Mtumishi wa serikali ambaye Take home yake ni around Tsh 450k, 500k na kuendelea, sikia hii

Mtumishi wa serikali ambaye Take home yake ni around Tsh 450k, 500k na kuendelea, sikia hii

jozee jose

Senior Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
147
Reaction score
360
WATASHA walisema Maisha ni mipango hili ni sahihi kwa 100%, yawekana tumeshindwa kutoboa kwa kukosa mipango sahihi na kuwa na Nidhamu hafifu ya Fedha.

Muda wa kustaafu kwa mtumishi wa umma ni miaka 60 kisheria, lakini kwa hiari ni kuanzia miaka 55 hadi 59.
Sasa kwa mtu mwenye umri wa Miaka tuseme 35 atakuwa amebakiza miaka 25 hadi atakapofikisha miaka 60.
Hadi hapo utakuwa umebakiza mishahara ya thamani hii
[Miaka 25 × miezi12 × mshahara Tsh500 000] utapata Tsh 150 000 000 (150M)

Kumbuka Pesa hiyo haihusiani na PENSION kutoka mifuko ya kijamii kama PSSSF na NSSF na nk, ni pesa ambayo inapita mikoni mwako moja kwa moja.

Hii pesa inaweza ikawa kubwa saaana au ndogo inategemeana na matumizi ya mtu binafsi maana kila mtu ana partern yake.

Ninachotaka kusema kwa kupitia pesa hiyo kuna Watu wamefanikiwa kuwekeza na kupata vipato ambavyo ni (Active na passive income) Yaani utaingiza pesa kwa kuhusika na kutokuhusika kwenye mradi moja kwa moja.

Mtumishi jibaneeeee, Anzisha hata miradi ya kupanda miti kama parachichi,miti ya mbao,nunua mapori kuna sehemu wanauza ekari moja hadi 150k....Tatizo huwa tunawaza Kesho na kesho kutwa na tuna usahau uzee wetu na hutujajifunza kuandaa urithi wa Watoto wetu.

Pesa ya Pension sio pesa ya kuanzisha miradi ambayo hujawahi kufanya yaani utaishi maisha ya stress nyingi sana mara B.P mara kisukari kitafuta Kifo.

Mtumishi usiishi kinyongeeee Pesa unayo jitahidi kurahisisha Maisha,

Kila mmoja ajaribu kufanya Hesabu hiyo kutokana na umri aliobakiza kazini na Ajifanyie tathimini, Je ;pesa yake itakayoipata itamsaidia kuishi Uzee usio toa jasho?
Karibuni
 
500k ni pesa ndogo Sana kwa mahitaji ya Mtu mzima
Mtu mzima wa nchi gani?
Screenshot_20250401-214303.jpg
 
Maend
Hiyo pesa ni ndogo Sana kwa mazingira ya kitanzania
Labda kwa mwanachuo ambaye Hana majukumu ya kifamilia

500k × 12 months = 6M
6M × 25 Yrs = 150M
Hiyo pesa ni Miaka miatano ya mbunge
Maendeleo hayahusiani na wingi wa pesa moja kwa moja ni Akili za mtu...kuna jamaa anapokea 1.2 kwenye kampuni la cement lakini yeye ni pombe na wanawake
Anamaisha magumu kuliko mtu wackipato cha 200k
 
Kama umesoma vizuri nimeishasema inategemea na mtu, kwa mwingine ni kidogo kwa mwingine ni kikubwa
Nimesoma vizuri, umeandika "500,000 ni ndogo sana kwa matumizi ya mtu mzima".

Hakuna neno "inategemea" hapo...
 
Kama umesoma vizuri nimeishasema inategemea na mtu, kwa mwingine ni kidogo kwa mwingine ni kikubwa

Hiyo pesa ni ndogo kwa mtu mzima mwenye familia.au hata kijana mwenye mambo mengi.

500k
Kodi
Nauli
Chakula kizuri sio kila siku Wanga.
Mawasiliano.
Mavazi
Bills kama umeme, Maji, taka,ulinzi.
Bado Wazazi sijui ndugu.

Hiyo pesa ni ndogo Sana mkuu
 
Pesa nayo hupungua thamani.

Sidhani ten la leo hii litakua sawa kwa thamani na ten la miaka 25 ijayo
Pesa inapopungua thamani, siyo kwa mshahara wa mtumishi wa umma TU, Bali kwa Kila bidhaa..... Na kwa Kila raia....
 
Maend
Maendeleo hayahusiani na wingi wa pesa moja kwa moja ni Akili za mtu...kuna jamaa anapokea 1.2 kwenye kampuni la cement lakini yeye ni pombe na wanawake
Anamaisha magumu kuliko mtu wackipato cha 200k

Huyo ni Mmoja Kati ya Mia Moja.
Maendeleo yana uhusiano wa karibu na kipato cha mtu. Asije akakudanganya Mtu.

Wewe unalipwa 500k huwezi mshinda maendeleo mtu anayelipwa 1.5M.

Hizo mambo ya Akili ya Mtu ni hadithi tuu. Na mara nyingi ni wale exceptional.
 
Hiyo pesa ni ndogo kwa mtu mzima mwenye familia.au hata kijana mwenye mambo mengi.

500k
Kodi
Nauli
Chakula kizuri sio kila siku Wanga.
Mawasiliano.
Mavazi
Bills kama umeme, Maji, taka,ulinzi.
Bado Wazazi sijui ndugu.

Hiyo pesa ni ndogo Sana mkuu
Udogo wa pesa au ukubwa ni kichwa chako mkuu.
Kwani uliambiwa ni lazima uwe na watoto 4 hadi 5?
Kwani serikali imekuajili wewe au imeajili matumizi yako?
 
Back
Top Bottom