Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Soma aya ya 6 inasema alichomwa sindano ya usingizi.

"Maofisa hao wa Polisi wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa waliyemchoma sindano ya sumu katika kituo cha Polisi Mitengo Wilaya ya Mtwara, Mkoa wa Mtwara, Januari 5, 2022."

Aya ya tisa 9 inasema sindano ya sumu

"Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Pascal Marungu aliieleza mahakama kuwa Mussa aliuawa na SP Kalanje Kwa kumziba kwa tambala mdomoni na puani, muda mfupi baada ya Dk Msuya (mshtakiwa wa Tano) kumdunga sindano ya usingizi."
 
Katika ilo kundi Kuna Askari mmoja Sasa hivi familia yake wanateseka Sana, yeye ndio alikuwa tegemezi kwao.[emoji17]
Na Mungu azidi kumlaani huyo askari na wenzake wote walioshiriki hicho kitendo cha kikatili, yaani anadhulumu haki za watu wengine ili kulisha familia yake,huo ni ushetani wa hali ya juu sana!!
 
Mpaka sasa hivi Bwana Mdakuzi bado sijajua point yako ni ipi,hiyo Kesi ya Zombe hao wote kina Saad,Lema,Koplo Bakari nk nilifanya nao kazi Oysterbay kabla hata Bageni hajaja kuwa OC CID,kipindi OC CID ni Mkumbo ambaye sasa hivi ni Kamishna wa Intellijensia,kwa hiyo ninaifahamu A to Z. Hukumu ya Kesi Kuu Jaji aliuambia upande wa Mashtaka wamlete muuaji ambaye ni Koplo Saad Ally kwani ndie ambaye Silaha yake ilitumika siku ya tukio full stop. Bageni amekuja kuhukumiwa baada ya Jamhuri kukata Rufaa. Hukumu ya Kesi zote mbili ipo kwenye tovuti tanzilii pitia kwa Kumbukumbu
 
Huyo dr wa polisi Msuya anajaribu kujitoa kwenye kundi la mauaji kiaina baada ya kuona limevunda. Inakuwaje umchome mtu sindano ya usingizi ili eti akiamka ndiyo aseme kila kitu. Alijua kabisa marehemu atafanywa nini baada ya kuchomwa sindano.
Soma vizuri maelezo,hakumchoma sindano.
 
Haya ndio maisha ya polisi 90%. Huwezi tenganisha polisi na dhuruma.

Ustawi wa maisha ya upolisi msingi wake mkubwa ni dhuruma. Ukiwa polisi bila dhuruma huwezi jenga nyumba nzuri, gari nzuri, maisha mazuri nk.

Maisha ya polisi yamekalia sufuria la dhuruma na damu za watu wasio na hatia.

Sijui ni lini polisi wataondokana na kuendekeza njaa
 
Mungu atulinde tu,pesa tunaipenda sana,lakini pesa hiyo hiyo ina mabalaa yake! Binaadamu wengine wabaya sana,kuna wengine wanatolewa rohoo kisa wanawake au wanaume!Dunia haada Ulimwengu Shujaa
 
Police,madactari,walimu mishahara yao iongezwe kwakweli hii hatar sana
 
Soma tena ni Sindano ya usingizi
 
Ila police wazuri pia wapo na wanafanya kazi yao kwa weledi mkubwa sana,sema tatizo lao ni kukaa kimya pale police wenzao wanapofanya maovu kwa raia!!
Kama unakaa kimya pindi uonevu unafanyika basi na wewe ni muovu tu.
 

Kama Maelezo y Grayson yaliandikwa kama ushahidi basi na alisaini na kuweka alama ya vidole basi kesi itakuwa Ngumu,nina wasiwasi kwanini Grayson amejiua? Au Ameuwawa maana yeye ndio mshikilia kesi kwa upande mkubwa na hii inatokana na kukubali maelezo ya Dr.

Je marehem Hamis alizikwa kwa siri au ilikuwaje? Huu ni msingi mwingine wa kesi.
 
Hakuzikwa mwili wake ulitupwa msituni, na walipienda walikuta mabaki yake.
 
Mostly likely !! From the picture, he seems to be regretting for all that happened !!! How could he involved himself into mess !!!?
Swali jepesi litakalozua maswali mengi "je wewe ni mtaalamu wa dawa za usingizi? I no...! Una uhakika gani kama dawa uliyomdunga ni ya usingizi na sio sumu?

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…