Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Kwako Hassan Mambosasa

Majira hubadilika,
Miaka inasogea,
Nyasi nazo hunyauka,
Mimea kujiozea,
Lakini nina hakika,
Wewe hutonipotea.

Wewe unayo thamani,
Ya upendo ulo kweli,
U pekee duniani,
Ambaye wastahili,
Kukupa yalo moyoni,
Kwa pendo letu wawili.

Mi nawe twapendezana,
Kwa pendo lililoshiba,
Hakika tunatoshana,
Kwa dhati pia kwa huba,
Pendo tunalopeana,
Linayo tele mahaba.

Wanipa mie furaha,
U zawadi maishani,
Kuwa nawe kuna raha,
Ni raha iso kifani,
Nafurahi kwa madaha
Beti maridhawa, zenye maana sawia,
Zenye mizani sawa, mpaka ujumbe ukanifikia,
Moyo ni kawa, mengi hufunikia,
Nasema shukriya, machache umefungikia.

Ujasiri umejizazia, binti usiye na ria,
Jambo kulifikishia, pasipo udhia,
Walimwengu wakisikia, bila kukukasirikia,
Nasema shukriya, machache umefungukia.

Sina zaidi ya asante, kwa nilopokea,
Baraka nazo upate, mema yatakuneemea,
Kwa yako machache, uliyonighania,
Nasema shukriya, Demiss kwa uloniambia,

Nashindwa kuendelea, nina hofu,
Mganga ananiangalia, atanipa upofu,
Mali yake kuighania, litamtoka povu,
Nasema shukriya, Demiss kwa uloniambia
 
Hakika nakusalimu, mlimbwende Preta ,
Wewe ndiwe mahamumu, mtima nimekupakata,
Penzi lako adhimu, kwingine sitolipata,
Preta wangu tulia, baru baru uwaepuke
 
Jicho lako ni kama kobe,mgongo wako mithili ya mamba mtoa roho!
E mupenzi nikujutiae,uhali gani huko jehanam..?
figure yako namba tasa,ni kama nafungua kurasa
uangaliapo mboga huchacha,kwa tabasam swadakta!.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu hebu mtaje.

Ukikaa naye kula si vinachacha kabla ya kula sasa
 
Moyo wangu, moyo wangu unauadhibu,
Basi fanya japo taratibu!
Niondolee madhila yaliyozidia hesabu,
Utaniuwa mwana wa mwenzio!

Taratibu, twende taratibu basi taratibu,
Nitese tu kidogo ukipata sababu!
Ukizidisha moyo wangu wauharibu,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] mnanifurahisha sana leo.
 
Beti maridhawa, zenye maana sawia,
Zenye mizani sawa, mpaka ujumbe ukanifikia,
Moyo ni kawa, mengi hufunikia,
Nasema shukriya, machache umefungikia.

Ujasiri umejizazia, binti usiye na ria,
Jambo kulifikishia, pasipo udhia,
Walimwengu wakisikia, bila kukukasirikia,
Nasema shukriya, machache umefungukia.

Sina zaidi ya asante, kwa nilopokea,
Baraka nazo upate, mema yatakuneemea,
Kwa yako machache, uliyonighania,
Nasema shukriya, Demiss kwa uloniambia,

Nashindwa kuendelea, nina hofu,
Mganga ananiangalia, atanipa upofu,
Mali yake kuighania, litamtoka povu,
Nasema shukriya, Demiss kwa uloniambia
Naangalia mpira nitakujibu
 
Back
Top Bottom