Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Wewe hujaelewa soma tena, wapi walisema ameuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu? Wamesema walishauri achomwe sindano ya sumu Dr akakataa akashauri achomwe ya Usingizi ili akiamka ahojiwe vyema, ndio walipoamua kumzima na tambala. Hizo habari umesoma wapi?
Soma aya ya 6 inasema alichomwa sindano ya usingizi.

"Maofisa hao wa Polisi wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa waliyemchoma sindano ya sumu katika kituo cha Polisi Mitengo Wilaya ya Mtwara, Mkoa wa Mtwara, Januari 5, 2022."

Aya ya tisa 9 inasema sindano ya sumu

"Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Pascal Marungu aliieleza mahakama kuwa Mussa aliuawa na SP Kalanje Kwa kumziba kwa tambala mdomoni na puani, muda mfupi baada ya Dk Msuya (mshtakiwa wa Tano) kumdunga sindano ya usingizi."
 
Katika ilo kundi Kuna Askari mmoja Sasa hivi familia yake wanateseka Sana, yeye ndio alikuwa tegemezi kwao.[emoji17]
Na Mungu azidi kumlaani huyo askari na wenzake wote walioshiriki hicho kitendo cha kikatili, yaani anadhulumu haki za watu wengine ili kulisha familia yake,huo ni ushetani wa hali ya juu sana!!
 
Nadhani ulianza kufuatilia suala hili baada ya kuanza kesi, pengine huna story ya moja kwa moja kabla ya kesi kwenda mahakamani.

Nasema hivi kutokana na story yako kwa DC Lema. Kwamba alionewa kukamatwa, wakati yeye alijisalimisha mwenyewe.

Ni kwamba, Lema ndiye aliyeendesha gari iliyopeleka miili ya waliuawa kwenye chumba cha kuhofadhia maiti, Muhimbili.

Lema ndiye aliyetoa ushahidi mzito uliofanya ACP Zombe aingizwe kwenye kesi na kuwa mshitakiwa namba moja.

Ilikuwa hivi,
Tukio lilitokea wakati Zombe akikaimu nafasi Kanda Maalum, wakati ambao Tibaigana alikuwa likizo. Yakatokea ya kutokea.

Zombe akaibuka na press akisema marehemu walikuwa majambazi. Na kwa wakati huo CPL Saad Alawi na DC Rashid Lema walishatoroka.

Saad aliwafyatulia risasi na Lema alipeleka miili Muhimbili. Baada ya kelele nyingi, Rais Jakaya Kikwete akaunda tume.

Tume iliongozwa na Jaji Ramadhan Kipenka, na ikatangaza kwa umma mwenye ushahidi aende nao. Hadi wakati huo Zombe yuko uraiani.

Lema alienda kwao Arusha, na huko akasimulia wazazi wake. Kutokana na uchamungu wa wazazi wakagoma kumwelewa.

Wakamshinikiza akatoe ushahidi kwa tume ya Kipenka. Ndipo hapo kila kitu kwenye kesi kikabadilika, alinyoosha kama huyo daktari wa Mtwara.

Na msingi wa kesi uliundwa zaidi kwa ushahidi wa Lema, kama ya Mtwara ilivyoundwa kwa ushahidi wa daktari.

Hadi suala la Msitu wa Pande ni Lema alileta. Ndiyo maana Lema alikuwa shahidi muhimu katika ile kesi na kifo chake kilitoa ahueni ya kesi.

Saad na Lema ndiyo waliokwenda kufyatua risasi hewani kwenye misitu ya Bunju ili kuunda ushahidi hewa wa kuwa wajibizana kwa risasi na marehemu.

Tume ya Kipenka ilipokea ushahidi hadi wa wezi halisi waliofanya tukio la ujambazi ambalo Zombe alisema kwenye press kuwa lilifanywa na marehemu.

Kwa hiyo;
Haya maelezo yaliyotolewa na daktari yanabaki kama msingi wa kesi huku daktari akiwa ndiye shahidi muhimu kama Lema.

Sasa tuifuatilie hii kesi hadi mwisho, na tuwe na kalamu na karatasi ya kunakili maswali ya Magafu kwa hao mashahidi ili tusichanganyikiwe na hukumu.

Ila naendelea kushauri, Magafu yuko hapo. Tusibet.

Ova
Mpaka sasa hivi Bwana Mdakuzi bado sijajua point yako ni ipi,hiyo Kesi ya Zombe hao wote kina Saad,Lema,Koplo Bakari nk nilifanya nao kazi Oysterbay kabla hata Bageni hajaja kuwa OC CID,kipindi OC CID ni Mkumbo ambaye sasa hivi ni Kamishna wa Intellijensia,kwa hiyo ninaifahamu A to Z. Hukumu ya Kesi Kuu Jaji aliuambia upande wa Mashtaka wamlete muuaji ambaye ni Koplo Saad Ally kwani ndie ambaye Silaha yake ilitumika siku ya tukio full stop. Bageni amekuja kuhukumiwa baada ya Jamhuri kukata Rufaa. Hukumu ya Kesi zote mbili ipo kwenye tovuti tanzilii pitia kwa Kumbukumbu
 
Huyo dr wa polisi Msuya anajaribu kujitoa kwenye kundi la mauaji kiaina baada ya kuona limevunda. Inakuwaje umchome mtu sindano ya usingizi ili eti akiamka ndiyo aseme kila kitu. Alijua kabisa marehemu atafanywa nini baada ya kuchomwa sindano.
Soma vizuri maelezo,hakumchoma sindano.
 
Haya ndio maisha ya polisi 90%. Huwezi tenganisha polisi na dhuruma.

Ustawi wa maisha ya upolisi msingi wake mkubwa ni dhuruma. Ukiwa polisi bila dhuruma huwezi jenga nyumba nzuri, gari nzuri, maisha mazuri nk.

Maisha ya polisi yamekalia sufuria la dhuruma na damu za watu wasio na hatia.

Sijui ni lini polisi wataondokana na kuendekeza njaa
 
Ni kweli kabisa, ogopa sana Polisi kujua kwamba una pesa, watakufuata ili wakupore pesa ulizonazo na Kisha wakuue ili kupoteza kabisa ushahidi. Nakumbuka mojawapo ya kisa kimoja cha kweli kilichotokea miaka zaidi ya kumi iliyopita ktk mkoa fulani ambao nisingependa kuutaja jina, wafanyabiashara wawili wa mifugo walikodi gari ili liwapeleke kwenye mnada wa mifugo (ng'ombe) ktk mji fulani. Wakiwa safarini njiani walikutana na gari la Polisi wa doria za barabarani, na Kisha gari la wafanyabiashara likasamishwa, walikuwapo Askari Polisi wawili tu ambao baadaye ilijulikana kuwa walitumwa na Rpc ili kuwafuatilia wafanyabiashara hao na kuwakamata kwa sababu Polisi walishatonywa kuwa wafanyabiashara hao wamebeba fedha nyingi za kwenda kununulia ng'ombe. Wale wafayabiashara walikamatwa na Kisha kwenda kuhifadhiwa sehemu fulani kwenye nyumba binafsi ya mmoja wa maaskari, hawakupelelwa kituoni. Baadaye usiku "mkubwa" aiyewatuma kazi alikuja kwenye hiyo nyumba na kuchukua 'mzigo wake' na kisha kuamuru wafanya iashara hao wote na dereva wamalizwe gari yao kwenda kutelekezwa ktk mji wa mbali karibu 80km kwenye wilaya ya jirani, na ilifanyika hivyo usiku huo huo na baadaye ilijulikana kuwa wale wafanyabiashara walikwa na Tshs. 60milioni cash. Maiti za wale wafanyabiashara walienda kuzitupa mbali kwenye mashamba ya wakulima. Walati matukio yote haya yakiendelea kulikuwa na Askari Polisi mmoja ambaye hakuwa zamu siku hiyo ambaye alikuwa akiishi kwenye mtaa mmoja wenye nyumba walikohifadhiwa wafanyabiashara waliotekwa. Askari huyo baada ya kuona gari la Polisi wa doria lenye namba za kawaida za kiraia lilikuwa linapita mara kwa mara mtaani hapo siku hiyo aliamua kulifuatilia gari hilo na mchongo huo kisirisiri bila hao Askari wenzake kujua.
Miezi michache baaaye minong'ono ya taarifa hii ilianza kusambaa mitaani, wale Askari waliopiga dili walifuatilia ili kujua nani hasa chanzo cha taarifa za kubumbuluka kwa dili lao la Siri kubwa, wakagundua kuwa ni Askari mwenzao . Ndani ya muda mfupi kabisa yule Askari alimalizwa, alikutwa amekufa nyumbani kwake na muda mfupi baadaye yule Rpc alihamishwa mkoa ule(inavyoonekana makao makuu ya Polisi walipata taarifa za dili lile). Polisi ni hatari, kaa nao mbali kama umebeba pesa cash.
.
Mungu atulinde tu,pesa tunaipenda sana,lakini pesa hiyo hiyo ina mabalaa yake! Binaadamu wengine wabaya sana,kuna wengine wanatolewa rohoo kisa wanawake au wanaume!Dunia haada Ulimwengu Shujaa
 
Police,madactari,walimu mishahara yao iongezwe kwakweli hii hatar sana
 
Soma aya ya 6 inasema alichomwa sindano ya usingizi.

"Maofisa hao wa Polisi wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa waliyemchoma sindano ya sumu katika kituo cha Polisi Mitengo Wilaya ya Mtwara, Mkoa wa Mtwara, Januari 5, 2022."

Aya ya tisa 9 inasema sindano ya sumu

"Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Pascal Marungu aliieleza mahakama kuwa Mussa aliuawa na SP Kalanje Kwa kumziba kwa tambala mdomoni na puani, muda mfupi baada ya Dk Msuya (mshtakiwa wa Tano) kumdunga sindano ya usingizi."
Soma tena ni Sindano ya usingizi
 
Ila police wazuri pia wapo na wanafanya kazi yao kwa weledi mkubwa sana,sema tatizo lao ni kukaa kimya pale police wenzao wanapofanya maovu kwa raia!!
Kama unakaa kimya pindi uonevu unafanyika basi na wewe ni muovu tu.
 
Nadhani ulianza kufuatilia suala hili baada ya kuanza kesi, pengine huna story ya moja kwa moja kabla ya kesi kwenda mahakamani.

Nasema hivi kutokana na story yako kwa DC Lema. Kwamba alionewa kukamatwa, wakati yeye alijisalimisha mwenyewe.

Ni kwamba, Lema ndiye aliyeendesha gari iliyopeleka miili ya waliuawa kwenye chumba cha kuhofadhia maiti, Muhimbili.

Lema ndiye aliyetoa ushahidi mzito uliofanya ACP Zombe aingizwe kwenye kesi na kuwa mshitakiwa namba moja.

Ilikuwa hivi,
Tukio lilitokea wakati Zombe akikaimu nafasi Kanda Maalum, wakati ambao Tibaigana alikuwa likizo. Yakatokea ya kutokea.

Zombe akaibuka na press akisema marehemu walikuwa majambazi. Na kwa wakati huo CPL Saad Alawi na DC Rashid Lema walishatoroka.

Saad aliwafyatulia risasi na Lema alipeleka miili Muhimbili. Baada ya kelele nyingi, Rais Jakaya Kikwete akaunda tume.

Tume iliongozwa na Jaji Ramadhan Kipenka, na ikatangaza kwa umma mwenye ushahidi aende nao. Hadi wakati huo Zombe yuko uraiani.

Lema alienda kwao Arusha, na huko akasimulia wazazi wake. Kutokana na uchamungu wa wazazi wakagoma kumwelewa.

Wakamshinikiza akatoe ushahidi kwa tume ya Kipenka. Ndipo hapo kila kitu kwenye kesi kikabadilika, alinyoosha kama huyo daktari wa Mtwara.

Na msingi wa kesi uliundwa zaidi kwa ushahidi wa Lema, kama ya Mtwara ilivyoundwa kwa ushahidi wa daktari.

Hadi suala la Msitu wa Pande ni Lema alileta. Ndiyo maana Lema alikuwa shahidi muhimu katika ile kesi na kifo chake kilitoa ahueni ya kesi.

Saad na Lema ndiyo waliokwenda kufyatua risasi hewani kwenye misitu ya Bunju ili kuunda ushahidi hewa wa kuwa wajibizana kwa risasi na marehemu.

Tume ya Kipenka ilipokea ushahidi hadi wa wezi halisi waliofanya tukio la ujambazi ambalo Zombe alisema kwenye press kuwa lilifanywa na marehemu.

Kwa hiyo;
Haya maelezo yaliyotolewa na daktari yanabaki kama msingi wa kesi huku daktari akiwa ndiye shahidi muhimu kama Lema.

Sasa tuifuatilie hii kesi hadi mwisho, na tuwe na kalamu na karatasi ya kunakili maswali ya Magafu kwa hao mashahidi ili tusichanganyikiwe na hukumu.

Ila naendelea kushauri, Magafu yuko hapo. Tusibet.

Ova

Kama Maelezo y Grayson yaliandikwa kama ushahidi basi na alisaini na kuweka alama ya vidole basi kesi itakuwa Ngumu,nina wasiwasi kwanini Grayson amejiua? Au Ameuwawa maana yeye ndio mshikilia kesi kwa upande mkubwa na hii inatokana na kukubali maelezo ya Dr.

Je marehem Hamis alizikwa kwa siri au ilikuwaje? Huu ni msingi mwingine wa kesi.
 
Hakuzikwa mwili wake ulitupwa msituni, na walipienda walikuta mabaki yake.
 
Mostly likely !! From the picture, he seems to be regretting for all that happened !!! How could he involved himself into mess !!!?
Swali jepesi litakalozua maswali mengi "je wewe ni mtaalamu wa dawa za usingizi? I no...! Una uhakika gani kama dawa uliyomdunga ni ya usingizi na sio sumu?

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom