Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Ile taarifa ya mauaji ya yule kijana iliniumiza sana mtu unapambana hustle zako zinajibu shimo linatema wanakuja watu na njaa zao wanakubambikizia kesi wachukue pesa zako wanaona haitoshi wanaamua kufanya ukatili wa mauaji..
Daah inasikitisha sana aisee, ukikosa msala ukipata msala. Huyu si ndo yule walienda hadi kwao kusachi na kuchukua pesa?
 
Ninamfahamu sana huyo Mkuu wa Upelelezi SP Gilbert Kalanje ambaye Shahidi anasema ndie aliyemziba na tambala Marehemu,actually nilikuwa Askari Polisi na huyo Gilbert tuliingia nae Depo moja CCP mwezi Juni 1998 na tukamaliza Februari 1999 na wote tukapangwa kazi Kituo cha Polisi Oysterbay japo mimi baadaye nilikuja kuacha kazi kwa hiari. Maisha haya Mungu tu ndie anayejua,niishie hapa NB:kwenye picha Gilbert Kalanje ni yule mwishoni kulia, alifanya sana kazi Kituo cha Polisi Oysterbay na Kituo cha Polisi Kawe
 
Sana ikizingatiwa baadhi ya polisi waovu wakitumia nafasi zao kufunika jinai zao ni hatari kwa haki za wananchi walio nje ya mfumo wa haki jinai.

Raia wanaweza kusingiziwa chochote kwa kuwa taratibu za kiPolisi zilizoandikwa ktk kijitabu chao cha muongozo wa jinsi ya kufanya kazi zao kutofuatwa kwa makusudi kabisa.

Mfano wa polisi kutozingatia hatua zote zilizoelezwa ndani ya GPO ya kuwa mtuhumiwa akikamatwa lazima mashahidi wawepo na kutiwa ktk kumbukumbu , pia mtuhumiwa akienda au kuingizwa ndani ya kituo cha polisi lazima atiwe katika register ya kituo cha polisi na pia akitolewa kupelekwa kwa ajili ya ushahidi au kuhamishwa kituo lazima irekodiwe. Kwa mfano huu mmoja, mtu mtuhumiwa anaweza kupotezwa na askari polisi waovu na isijulikane kwa urahisi amepotelea wapi kwa kuwa amekamatwa bila kufuata taratibu za GPO za kipolisi .
sio GPO,ni PGO(Police General Order)
 
Namwona mtaalam wa kesi za mauaji hapo, Majura Magafu ameshachukua kazi anayoiweza zaidi.

Ova
Majura Magafu licha ya utaalamu wake lakini kama Ushahidi umenyooka huwa anagonga mwamba,nadhani alikuwepo kwenye kuwatetea wale waliomuua Bilionea Msuya na wote walihukumiwa KUNYONGWA japo kwenye Rufaa akachomoka mmoja huku Master mwenyewe aliyefadhili Pesa ili mpango ukamilike akibaki ndani mpaka leo kusubiria Hukumu licha ya utajili wake wote. Kwa hiyo kwa kifupi Kesi hii ni ngumu kwa ndugu yangu Gilbert Kalanje. Inafanana na ile Kesi ya Zombe lakini hii ni ngumu maana Mtekelezaji wa Mauaji ndie mshtakiwa wa kwanza(Gilbert Kalanje). Ile Kesi ya Zombe Mtekelezaji wa Mauaji ya wale Wafanyabiashara na Dreva Tax (Koplo Saad)hakuwahi kukamatwa mpaka leo ndio maana Jaji aliwaachia huru kina Zombe na akawaambia Upande wa Mashtaka wamlete Muuaji Mahakamani yaani Koplo Saad
 
Ninamfahamu sana huyo Mkuu wa Upelelezi SP Gilbert Kalanje ambaye Shahidi anasema ndie aliyemziba na tambala Marehemu,actually nilikuwa Askari Polisi na huyo Gilbert tuliingia nae Depo moja CCP mwezi Juni 1998 na tukamaliza Februari 1999 na wote tukapangwa kazi Kituo cha Polisi Oysterbay japo mimi baadaye nilikuja kuacha kazi kwa hiari. Maisha haya Mungu tu ndie anayejua,niishie hapa NB:kwenye picha Gilbert Kalanje ni yule mwishoni kulia, alifanya sana kazi Kituo cha Polisi Oysterbay na Kituo cha Polisi Kawe
Kamanda mstaafu umeongea kwa code number nimekuelewa vizuri sana...
 
Natamani tu kujua yule Insp alietangulizwa je alihusika au alitaka awachome wakamleftisha
Hao manjagu ni wauaji itakua walimuua yule maana inaonekana hakuwepo kwenye deal na alitaka kusema ukweli yupo mmoja nae alitangulizwa kesi ya Zombe kama unakumbuka wanapokuangalia wakigundua pana mmoja atatoa taarifa na mgao hakupata wanakuua hao wana vina saba vya Ujambazi Sugu ila wanatumia Kodi zetu kuiba...
 
Huyo kalanje nadhani ni yule aliyemtolea nape bastola kipindi cha magu,jamaa ni jambazi anayevaa magwanda,kule mbezi malamba mawili ana hekalu ambalo aliendani na kazi yake,akishapatikana na hatia serikali itaifishe na mali zake zote ili iwe fundisho kwa watumishi wezi
 
Extremely dangerous event.
Frankly speaking from the bottom of my heart, Jeshi la Polisi Tz na TISS ni Makundi ya Kigaidi hapa nchini . Habari hii inatisha sana kupita kiasi, na hiyo ndio namna yao ya utendaji kazi. Completely taasisi hizi zimepoteza kabisa uhalali wa kuwa Majeshi ya Serikali ya nchi, ni makundi ya kigaidi.
Kwa hali hii namshauri Rais wa nchi hii akae na wataalamu huru wa masuala ya Sheria/Katiba pamoja na wataalamu huru wa masuala ya Ulinzi na Usalama ili wamshauri namna nzuri zaidi ya kulivunja Jeshi la Polisi na TISS, kuwapokonya silaha zote walizokabidhiwa pamoja na Kutangaza Hali ya Hatari kwa muda Fulani huku ukiandaliwa utaratibu mwingine mpya ulio mzuri zaidi na bora wa kuunda upya taasisi hizi.
Mkuu acha kabisa ....

Mimi nilishasema ukiwa mikononi mwa polisi ...toa ushirikiano hata kama ni uongo ...wakikulazimisha kwamba sign hapa...wewe tii amri

Usijifanye mjuaji ..ukifika mahakamani sema nililazimishwa kusema uongo...

Kuna jamaa pale Moshi mjini mpaka Leo mwaka wa 8 ..magoti yake kila mwezi yanajaa maji kwa kipigo kikali baada ya kujifanya mjuaji kituo cha polisi ... Kwamba sema Mimi Jambazi na Nina miliki silaha nyumbani ..ili maelezo yatumike kama ushahidi ..

Mahakamani ..iliona hakuna ushahidi wa moja kwa moja kumtia hatiani ..lakini tayari ana maumivu ya maisha...
Hawezi kutembea hatua 15 bila msaada wa fimbo ..huwezi kustaki polisi ..maana muundo wa haki una shida ...unaweza kujikuta unastakiwa tena kwa ujambazi...

Ndio maana ukisikia MTU kafa kituoni ..jua kwamba kuna tukio LA kilazima lilikuwa linafanyika na mtuhumiwa anaonyesha jeuri
 
Wauaji itakua walimuua yule maana inaonekana hakuwepo kwenye deal na alitaka kusema ukweli yupo mmoja nae alitangulizwa kesi ya Zombe kama unakumbuka wanapokuangalia wakigundua pana mmoja atatoa taarifa na mgao hakupata wanakuua hao wana vina saba vya Ujambazi Sugu ila wanatumia Kodi zetu kuiba...
Ukisoma Ushahidi wa huyo ACP Mgonja anaeleza kwamba siku walipomfuata huyo Dr.kwenye Zahanati kwenda kumchukua na kwenda nae kituoni kwa nia ya kumchoma Sindano Mtuhumiwa,gari alikuwa anaendesha SP Gilbert na siti za nyuma alikaa Onyango(Mkuu wa Kituo ambaye ni Mtuhumiwa namba 2, katikati alikaa huyo kijana(Marehemu)na pembeni alikaa Askari(Inspekta Msaidizi)ambaye ndie baadaye inasemekana alijinyonga Mahabusu[emoji28]kazi kwako kuunganisha dots
 
Back
Top Bottom