Nadhani ulianza kufuatilia suala hili baada ya kuanza kesi, pengine huna story ya moja kwa moja kabla ya kesi kwenda mahakamani.
Nasema hivi kutokana na story yako kwa DC Lema. Kwamba alionewa kukamatwa, wakati yeye alijisalimisha mwenyewe.
Ni kwamba, Lema ndiye aliyeendesha gari iliyopeleka miili ya waliuawa kwenye chumba cha kuhofadhia maiti, Muhimbili.
Lema ndiye aliyetoa ushahidi mzito uliofanya ACP Zombe aingizwe kwenye kesi na kuwa mshitakiwa namba moja.
Ilikuwa hivi,
Tukio lilitokea wakati Zombe akikaimu nafasi Kanda Maalum, wakati ambao Tibaigana alikuwa likizo. Yakatokea ya kutokea.
Zombe akaibuka na press akisema marehemu walikuwa majambazi. Na kwa wakati huo CPL Saad Alawi na DC Rashid Lema walishatoroka.
Saad aliwafyatulia risasi na Lema alipeleka miili Muhimbili. Baada ya kelele nyingi, Rais Jakaya Kikwete akaunda tume.
Tume iliongozwa na Jaji Ramadhan Kipenka, na ikatangaza kwa umma mwenye ushahidi aende nao. Hadi wakati huo Zombe yuko uraiani.
Lema alienda kwao Arusha, na huko akasimulia wazazi wake. Kutokana na uchamungu wa wazazi wakagoma kumwelewa.
Wakamshinikiza akatoe ushahidi kwa tume ya Kipenka. Ndipo hapo kila kitu kwenye kesi kikabadilika, alinyoosha kama huyo daktari wa Mtwara.
Na msingi wa kesi uliundwa zaidi kwa ushahidi wa Lema, kama ya Mtwara ilivyoundwa kwa ushahidi wa daktari.
Hadi suala la Msitu wa Pande ni Lema alileta. Ndiyo maana Lema alikuwa shahidi muhimu katika ile kesi na kifo chake kilitoa ahueni ya kesi.
Saad na Lema ndiyo waliokwenda kufyatua risasi hewani kwenye misitu ya Bunju ili kuunda ushahidi hewa wa kuwa wajibizana kwa risasi na marehemu.
Tume ya Kipenka ilipokea ushahidi hadi wa wezi halisi waliofanya tukio la ujambazi ambalo Zombe alisema kwenye press kuwa lilifanywa na marehemu.
Kwa hiyo;
Haya maelezo yaliyotolewa na daktari yanabaki kama msingi wa kesi huku daktari akiwa ndiye shahidi muhimu kama Lema.
Sasa tuifuatilie hii kesi hadi mwisho, na tuwe na kalamu na karatasi ya kunakili maswali ya Magafu kwa hao mashahidi ili tusichanganyikiwe na hukumu.
Ila naendelea kushauri, Magafu yuko hapo. Tusibet.
Ova