Taribo West
Member
- Sep 6, 2020
- 29
- 59
GROUP LIMECHANGAM KA SANA, BONYEZA HII LINK uJIUNGE WhatsApp Group InviteWATASHA walisema Maisha ni mipango hili ni sahihi kwa 100%, yawekana tumeshindwa kutoboa kwa kukosa mipango sahihi na kuwa na Nidhamu hafifu ya Fedha.
Muda wa kustaafu kwa mtumishi wa umma ni miaka 60 kisheria, lakini kwa hiari ni kuanzia miaka 55 hadi 59.
Sasa kwa mtu mwenye umri wa Miaka tuseme 35 atakuwa amebakiza miaka 25 hadi atakapofikisha miaka 60.
Hadi hapo utakuwa umebakiza mishahara ya thamani hii
[Miaka 25 Γ miezi12 Γ mshahara Tsh500 000] utapata Tsh 150 000 000 (150M)
Kumbuka Pesa hiyo haihusiani na PENSION kutoka mifuko ya kijamii kama PSSSF na NSSF na nk, ni pesa ambayo inapita mikoni mwako moja kwa moja.
Hii pesa inaweza ikawa kubwa saaana au ndogo inategemeana na matumizi ya mtu binafsi maana kila mtu ana partern yake.
Ninachotaka kusema kwa kupitia pesa hiyo kuna Watu wamefanikiwa kuwekeza na kupata vipato ambavyo ni (Active na passive income) Yaani utaingiza pesa kwa kuhusika na kutokuhusika kwenye mradi moja kwa moja.
Mtumishi jibaneeeee, Anzisha hata miradi ya kupanda miti kama parachichi,miti ya mbao,nunua mapori kuna sehemu wanauza ekari moja hadi 150k....Tatizo huwa tunawaza Kesho na kesho kutwa na tuna usahau uzee wetu na hutujajifunza kuandaa urithi wa Watoto wetu.
Pesa ya Pension sio pesa ya kuanzisha miradi ambayo hujawahi kufanya yaani utaishi maisha ya stress nyingi sana mara B.P mara kisukari kitafuta Kifo.
Mtumishi usiishi kinyongeeee Pesa unayo jitahidi kurahisisha Maisha,
Kila mmoja ajaribu kufanya Hesabu hiyo kutokana na umri aliobakiza kazini na Ajifanyie tathimini, Je ;pesa yake itakayoipata itamsaidia kuishi Uzee usio toa jasho?
Karibuni
Kuwa mbunge basHiyo pesa ni ndogo Sana kwa mazingira ya kitanzania
Labda kwa mwanachuo ambaye Hana majukumu ya kifamilia
500k Γ 12 months = 6M
6M Γ 25 Yrs = 150M
Hiyo pesa ni Miaka miatano ya mbunge
Hayo makadilio ni rigid....yaani unakadilia malipo ya miaka mitatu TU na unasahau mtumishi anazaidi ya miaka 20 mbele ya utumishi.Na ndio maana kuna Hesabu zinaitwa approximation sio lazima upate figure kamili ni projection
Kitu cha kwanza katika maendeleo sio kipato ni Akili na ndio maana hiyo 500k kuna walifanya makubwa wengine bado wanalialia tu mtaaniHuyo ni Mmoja Kati ya Mia Moja.
Maendeleo yana uhusiano wa karibu na kipato cha mtu. Asije akakudanganya Mtu.
Wewe unalipwa 500k huwezi mshinda maendeleo mtu anayelipwa 1.5M.
Hizo mambo ya Akili ya Mtu ni hadithi tuu. Na mara nyingi ni wale exceptional.
Udogo wa pesa au ukubwa ni kichwa chako mkuu.
Kwani uliambiwa ni lazima uwe na watoto 4 hadi 5?
Kwani serikali imekuajili wewe au imeajili matumizi yako?
Sidhani, hebu nitajie balance diet (asili) inayozidi 10k hapa TZ.Hiyo pesa ni ndogo Sana Mkuu.
Mtu yeyote anayelipwa hiyo Hana uwezo wa Kula balance diet, kuvaa vizuri.
Atakuwa wale wa Kula Wanga zaidi kuliko protein
Bado hujasoma vizuri soma tenaaaaNimesoma vizuri, umeandika "500,000 ni ndogo sana kwa matumizi ya mtu mzima".
Hakuna neno "inategemea" hapo...
Nenda VETA, mtaani hakukufaiBado hujasoma vizuri soma tenaaaa
Kitu cha kwanza katika maendeleo sio kipato ni Akili na ndio maana hiyo 500k kuna walifanya makubwa wengine bado wanalialia tu mtaani
Ukweli unauma eee, ukikuta kitu kinakukera waachie wenzioNenda VETA, mtaani hakukufai
Maendeleo ni hatua moja kwenda nyingineAkili ni kitu kingine,
Kipato ni kitu kingine
Na maendeleo ni kitu kingine.
Ukiwa na kipato kikubwa maendeleo kwako ni uhakika hata usipokuwa na Akili kubwa.
Ukiwa na kipato kidogo hata uwe na akili kubwa bado hiyo sio Guarantee ya kuwa na maendeleo.
Sidhani, hebu nitajie balance diet (asili) inayozidi 10k hapa TZ.
ππππππ hapo sasaNashukuru kwa ushauri mujarabu mkuu wangu ila nauliza kwa ambaye ana miaka arobaini na tano sasa tufanyeje mkuu wangu π
Maendeleo ni hatua moja kwenda nyingine
Tena zipo qualitative na quantitative development.
Ingekuwa pesa nyingi ni utajiri unadhani kwa nini nchi haiprint pesa nyingi?
Kama akili huna hata upewe 500m utakuwa masikini
Maendeleo yanaendana na kujinyima hili ndo tatizo letu ,Kwa mtu mwenye Mke na watoto wawili.
Protein inatakiwa iwe nyingi kuliko Wanga.
Mfano unapokula Nyama ndio inatakiwa iwe nyingi kuliko ugali au wali.
Maziwa, mayai, maharagwe,
Matunda ni bei rahisi,
Elfu 15 kwa familia ya kawaida ya watu wanne au Watano kwa chakula inatosha kwa siku.
Hapo hujapiga mambo mengine