivi hivi kungekuwa kinyume cha uadilifu halisi.

Sifa hiyo ya Mungu inasababisha kafara ilivyoaminiwa na Wakristo kuwa jambo la lazima.

Sehemu ya pili ni kwamba mtu ni mwenye dhambi kwa sababu Adamu na Hawa walitenda dhambi. Matokeo yake ni kwamba
wazao wao wakaanza kurithi dhambi, kana kwamba hiyo dhambi ikaingizwa katika vijine (genes) vyao na tangu hapo watoto wote
wa Adamu huzaliwa wakiwa wenye dhambi.

Sehemu ya tatu ya itikadi hiyo ni kwamba mwenye dhambi hawezi kutoa kafara ya dhambi ya mwingine: mtu asiye na dhambi pekee ndiye anayeweza kutoa kafara ya dhambi za wengine.

Juu ya msingi huu, inakuwa wazi sawa na ufahamu wa Kikristo, ya kwamba Nabii yeyote wa Mungu hata akiwa mwema namna gani ama akiwa karibu sana na ukamilifu hawezi kumtakasa mtu nakumwondolea dhambi na matokeo yake. Akiwa mwana wa Adamu, asingeweza kuepukana na dhambi aliyorithi alipozaliwa.

Huo ndiyo muhtasari wa muradi wa imani nzima ya kafara.
Jidunge ndoba afu kambishie Mungu [emoji53]
 
Uko kilingeni gavana [emoji47] [emoji4] hayo uliyo cp ni kutoka maabara yako [emoji38] [emoji38]

MATESO YA BINADAMU YAENDELEA:

Akiisha soma maelezo ya Biblia kuhusu walivyoadhibiwa Adamu na Hawa, mtu hana budi kustaajabu kama kweli uchungu wa kuzaa haukujulikana kwa mwanamke hadi zama za Adamu na Hawa zilipoanza.

Mwanasayansi yeyote hawezi kukurubia kuwaza mawazo kama hayo yasiyo ya kweli. Isitoshe, tunao ushahidi mwingi usiyoweza kukanushwa ya kwamba, muda mrefu hata kabla ya Adamu na Hawa hawajapatikana, wanadamu walikuwa
wanaishi katika mabara yote ya dunia, hata huko visiwa vya Bahari ya Pasifiki vilivyo mbali kabisa, na daima walijibidiisha sana ili kupona katika hatari.

Kwa hiyo kusema kwamba Adamu na Hawa walikuwa watu wa kwanza kutenda dhambi kwa sababu hiyo sheria ya kumwadhibu mwanamke kwa uchungu wa kuzaa iliundwa, kumethibitika kwamba ni batili kabisa, hakuna msingi wake, tukitaali maisha ya binadamu.

Hata wanyama wa daraja la chini zaidi wanajifungua kwa uchungu.

Kama mtu akishuhudia ng’ombe akimzaa ndama, ataona ya kwamba uchungu wake unafanana na uchungu wa mwanamke akizaa.

Wanyama wengi sana mno wa aina hiyo twajua walipatikana juu ya uso wa ardhi mamilioni ya miaka kabla ya Adamu na Hawa.

Kuchuma riziki kwa taabu ni jambo la kawaida kwa mtu, lakini haihusikani na wanaume pekee bali hata wanawake pia wanapata taabu kwa kuchuma riziki zao. Tangu zamani kila kiumbe hujipatia riziki yake kwa kujibidiisha na kusumbuka.

Hakika hiyo ndiyo iliyosababisha kuleta mabadiliko na maendeleo katika uhai.

Kujibidiisha ili kubaki hai ndiyo pengine kipambanuzi kinachopambanua baina ya kilicho hai na kisichokuwa na uhai.

Hiyo ndiyo kanuni ya kawaida isiyohusikana na dhambi. Kama hiyo ndiyo adhabu iliyotolewa kwa sababu ya dhambi
waliyotenda Adamu na Hawa, basi mtu atashangaa itatokea nini baada ya kafara yaani baada ya dhambi hiyo kufutiliwa mbali.

Kama Yesu Kristo alikuwa amefutilia mbali dhambi za watu wenye dhambi, je, adhabu iliyotolewa kwa Dhambi ya Adamu na Hawa iliondolewa baada ya tukio la Msalaba?

Je, wale wanawake waliomwamini Yesu Kristo kuwa 'Mwana wa Mungu' hawasikii sasa uchungu wakati wa kuzaa?

Na je, wanaume waumini wameanza kuchuma riziki zao pasipo kujibidiisha kufanya kazi kwa mikono?

Je, tabia ya kutenda dhambi iliishia papo hapo pasipo kuingia ndani ya vizazi vingine na watoto wasio na dhambi wakaanza kupata kuzaliwa?

Kama majibu ya maswali yote hayo ndiyo 'Naam', hapo bila shaka kuna sababu kiasi fulani ya kutafakari kwa makini falsafa ya Kikristo kuhusu Dhambi na Kafara yake.

Lakini, ole wako, majibu ya maswali hayo yote ni: Hapana, hapana tena hapana! Kama lolote halikupata kubadilika tangu tukio la Msalaba katika ulimwengu wa Wakristo na wasio Wakristo, basi Kafara ina maana gani tena?

Hata baada ya Yesu kusulibiwa, uadilifu unamtuma mtu duniani kote ya kwamba mtu yeyote akitenda dhambi, aadhibiwe yeye huyo tu aliyefanya dhambi hiyo pasipo kuwaadhibu wengine.

Wanaume na wanawake wote watasumbuka kwa sababu ya dhambi zao wao wenyewe. Watoto huwa wanazaliwa bila ya dhambi. Kama hiyo siyo sawa, basi uadilifu wa Mungu unatupiliwa mbali.

Sisi tukiwa Waislamu tunaamini ya kwamba vitabu vyote vya Mungu vina msingi juu ya ukweli wa daima wala hakuna awezaye kudai dhidi yake.

Tunapoona hitilafu katika kitabu kimojawapo miongoni mwa vitabu vinavyodaiwa kuwa vya Mungu, hatukikani moja kwa moja bali twashika njia ya kukichunguza kwa uangalifu na kwa upole.

Maneno mengi ya Agano la Kale na Agano Jipya tunayoona ni dhidi ya ukweli wa kawaida, hapo kwanza twajaribu kuyachukua hayo kimithali na kimafumbo, ama twayakataa tukifahamu kwamba hiyo sehemu imeingizwa na watu humo ndani wala siyo maneno ya Mungu.

Ukristo ukiwa dini ya kweli usingekuwa na upotevu, mambo na itikadi zisizokubalika zilizo dhidi ya kanuni ya ulimwengu. Ndiyo sababu hatukuanzia na uchunguzi wa matini ya Biblia, bali tukaanzia na imani za kimsingi ambazo imani hizo zilikubaliwa na ridhaa ya watu wote kuwa sehemu za lazima za falsafa ya Kikristo. Kitu cha kwanza kabisa katika itikadi hizo ni muradi wa Kikristo wa Dhambi na Kafara.
 
Pili, kwa kujaribu kutatua tatizo la Adamu kwa kutoa shauri ya kuwa dhambi inahamishwa kwa vizazi vijavyo ambavyo vinairithi
tangu kuzaliwa, msingi wenyewe unabomolewa ambao juu yake imani ya 'Dhambi na kafara' imejengwa.

Kama Mungu ndiye mwadilifu halisi, basi upo wapi uadilifu katika kuwahukumu wazao wote wa Adamu na Hawa kwa dhambi yao waliyotenda mara mmoja tu na kisha wakatubu pia?

Kwa vyovyote, hiyo ilikuwa dhambi ambayo waliadhibiwa vikali kwa sababu yake na wakafukuziliwa mbali katika Pepo kwa
fedheha kubwa .

Ni aina gani ya uadilifu ya kwamba baada ya kuwaadhibu Adamu na Hawa sana sana kupita kiasi kwa sababu ya dhambi yao, bado hamaki ya kujilipiza kisasi haijapoa na akawahukumu wanadamu wote wapate fedheha ya kuzaliwa tayari wamerithi dhambi?

Nafasi gani wanayo wazao wa Adamu kuikwepa dhambi?

Kama wazazi wanafanya kosa, kwa nini watoto wao wasiokosea wasumbuke daima kwa sababu ya kosa la wazazi wao?

Kama ni hivyo, basi batilifu iliyoje maana ya uadilifu anayojidaia Mungu na kuifurahia ikiwa Yeye anawaadhibu watu
waliopangiwa kutenda dhambi hata wakichukia dhambi namna gani?

Dhambi ikafanywa sehemu ya maana sana ya maumbile yao. Hamna kabisa sasa nafasi kwa mtoto wa Adamu kubaki
katika hali ya kutokuwa na dhambi. Kama dhambi ndiyo jinai basi ni jinai ya Mwumbaji siyo ya viumbe.

Basi, uadilifu gani ungetaka kuwaadhibu wasiokosea kwa jinai za wengine?
Tangazo la Kurani Tukufu ni tofauti kabisa na ufahamu wa Kikristo wa dhambi na matokeo yake. Kurani Tukufu inatangaza:

Hakuna mbebaji atakayebeba mzigo wa mwingine. (35: 19)
Mungu haikalifishi nafsi yoyote zaidi ya uwezo wake. (2:287)

Tangazo hilo la Kurani kwa kulinganisha na imani ya Kikristo kuhusu Dhambi na Kafara ndiyo taratibu halisi ya kuituliza roho.

Sasa tugeukie maelezo ya Biblia kuhusu yaliyotendeka hasa wakati Adamu na Hawa walipotenda dhambi, na matokeo
yaliyofuata nyuma ya wao kuadhibiwa.

Sawa na mafunzo ya Mwanzo, Mungu alikubali nusu-nusu udhuru wao na wakapewa adhabu ya kudumu milele inavyoelezwa hapa chini:

Wanadamu walikuwapo muda mrefu sana kabla hawajazaliwa Adamu na Hawa. Wanasayansi wa magharibi wenyewe
waligundua mabaki ya watu wengi waliokuwepo ardhini katika zama za kale sana na wakawapa majina mbali mbali ya
kupambanua. Neanderthal - mtu pengine ndiye anayejulikana zaidi miongoni mwa hao.

Wa-Neanderthal waliishi zaidi katika Yoropa,Mashariki ya Karibu na Asia ya Kati, baina miaka 100,000 na 35, 000 mpaka sasa. Maiti ya mtu mkamilifu imenguduliwa ambaye mtu huyo aliishi ardhini miaka 29,000 kabla Adamu na Hawa hawajaanza safari yao fupi huko Peponi.

Katika zama hizo wanadamu kimaumbile walikuwa kama sisi na waliishi katika Yoropa, Afrika na Asia, na baadaye mnamo zama za Theluji (Ice Age) walienea hadi Marekani pia. Vilevile huko Australia historia thabiti ya utamaduni wa Waaborijini (Aborigines) inaonesha ulianza miaka 40,000 iliyopita kutoka leo. Waaborijini ni watu wa asili ya Australia.

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto, na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo kwa hiyo ulitwaliwa kwa maana u mavumbi wewe nawe mavumbini utarudi (Mwanzo 3:16-19)

Kwa kulinganisha na zama za hivi majuzi, mifupa yote ya mwili ikiwa pamoja, ya mwanamke, imepatikana huko Hedar katika Ethiopia ambayo mifupa hiyo ni ya tangu miaka milioni 2.9. Sasa kwa kulingana na matukio ya historia yalivyoelezwa katika Biblia, Adamu na Hawa waliishi karibu miaka 6,000 tu tangu leo.

Mtu aweza kuangalia nyuma kwa mshangao taarifa ya historia ya wanadamu, ama Homo Sapiens wanavyoitwa katika istilahi
ya Kisayansi
Kakufundisha nani [emoji47] mwalimu wako na kigezo chako baba fatúu kafa [emoji12]
 
MATESO YA BINADAMU YAENDELEA:

Akiisha soma maelezo ya Biblia kuhusu walivyoadhibiwa Adamu na Hawa, mtu hana budi kustaajabu kama kweli uchungu wa kuzaa haukujulikana kwa mwanamke hadi zama za Adamu na Hawa zilipoanza.

Mwanasayansi yeyote hawezi kukurubia kuwaza mawazo kama hayo yasiyo ya kweli. Isitoshe, tunao ushahidi mwingi usiyoweza kukanushwa ya kwamba, muda mrefu hata kabla ya Adamu na Hawa hawajapatikana, wanadamu walikuwa
wanaishi katika mabara yote ya dunia, hata huko visiwa vya Bahari ya Pasifiki vilivyo mbali kabisa, na daima walijibidiisha sana ili kupona katika hatari.

Kwa hiyo kusema kwamba Adamu na Hawa walikuwa watu wa kwanza kutenda dhambi kwa sababu hiyo sheria ya kumwadhibu mwanamke kwa uchungu wa kuzaa iliundwa, kumethibitika kwamba ni batili kabisa, hakuna msingi wake, tukitaali maisha ya binadamu.

Hata wanyama wa daraja la chini zaidi wanajifungua kwa uchungu.

Kama mtu akishuhudia ng’ombe akimzaa ndama, ataona ya kwamba uchungu wake unafanana na uchungu wa mwanamke akizaa.

Wanyama wengi sana mno wa aina hiyo twajua walipatikana juu ya uso wa ardhi mamilioni ya miaka kabla ya Adamu na Hawa.

Kuchuma riziki kwa taabu ni jambo la kawaida kwa mtu, lakini haihusikani na wanaume pekee bali hata wanawake pia wanapata taabu kwa kuchuma riziki zao. Tangu zamani kila kiumbe hujipatia riziki yake kwa kujibidiisha na kusumbuka.

Hakika hiyo ndiyo iliyosababisha kuleta mabadiliko na maendeleo katika uhai.

Kujibidiisha ili kubaki hai ndiyo pengine kipambanuzi kinachopambanua baina ya kilicho hai na kisichokuwa na uhai.

Hiyo ndiyo kanuni ya kawaida isiyohusikana na dhambi. Kama hiyo ndiyo adhabu iliyotolewa kwa sababu ya dhambi
waliyotenda Adamu na Hawa, basi mtu atashangaa itatokea nini baada ya kafara yaani baada ya dhambi hiyo kufutiliwa mbali.

Kama Yesu Kristo alikuwa amefutilia mbali dhambi za watu wenye dhambi, je, adhabu iliyotolewa kwa Dhambi ya Adamu na Hawa iliondolewa baada ya tukio la Msalaba?

Je, wale wanawake waliomwamini Yesu Kristo kuwa 'Mwana wa Mungu' hawasikii sasa uchungu wakati wa kuzaa?

Na je, wanaume waumini wameanza kuchuma riziki zao pasipo kujibidiisha kufanya kazi kwa mikono?

Je, tabia ya kutenda dhambi iliishia papo hapo pasipo kuingia ndani ya vizazi vingine na watoto wasio na dhambi wakaanza kupata kuzaliwa?

Kama majibu ya maswali yote hayo ndiyo 'Naam', hapo bila shaka kuna sababu kiasi fulani ya kutafakari kwa makini falsafa ya Kikristo kuhusu Dhambi na Kafara yake.

Lakini, ole wako, majibu ya maswali hayo yote ni: Hapana, hapana tena hapana! Kama lolote halikupata kubadilika tangu tukio la Msalaba katika ulimwengu wa Wakristo na wasio Wakristo, basi Kafara ina maana gani tena?

Hata baada ya Yesu kusulibiwa, uadilifu unamtuma mtu duniani kote ya kwamba mtu yeyote akitenda dhambi, aadhibiwe yeye huyo tu aliyefanya dhambi hiyo pasipo kuwaadhibu wengine.

Wanaume na wanawake wote watasumbuka kwa sababu ya dhambi zao wao wenyewe. Watoto huwa wanazaliwa bila ya dhambi. Kama hiyo siyo sawa, basi uadilifu wa Mungu unatupiliwa mbali.

Sisi tukiwa Waislamu tunaamini ya kwamba vitabu vyote vya Mungu vina msingi juu ya ukweli wa daima wala hakuna awezaye kudai dhidi yake.

Tunapoona hitilafu katika kitabu kimojawapo miongoni mwa vitabu vinavyodaiwa kuwa vya Mungu, hatukikani moja kwa moja bali twashika njia ya kukichunguza kwa uangalifu na kwa upole.

Maneno mengi ya Agano la Kale na Agano Jipya tunayoona ni dhidi ya ukweli wa kawaida, hapo kwanza twajaribu kuyachukua hayo kimithali na kimafumbo, ama twayakataa tukifahamu kwamba hiyo sehemu imeingizwa na watu humo ndani wala siyo maneno ya Mungu.

Ukristo ukiwa dini ya kweli usingekuwa na upotevu, mambo na itikadi zisizokubalika zilizo dhidi ya kanuni ya ulimwengu. Ndiyo sababu hatukuanzia na uchunguzi wa matini ya Biblia, bali tukaanzia na imani za kimsingi ambazo imani hizo zilikubaliwa na ridhaa ya watu wote kuwa sehemu za lazima za falsafa ya Kikristo. Kitu cha kwanza kabisa katika itikadi hizo ni muradi wa Kikristo wa Dhambi na Kafara.
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]

DHAMBI YA KURITHIWA:

Hebu tufikirie kwa shabaha ya kuhojiana ya kwamba Adamu na Hawa walifanya dhambi hasa jinsi ilivyoelezwa katika Agano la
Kale.

Adhabu yake, inavyoelezwa katika kisa, haikutolewa kwao pekee bali hata kwa wazao wao wote. Kama adhabu hiyo ilikwisha
amuliwa na kutolewa tayari, ilikuwa haja gani tena ya adhabu nyingine yoyote?

Kama adhabu imekwisha tolewa kwa dhambi moja, basi habari ikaisha. Hukumu ikiisha tolewa tayari, mtu yeyote hana haki ya kuendelea kuongeza daima adhabu nyinginezo.

Katika kesi ya Adamu na Hawa siyo kwamba walilaumiwa tu vikali sana kana kwamba walitenda jambo lililozidi kuliko dhambi inayotolewa adhabu, bali hata aina ya adhabu waliyotolewa ambayo iliendelea kwa wazao wao pia siyo
barabara kabisa.

Kuhusu hiyo tumekwisha eleza vya kutosha.

Tunalojaribu kulidokeza ni uvunjaji wa uadilifu halisi unaochukiza sana sana. Kuadhibiwa kwa kudumu kwa dhambi
walizotenda babu zetu ni jambo tofauti lakini ni chukizo moja kwa moja kulazimishwa kuendelea kufanya dhambi kwa sababu tu babu wa mtu aliwahi kufanya kosa fulani.

Hebu tufikirie hakika tupu ya majaribio ya mtu na kujaribu kuelewa falsafa ya Kikristo ya dhambi na adhabu kwa kulingana
na yale tunayoshuhudia kila siku.

Tufikirie hukumu aliyotolewa mvunja sheria ambayo hukumu hiyo ni kali zaidi sana kulingana na dhambi iliyotendwa. Kila mtu mwenye akili atailaumu vikali sana hiyo hukumu isiyolingana kabisa na kosa lililotendwa.

Kwa hiyo, twaona ni vigumu kuamini ya kwamba adhabu aliyopewa Adamu kwa dhambi yake ilitolewa na Mungu mwadilifu.

Hiyo siyo tu habari ya adhabu kutokulingana na dhambi. Hiyo ndiyo adhabu ambayo sawa na ufahamu wa Kikristo wa mwenendo wa Mungu ikaendelea hata baada ya Adamu na Hawa kufariki na kudumu kupatikana kwa wazao wao kizazi baada ya kizazi.

Wazao kupata adhabu ya wazazi wao kwa hakika ni kuuvunjilia mbali uadilifu kupita mipaka.

Lakini hatuzungumzii hiyo pia. Kama kwa bahati mbaya tukishuhudia jaji mmoja wa zama hizi katoa hukumu iliyowalazimisha watoto wajukuu na vilembwe na kadhalika wa mvunja sheria fulani na kuwashurutisha kisheria kuendelea na dhambi hiyo na kuhalifu na kuadhibiwa kadhalika daima dawamu, itafanyaje jamii ya kisasa ambayo imekwisha tambua maana hasa ya uadilifu kwa sababu ya utamaduni kupata maendeleo?

Msomaji anapaswa kukumbushwa hapa ya kwamba nadharia hiyo ya dhambi ya kurithiwa imeletwa na Bwana Paulo aliyeeleza vibaya sehemu fulani ya maandiko. Hiyo haiwezi kunasibishwa kwa mafundisho ya Agano la Kale.

Upo ushuhuda wa kuelemea katika vitabu vingi vya Agano la Kale ulio kinyume chake kabisa.

Mnamo karne ya tano, Augustine, Askofu wa Hippo, aliingia katika mapambano na mwendeleo wa (Pelagian Movement)
kuhusu majadiliano juu ya hakika ya Adamu na Hawa kuanguka kwa kufanya dhambi.

Bwana Askofu alitangaza ya kwamba wafuasi wa mwendeleo wa Pelagius ndio wazushi kwa sababu wanafundisha ya kwamba dhambi ya Adamu ilimwathiri Adamu tu pekee siyo kizazi kizima cha Adamu kwa ujumla, na kwamba kila mmoja anazaliwa akiwa hana dhambi na anao uwezo wa kuishi maisha yasiyo na dhambi na kwamba walikuwepo watu
waliofaulu kuishi pasipo dhambi.

Waliokuwa sawa wakabandikwa jina 'wazushi' .

Mchana ukaitwa usiku na usiku ukaitwa mchana . Uzushi ukawa ukweli na ukweli ukawa uzushi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom