Unagonga ncha ya mkuki na kuumia mwenyewe afu unadai unatoa kipigi [emoji12] akili za kisla ni kichekesho [emoji4] "HAKUNA MUNGU APASWAYE KUABUDIWA KWA HAQI ILAHA YESU NA PROF PAULO BAKORA YA MAJAHIDI NI MTUME WAKE [emoji123] [emoji106] " Hutaki meza sumu ya panya ufe, team kiguzo wapate tenda ya kukukamua ngama [emoji4]
USHIRIKIANO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA UUMBAJI:
Hatuoni kazi yoyote iliyoshughulikiwa na Roho mtakatifu au Yesu Kristo katika mpango wa uumbaji:
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. (Mwanzo 1:1)
Hakuna shaka kwamba katika Agano la Kale Mungu Baba ndiye ametajwa aliyeumba mbingu na nchi pasipo hata kudokeza habari ya Kristo ama Roho mtakatifu.
Zama zote za kabla ya Ukristo, miongoni mwa Mayahudi ,walioliamini Agano la Kale na bila
shaka waliwahi kusikia mstari huo hapo juu mara malaki kwa malaki, hakuna hata mmoja aliyeweza kulisoma jina la Kristo au
la Roho Mtakatifu katika kisa cha uumbaji wa ulimwengu.
Katika Injili ya Yohana Mtakatifu 'Neno' limetumika kwa ajili ya Yesu. Ni la ajabu ya kwamba habari ya muhimu kabisa imezungumzwa na Injili moja peke yake; tena na yule ambaye hata hakuwa mwanafunzi wa Yesu.
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. (Yohana 1:1).
Hata mtu akikubali usemi wake kuwa neno la Mungu, hata hivyo huo utamaanisha kuwa Takwa la Mungu; hilo ni wazo linalopatikana katika dini nyingine vile vile katika habari ya uumbaji.
Ni mshangao mkubwa ya kwamba siri ya zamani sana ya Kristo na Roho Mtakatifu kushirikiana pamoja katika uumbaji ikabaki
kuwa siri hata kwa Yesu mwenyewe. Hatusomi hata mara moja ya kwamba Yesu Kristo alidai kuwa Neno.
Hivyo, Yesu wala Roho Mtakatifu hawakuwa na sehemu yoyote ya kazi ya kufanya katika uumbaji. Tena twaambiwa ya kwamba alikuwa ni Mungu Baba peke yake aliyemfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi kwa mikono yake mwenyewe.
Sijasoma kabisa katika maandiko yoyote ya Kikristo ya kwamba mikono hiyo miwili ilikuwa ya Yesu na Roho Mtakatifu.
Basi Mungu aliumba vitu vyote pasipo kusaidiwa hata kidogo ama kushirikiana na Yesu ama Roho Mtakatifu.
Je, hao walikaa tu na kuangalia wakikubaliana kwa jumla na aliyokuwa anafanya Mungu ama walishirikiana naye
hasa?
Kama wataalamu wa Kikristo wanapendelea kukubali ya kwamba hao wawili nao walishirikiana katika uumbaji, basi haraka swali litazuka ya kwamba je, kila mmoja kati yao alikuwa na uwezo wa kuumba bila kusaidiwa na wengine, ama walikuwa
na uwezo huo wakiwa pamoja?
Isitoshe, kama wote watatu walihitajika kutoa mchango wao kwa kuumba, hapo je, wote wakatoa mchango kwa usawa ama mmoja wao akalazimika kutoa sehemu kubwa zaidi katika mpango wa uumbaji?
Je, kila mmoja katika hao watatu alikuwa na namna na kiasi cha uwezo tofauti ama uwezo wa kila mmoja ulikuwa sawa
na uwezo wa mwenzake?
Mtu hata akikiri hii au ile analazimika kukubali ya kwamba kila mmoja katika Utatu hana uwezo wa kuumba chochote peke yake.
Kama hoja hiyo itumiwe kwa kazi nyinginezo za Mungu, swali hilo hilo litawasumbua wataalamu wa Kikristo. Na mwishowe Wakristo watalazimika kukiri ya kwamba wao hawaamini dhati moja ya Mungu mwenye jiha na sura tatu za nguvu kuu na utukufu.
Bali wanaamini sehemu tatu za Uungu zilizo mikato mitatu ya mwili wa Mungu.
Hapo swala la sehemu zote kuwa sawa ama si sawa halitakuwa na uzito zaidi. Kwa mfano, chukueni sifa ya uadilifu na msamaha. 'Mwana' anaonekana kuwa na huruma zaidi ilhali Mungu Baba anaonekana Mwadilifu kidogo kuliko Roho Mtakatifu ambaye hakushirikiana na Mungu Baba katika dhuluma yake.
Uwezekano wa pili tuliozungumzia ulikuwa kwamba pengine Yesu na roho Mtakatifu walikaa tu pasipo kushirikiana kwa kitendo katika shughuli za uumbaji na kuendesha kanuni za ulimwengu. Kama ni hivi, hapo yatazuka maswali mengi mengine.
Kwanza kabisa, hao washiriki wawili wa Mungu walipewa kazi gani katika kutekeleza wajibu wao wa Kiungu.
Kama hao ndio washiriki wa kukaa tu kimya kama washiriki katika biashara wanaokaa tu pasipo kushughulikia kazi kwa kitendo, hapo wamekwisha punguziwa hadhi yao na kupewa daraja la pili ambako wanakuwapo pamoja na Mungu lakini bila ya kushirikiana naye hususan katika madaraka yake.
Wazo hili la Mungu kuwa na nyongeza mbili zisizo na kazi ni jambo la kutatanisha kusema kwa uchache. Nashangaa, wazo hilo linaweza kuwatuliza kina nani.
Hiyo haiwezi kukubaliwa kiakili wala haiafikiani na imani ya Kikristo ya 'Watatu katika Mmoja' na 'Mmoja katika Watatu'. Watatu hawawezi kuwa na Umoja wala haiwezekani kuwaza umoja huo pasipo hao watatu kuunganika kikamilifu katika nia, madaraka na mengine yote yanayoweza kudhaniwa katika maisha ya mmoja.
Ama Roho Mtakatifu akiwa dhati peke yake, asipofungamana kikamilifu kwa kudumu na wengine wawili akitengana na nafsi
yake, hakuna tumaini kujitokeza kwa Mungu mwenye vichwa vingi akiwa na fikara moja nia moja na mwili mmoja.