WATASHA walisema Maisha ni mipango hili ni sahihi kwa 100%, yawekana tumeshindwa kutoboa kwa kukosa mipango sahihi na kuwa na Nidhamu hafifu ya Fedha.
Muda wa kustaafu kwa mtumishi wa umma ni miaka 60 kisheria, lakini kwa hiari ni kuanzia miaka 55 hadi 59.
Sasa kwa mtu mwenye umri wa Miaka tuseme 35 atakuwa amebakiza miaka 25 hadi atakapofikisha miaka 60.
Hadi hapo utakuwa umebakiza mishahara ya thamani hii
[Miaka 25 × miezi12 × mshahara Tsh500 000] utapata Tsh 150 000 000 (150M)
Kumbuka Pesa hiyo haihusiani na PENSION kutoka mifuko ya kijamii kama PSSSF na NSSF na nk, ni pesa ambayo inapita mikoni mwako moja kwa moja.
Hii pesa inaweza ikawa kubwa saaana au ndogo inategemeana na matumizi ya mtu binafsi maana kila mtu ana partern yake.
Ninachotaka kusema kwa kupitia pesa hiyo kuna Watu wamefanikiwa kuwekeza na kupata vipato ambavyo ni (Active na passive income) Yaani utaingiza pesa kwa kuhusika na kutokuhusika kwenye mradi moja kwa moja.
Mtumishi jibaneeeee, Anzisha hata miradi ya kupanda miti kama parachichi,miti ya mbao,nunua mapori kuna sehemu wanauza ekari moja hadi 150k....Tatizo huwa tunawaza Kesho na kesho kutwa na tuna usahau uzee wetu na hutujajifunza kuandaa urithi wa Watoto wetu.
Pesa ya Pension sio pesa ya kuanzisha miradi ambayo hujawahi kufanya yaani utaishi maisha ya stress nyingi sana mara B.P mara kisukari kitafuta Kifo.
Mtumishi usiishi kinyongeeee Pesa unayo jitahidi kurahisisha Maisha,
Kila mmoja ajaribu kufanya Hesabu hiyo kutokana na umri aliobakiza kazini na Ajifanyie tathimini, Je ;pesa yake itakayoipata itamsaidia kuishi Uzee usio toa jasho?
Karibuni