Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Unaita "Queen" kudhihirisha jinsi Dini yako inavyo dharau Wanawake..
TULIA UPATE ELIMU
KUHUIKA AU KUFUFUKA
Habari ya Yesu kuhuika katika wafu inaleta matatizo mengi.
Sasa tunageukia baadhi ya sababu nyingine na matatizo mengine.
Tunachokusudia ni asili ya 'ubongo' wa Yesu kabla hajasulubiwa na baada ya kufufuka katika wafu. Ubongo wake ukahuishwa
baada ya kuacha kufanya kazi kwa siku tatu mchana na usiku.
Swali lenyewe ni kwamba mtu anapokufa ubongo unakuwaje hasa?
Kuhusu jambo moja wataalamu wa matibabu walio Wakristo na wasio Wakristo wanapatana. Na jambo lenyewe ni ya kwamba ubongo ukifa kwa zaidi ya dakika chache unakufa kwa kudumu hauhuiki tena.
Damu ikatikapo tu, ubongo huanza kuchanganua.
Kama Yesu alikufa juu ya msalaba, hiyo inamaanisha kuwa moyo wake ulikoma kufanya kazi na kuacha kupeleka damu kwenye
ubongo wake na kwa hiyo ubongo wake ukafa haraka baadaye.
Basi utaratibu mzima wa kusaidia uhai kubaki ukakoma kufanya kazi, la sivyo yeye asingeweza kuchukuliwa kwamba amekufa.
Kama ni hivi, twakabiliwa na tatizo la kukanganya kuhusu ufahamu wa uhai na mauti ya Yesu Kristo.
Kifo cha Yesu Kristo, ilivyoelezwa nyuma, kinamaanishakuondoka mwili wa kiroho, ama roho, katika kizimba cha mwili wa kibinadamu. Kama ni hivi, basi kuhuika kwake kutamaanisha kurejea mwili huo huo wa kiwiliwili aliouacha siku tatu kabla.
Kurudi roho hivyo kutaanzisha upya uhai wa kiwiliwili. Na ili kutendeka hilo hakuna budi seli zilizokufa za ubongo zihuike
ghafla na hali ya kuchanganuka haraka irudishwe nyuma kabisa.
Habari hiyo italeta matatizo mengi ambayo yatawadaia milele wanakemia Wakristo kuyatatua. Kueleza kurudi nyuma kabisa
kuchanganuka na kuoza utaratibu wa kati wa ki-neva ni jambo lisiloweza kuwazwa na mwanasayansi.
Kama kwa vyovyote ilifanyika, basi itakuwa ni mwujiza tu ukigongana na Sayansi na kuzidhihaki kanuni zilizoundwa na Mungu Mwenyewe; lakini itakuwa ni mwujiza ambao bado utashindwa kutatua tatizo lililoko mbele yetu.
Kuhuika hivyo siyo tu kuhuika seli za utaratibu wa kati wa kineva,bali kwa hakika kuziunganisha pamoja hadi zikawa kitu kimoja.
Hata kama seli zilezile za zamani ziundwe tena na kuhuishwa kabisa zilivyokuwa hapo kabla, hata hivyo kwa hakika huo utakuwa utaratibu mpya wa seli usiokuwa kabisa na kumbukumbu ya zamani. Hizo hazitakuwa na budi kuundwa mara nyingine na kujazwa humo mambo yote yaliyolingana na maisha ya Yesu ambayo yalifutiliwa mbali katika ubongo wake baada ya kufa kwake.
Tujuavyo, uhai huwa na ufahamu unamojazwa taarifa mbalimbali zinazopatikana katika mabilioni ya neva zilizomo katika ubongo.
Taarifa hiyo tena inagawanyika katika sehemu ndogondogo ngumu kufahamika zinazohusiana zenyewe kwa zenyewe za taarifa zilizohesabiwa ki-kompyuta zinazopokelewa kutoka katika kila nguvu miongoni mwa nguvu tano za kuona, kusikia, kunusa,
kuonja na kugusa.
Kama taarifa hizo zikifutika basi na uhai wenyewe unafutika. Kwahiyo, kuhuika kwa ubongo wa Yesu kunamaanisha kufanyiza kompyuta mpya ya ubongo pamoja na taarifa mpya kabisa na kadhalika humo ndani.
Matatizo hayo yatahusika pia na kemia ya sehemu nyingine za mwili wa Yesu Kristo. Ili kuhuisha mwili kazi kubwa ya kufanyiza upya itaanzishwa baada ya kukomboa vilivyokwisha oza na kupotea.
Mwujiza huo wote ukisha fanyika tayari, swali zitazuka nani alihuika na matokeo yake ni nini?
Je, ni 'mtu' ndani ya Yesu aliyehuika, ama ni 'mungu' aliyekuwamo ndani yake?
Ndiyo maana nikasisitiza kuelewa vizuri uhakika wa dhati ya Yesu.
INAENDELEA