Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Shunie acha kichwa ngumu, fungulia vidume mlango

Au unaogopa uchungu, utapoamka na kuona tongotongo?

Usiwafungie kwenye chungu, na kuwapa madongo

Chako kitako km chungu, ruhusu wakitolee usongo

Mfyuuuu humuudhi mzungu, na zaid zaid mbongo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Naam,

The heading above is concerned!

Tunga shairi lenye ubeti mmoja au zaidi kwa mwanamke yeyote ambaye unampenda hapa jf.

Shairi linaweza kuwa la kimapokeo yaani lenye vina na mizani au la kisasa lisilozingatia urari wa vina na mizani...

Mimi ninamtungia Hajar, mwanamke wa ndoto zangu hapa JF.

"Nampenda msichana, Mnyange mrembo sana
Hajar ndo lake jina, hakuna wa kumfanana
Kichwani ushungi sana, nywele hutoziona
Mwanamke wa ndoto zangu, ni Hajar hakyanani "

Haya.. Tuendelee kuwatungia mashairi.. Yaani wasipoelewa kwa mashahiri haya, basi hatuna namna ingine..

==========================

Ona shairi la Psych Counselor kwa Demiss

" Demiss my love, nimekupenda siku nyingi.
Pembe langu la ndovu, lanitesa nikiona lako wigi.
Umati jf wanishangaa, napoandika shairi hili.
Uko wapi Demiss wangu, njoo ua la moyo wangu."
Duuh!

Maneno yote ya Hajar tu hayo lol.

[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
vanilla mtoto mrembo, moyoni ulishazama,
Leo nikwambie jambo, nimekupenda mazima,
sifuati mkumbo, huu uzi nimeusoma
Niwewe nikupendaye, na si avatar yako.


Ninogeshe....ninogeshe.... rahaaaaaaaa mweeeeeee. Hujapenda avatar kweli wewe?
 
moyo wangu ume lizia,
kuku penda wewe Inna
mwingine tena siwazi,
usije niumiza mtima

Nina muomba mwenyezi
maisha nikae nawe
Pendo langu mim nawe
halihitaji wapambe

Naomba sana uelewe
usi hofu wenginewe
wabaki na simulizi,
watuige wapagawe
Inna kakusikia... Haha... Hii ni tenzi siyo shairi [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duuh!

Maneno yote ya Hajar tu hayo lol.

[emoji120] [emoji120] [emoji120]
Nimpe nani maneno, matamu kama asali

Hajar ni yako haya maneno, hakika sili silali

Priority kwangu si ngono, bali upendo na kukujali

Kushika chako kiuno, hakika yanitoka akili

Mwanamke wa ndoto zangu, ni Hajar hakyanani.
 
Back
Top Bottom