Mtume Mwamposa kutoa pikipiki 20 kwa Jeshi la polisi Arusha kurahisisha kazi zao

Mtume Mwamposa kutoa pikipiki 20 kwa Jeshi la polisi Arusha kurahisisha kazi zao

Makanisani na misikitini tunachangia makanisa mangapi yamerudisha pesa kwa jamii kutoa huduma za bure kabisa ziwe shule,hospitali,polisi nk bure? Nitajie kanisa mojawapo linalopokea sadaka kwa waumini likatoa kitu bure kwa jamii au polisi

Naomba jina la hilo kanisa au msikiti kuwa OK tumepokea sadaka kwa jamii sasa tuirudishie jamii kiasi cha sadaka asilimia fulani ziwe za kweli au kutapeli warudishe kwa jamii bure bila kuwadai hata mia kama alivyofanya Mwamposya kwenye pikipiki
Kwa nini utoe pesa?
 
Mtume Mwamposa kutoa pikipiki 20 kwa Jeshi la polisi Arusha kurahisisha kazi zao

Hayo yalisemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda alipokuwa akihutubia kwenye kikao cha viongozi wa ulinzi na usalama Arusha

Hongera Mtume Mwamposa kwa msaada
Wakala wa kuzimu. Wapo wagonjwa wanakufa kwa kukosa dawa na wengine wanakufa kwa kukosa fedha za kufanyiwa operation za mwili nyie mnakuja kuhonga polisi utopolo! Serikali haijashindwa kuwapa polisi vitendea kazi ukizingatia ndio tegemeo lao kubwa kwenye kupora haki za wananchi za kuchagua viongozi wanaowataka. Shame on you! Bora angenunua nguo na vyakula apeleke wahitaji kama kwenye vituo vya watoto yatima
 
Serikali ina uwezo wa kugawa pikipiki kwa kila askari polisi nchini.
Hivyo tunamwomba Mwamposa aache kuwaibia mafukara na badala yake atoe sehemu ya mabilioni yake kuwapa mitaji bila masharti.
Mama abdul anagawa pkpk 700 kila mkoa kwa ccm lakini polisi wanunuliwe na mwamposa hii ni taabu
 
Mtume Mwamposa kutoa pikipiki 20 kwa Jeshi la polisi Arusha kurahisisha kazi zao

Hayo yalisemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda alipokuwa akihutubia kwenye kikao cha viongozi wa ulinzi na usalama Arusha

Hongera Mtume Mwamposa kwa msaada
Kwanini asiwape nguvu za kiroho kiroho kuudhihirishia ulimwengu kuwa roho wa Mungu ana nguvu kuliko mambo mengine yote
 
Asante kwa taarifa hii.

Asante kwa Mwamposa kulisaidia jeshi letu la polisi.

Charity begins at home!, ametoa pikipiki ngapi Kawe, Kinondoni, Dar es Salaam, hadi sasa aende na Arusha?. Isije kuwa ametoa Arusha kwa sababu ya Makonda ni RC!.
P
Charity begins at home if you want it to begin at home.
Mwamposa alliombwa atoe huo msaada na RC Makonda.Kama hao uliowataja hawana utashi na mahitaji hayo wasaidiwe kwa sababu ipi?
Sio lazima atoe Dar ndio aende Arusha.Wao wazubae na wanaotumia fursa wakishazitumia ndio unawakurupusha usingizini?
 
Huwa anawaombea wamama na wadada waweze kupata mimba, naamini next time atapeleka msaada kwenye wodi za wazazi pia, itakuwa vizuri zaidi na wana uhitaji zaidi kuliko hao polisi.

Wamama ambao ndiyo wanaunda asilimia kubwa ya waumini wake wanapitia shida nyingi sana za afya, adili nao, sio lazima iwe kikubwa hivyo ata akiweka utaratibu wa kuwafikia watu 20 mpaka 30 nayo poa tu.

Hao polisi serikali inaweza kuwanunulia tu.

Labda kama mzigo umezungushwa tu: Najinunulia maua siku ya valentine nafanyiwa delivery.
 
Asante kwa taarifa hii.

Asante kwa Mwamposa kulisaidia jeshi letu la polisi.

Charity begins at home!, ametoa pikipiki ngapi Kawe, Kinondoni, Dar es Salaam, hadi sasa aende na Arusha?. Isije kuwa ametoa Arusha kwa sababu ya Makonda ni RC!.
P
Unabariki new school which doctor kuitwa mtume ? Tumwogope Mungu jamani.
 
Back
Top Bottom