Mtumishi wa serikali ambaye Take home yake ni around Tsh 450k, 500k na kuendelea, sikia hii

Hiyo pesa ni ndogo Sana kwa mazingira ya kitanzania
Labda kwa mwanachuo ambaye Hana majukumu ya kifamilia

500k Γ— 12 months = 6M
6M Γ— 25 Yrs = 150M
Hiyo pesa ni Miaka miatano ya mbunge
Kwa kipato hiki English medium utaisikia kwenye tobo...........maana ukiwagusa kama wale malaika au excel wanakunyang'anya 3.5 kwa mwaka na wewe unapenda kuichapa kupita kiasi dada kakuretea watoto wazuri 3 😁 utaweza kweli kwenda na hiyo 6m au ndio utabaki kuwa chawa wa kijani na kusema mama anaupiga mwingi
 
A
Maendeleo yanaendana na kujinyima hili ndo tatizo letu ,
Tumezoea tule vitamu ingali bado ni masikini.
Hujajuliza kwa nini mtu ana kipato cha 500k wapo 2 tu alafu mwingine 200k na anafamilia kubwa, ila mlalamikaji ni wa 500k?

Huyo wa 200k ni Fukara
500k ni Maskini

Maisha ya kujima ndio umaskini wenyewe huo.
Ndio maana wenzako walisoma kozi zenye mishahara minono ili wasijinyime na kuteseka.

500k utatumia nguvu kubwa ya Akili kufikiri cha kufanya na bado uwezekano WA kushindwa ni asilimia 90 Kutokana na hiyo pesa kuwa ndogo.

Hiyo pesa Itakupa maisha ya kawaida kama Kula lakini sio chakula standard, kuvaa nguo za kawaida, kuishi mahali pa kawaida. Na
Ili usomeshe watoto sehemu nzuri lazima Ukope na uingie kwenye Madeni.
 
Hiyo sayansi kakufundisha nani kwamba "kwenye mlo kamili nyama ni lazima ipewe kipaumbele".

Ninawasi wasi na elimu Yako πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Hiyo sayansi kakufundisha nani kwamba "kwenye mlo kamili nyama ni lazima ipewe kipaumbele".

Ninawasi wasi na elimu Yako πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”

Protein ndio inapewa kipaombele kwenye Chakula
Wanga unatakiwa ule kidogo Sana

Mara Mojamoja uwe unaenda hata hotel za Nyota tano kama pale Serena Hotel uagize chakula wao wanazingatia Diet.
 
Nilifikiria kipato cha 500k nikagairi kuomba ajira sijui kama nimekosea au nimepatia nitajua mbele ya safari
 

Kimahesabu hiyo pesa ni pesa ya mboga na chakula

Kutokana na Umaskini wetu ndio tunajibana tunalazimishia matumizi mengine kama mavazi, malazi, Kodi, bills zingine, nauli, mawasiliano, Ada.

Alafu mtu anakuambia hiyo pesa ukitumia Akili unaweza kutoboa. Akili gani hapo.

Pesa ndogo, Muda unakimbia,utashangaa tuu umeshindwa
 
Protein ndio inapewa kipaombele kwenye Chakula
Wanga unatakiwa ule kidogo Sana

Mara Mojamoja uwe unaenda hata hotel za Nyota tano kama pale Serena Hotel uagize chakula wao wanazingatia Diet.
Ni nani kakukaririsha kuwa protein inapatikana kwenye nyama TU? Tena nyama zenyewe za Serena hotel (Broiler)....🧐🧐🧐
 
Ni nani kakukaririsha kuwa protein inapatikana kwenye nyama TU? Tena nyama zenyewe za Serena hotel (Broiler)....🧐🧐🧐

Wewe ndio umekariri kuwa nikitaja nyama basi ndio protein pekee.
Akili yako imeshindwa kujiongeza kuwa nyama ni mfano wa protein?
 
Mleta Uzi ana hoja nzuri sana,japokua huenda Uzi wake haujitoshelezi kufafanua in detail juu ya promotions za mtumishi atakazopata kwa kipindi cha hiyo miaka 25 aliyoipigia hesabu..lakini pia kuna semina,warsha na fursa zingine znazoweza kumuingizia kipato mtumishi nje na mshahara wa kila mwisho wa mwezi.
Ugumu au wepesi wa maisha kwa mshahara wa 500k itategemea unaishi wapi,mkoa gani,lakn kwa 500k kwa watumishi waliopo kwenye majiji hiyo pesa ni pasua kichwa,hapo lazima familia Ile wanga kwa wingi kuliko proteinπŸ˜†
Yote kwa yote,ni vyema mtumishi ukasoma mazingira na fursa zinazokuzunguka ili kuzitumia kutengeneza chanzo cha pili au cha tatu cha mapato,hii itasaidia kumudu bills mbali mbali,kuwekeza na kuishi ndoto zako. Hakuna mshahara unaotosha,ni vyema kuupunguzia mzigo mshahara kwa pesa za michongo ya pembeni...
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘ mawazo yenye Akili
 
Hiyo pesa kuna mkinga analima viazi vya chipsi njombe anaikunja kwa miezi mitatu, kwa mwaka anakunja kama hizo mara mbili. Kupanga ni kuchagua.

Huko mashambani watu wana pesa sana. Wadogo zangu bankers wanajua nini nasema.

There's time kama unalipwa mshahara wa laki 4 na huridhiki option best ni kuacha hiyo kazi ukafanye mambo ya maana hukuja kupamba dunia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…