Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Hutu Tajiri Mussa Hamisi Hamisi atakuw amtu mzito na mtu wa chama.

Sio rahisi kesi yake kusimama hivi. Kama tulivyozoea.

Vinginevyo tunawapongeza Jeshi la Polisi na Serikaki kusimamia haki.
Mussa Hamisi hakuwa tajiri hata kidogo. Ni kizazi masikini na alikua anachimba madini shimo likatema akadhulumiwa na hao polisi wakaona itakuwa msalama wakaamua wamzime kama taa.
Sema hii kesi ina mkono wa Katelephone waziri mkubwa. Yeye ndo alifosi mpaka tume iundwe ya kufanya uchunguzi kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye alikua Kanali wa Jeshi kama sikosei.
Otherwise wangeizima kimya kimya. Polisi sio watu.
 
Kijana alipata mamilion aisee akajua ndo ametoka kimaishaa kumbe ndo mwisho wa Uhai wakeee...maisha sometimes hayapo fair kabisaa ila polisi wana tamaa mamaee yanii sio watu kabisaaa mimi bi mkubwa alikataa katu katu dogo kuwa polisi.
 
KALANJE huyu sio aliyemtolea Nape Bastola kipindi kile kuwa muelewa Ndugu,acha kufuata uzushi ulioletwa na Magazeti,yule aliyemtolea Nape Bastola hakuwa Kalanje huyu Mshtakiwa kwenye Kesi hii
Mkuu unamtetea au???
Ngoja niitazame ile clip vizuri...
Unawezekana upo sahii mkuu
 
Mkuu unamtetea au???
Ngoja niitazame ile clip vizuri...
Unawezekana upo sahii mkuu
Sasa nimtetee kwa kipi,screen shot ile picha iweke hapa kisha fananisha,ni watu wawili tofauti na wote nawafahamu,na huyu Gilbert ni Depo Mate wangu CCP 1998/1999,tukafanya Kazi wote Oysterbay Polisi kabla ya mimi kuacha kazi
 
Sasa nimtetee kwa kipi,screen shot ile picha iweke hapa kisha fananisha,ni watu wawili tofauti na wote nawafahamu,na huyu Gilbert ni Depo Mate wangu CCP 1998/1999,tukafanya Kazi wote Oysterbay Polisi kabla ya mimi kuacha kazi
Mkuu i feel ur pain.
Nina watu wangu kibao nyuma ya nondo hapa nchini na ughaibuni!!!
I can feel ur pain brother!!
 

Acha kutetea ukatili wa polisi. Polisi wanaunyama hujawahi sikia. Wewe ongea tu kwa sababu hayajakufika. Eti wewe kubali tu utakataa mahakamani. Waulize akinabowe kilichotokea. Mahakama ilikubaliana na ushahidi wa Polisi. Usichukulie mambo simple kihivyo.
 
Harafu huyo greyson alikufaje?
" Mahembe alidaiwa kujinyonga hadi kufa Januari 22, 2022 akiwa mahabusu."

Hapa ninahisi ndipo pa kutokea.

Kwenye maelezo hapo juu, Grey kaelezwa kama mtu ambaye alikuwa anajua mengi kuhusu hii kesi.

Greyson alikuwa askari na ni mtoto wa mwanajeshi mstaafu.

Namna na chanzo cha kifo chake napo ni giza kulingana na maelezo ya ndugu zake kwenye vyombo vya habari.
 
We jamaa wewe.....!!...
Kulikoni? Jaribu kuvaa viatu vya huyu kijana aliyeuawa kinyama au wazazi wake ambao wamebaki hai. Seriously, matukio ya namna hii yanauma sana kupita kiasi, usiombe yakukute au yamkute ndugu, jamaa au mtu wako wa karibu unayempenda sana. Maumivu yake ni makali sana si ya dunia hii, hayavumiliki, ndio maana unaona Hamza Mohamed alijitoa muhamga kupambana nao mpaka kufa pale Selander Bridge Dsm.
 
You must be joking. Mwanzo umeeleza kwa usahihi sana kuhusu hayo magenge. Sasa kabla hujatoa mapendekezo jiulize ni “mazingira” gani yanayofanya polisi, TISS, na vyombo vingine vya dola kuwa kama magenge ya kimafia?

Bila shaka usingetoa hayo mapendekezo kama ulivyoyatoa. Kwanza, jiulize, unawafahamuje hao unaotaka wachukue hatua? Kwamba hawaoni huo uozo? Kwamba nao unawakera sana kama wewe na wananchi wengine wanavyokereka? Kwamba they are not part of the problem IF NOT the problem itself?
 
Polisi tizii wakijuwa una hela watafanya lolote wakutemeshe
Hata yule jamaa hmza chanzo ni hiyo hiyo dhlma aliyofanyiwa sema kwa sababu hatua aliyochukua yeye ilijuwa kali sana akageuziwa kibao

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…