Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Hivi na yule mtoto aliechana msahafu sijui juzuu kumthibitishia mwenzie kuwa hamna lolote walishamchinja?
 
Jee, alifanya hayo anayotuhumiwa kwa wadhifa wake kama Mtumishi wa Serikali au kama mtu binafsi? Kama hayo aliyofanya yanachukuliwa kama "hate speech" dhidi ya dini fulani au kundi fulani la imani kwenye jamii, basi Mohamed Said awe wa kwanza kukamatwa na kuswekwa gerezani.
 
Mbona wakristo na waislam wanachoma matungili na hirizi za waumini wa dini za kimila? Tena wanayaita ushirikina?
 
Wamemsimamisha kazi kwa sababu za kijinga sana.

Hilo nalo ni kosa?
Kosa kubwa sana ambalo linaweza kuigawa nchi vipande viwili. Hiyo adhabu haitoshi kabisa KUFANYA VITENDO VYA KUDHARAU DINI FURANI kunaweza kusababisha vita kati ya dini moja na nyingine. Kumbuka ishu ya kuchinja ilivyoleta matatizo makubwa miaka kadhaa iliyopita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kosa kwa sababu anasababisha migongano ambayo si ya lazima kwenye jamii. Hivi hata ukiuliza sababu ya kufanya alichofanya ni nini? Sifa tu za kijinga na utoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Kosa alilotenda halihusiani na Kazi yake, hilo nikosa kalitenda uraiani yeye Kama yeye, kisheria anapaswa kushughulikiwa Kwa utaratibu nje ya Kazi yake, hivyo ukimfukuza Kazi akaja kukushtaki anadai fidia unalipa hilo liko wazi maaana Hakuna kosa lolote alilo tenda eneo la Kazi au linalohusiana na Kazi Ya mwajiri wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikajua utaleta tafsiri kumbe na wewe umekuja na porojo.
Ndio muache kiherehere cha kupesti sheria na kuzipachika mitandaoni!

Hiyo ni taaluma ya watu wanakaa darasani miaka nane na zaidi kujifunza!

LLB miaka minne, PGLDP mwaka mzima, Ofisi ya mwansheria mkuu wa serikali mwaka mzima, LLM miaka miwili....na LLD.

Wewe mbumbumbu ngumbaru standard two failure unakimbia google unakopi na kubandika tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…