Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Polisi tizii wakijuwa una hela watafanya lolote wakutemeshe
Hata yule jamaa hmza chanzo ni hiyo hiyo dhlma aliyofanyiwa sema kwa sababu hatua aliyochukua yeye ilijuwa kali sana akageuziwa kibao

Ova
Ni kweli kabisa, ogopa sana Polisi kujua kwamba una pesa, watakufuata ili wakupore pesa ulizonazo na Kisha wakuue ili kupoteza kabisa ushahidi. Nakumbuka mojawapo ya kisa kimoja cha kweli kilichotokea miaka zaidi ya kumi iliyopita ktk mkoa fulani ambao nisingependa kuutaja jina, wafanyabiashara wawili wa mifugo walikodi gari ili liwapeleke kwenye mnada wa mifugo (ng'ombe) ktk mji fulani. Wakiwa safarini njiani walikutana na gari la Polisi wa doria za barabarani, na Kisha gari la wafanyabiashara hao likasimamishwa, walikuwapo Askari Polisi wawili tu ambao baadaye ilijulikana kuwa walitumwa na Rpc ili kuwafuatilia wafanyabiashara hao na kuwakamata kwa sababu Polisi walishatonywa kuwa wafanyabiashara hao wamebeba fedha nyingi za kwenda kununulia ng'ombe. Wale wafayabiashara walikamatwa na Kisha kwenda kuhifadhiwa sehemu fulani kwenye nyumba binafsi ya mmoja wa maaskari, hawakupelelwa kituoni. Baadaye usiku "mkubwa" aiyewatuma kazi alikuja kwenye hiyo nyumba na kuchukua 'mzigo wake' na kisha kuamuru wafanya iashara hao wote na dereva wamalizwe gari yao kwenda kutelekezwa ktk mji wa mbali karibu 80km kwenye wilaya ya jirani, na ilifanyika hivyo usiku huo huo na baadaye ilijulikana kuwa wale wafanyabiashara walikwa na Tshs. 60milioni cash. Maiti za wale wafanyabiashara walienda kuzitupa mbali kwenye mashamba ya wakulima. Walati matukio yote haya yakiendelea kulikuwa na Askari Polisi mmoja ambaye hakuwa zamu siku hiyo ambaye alikuwa akiishi kwenye mtaa mmoja wenye nyumba walikohifadhiwa wafanyabiashara waliotekwa. Askari huyo baada ya kuona gari la Polisi wa doria lenye namba za kawaida za kiraia lilikuwa linapita mara kwa mara mtaani hapo siku hiyo aliamua kulifuatilia gari hilo na mchongo huo kisirisiri bila hao Askari wenzake kujua.
Miezi michache baaaye minong'ono ya taarifa hii ilianza kusambaa mitaani, wale Askari waliopiga dili walifuatilia ili kujua nani hasa chanzo cha taarifa za kubumbuluka kwa dili lao la Siri kubwa, wakagundua kuwa chanzo Cha kuvuja kwa taarifa hiyo ni Askari mwenzao . Ndani ya muda mfupi kabisa yule Askari alimalizwa, alikutwa 'amekufa' nyumbani kwake, na muda mfupi siku chache baadaye yule Rpc alihamishwa kutoka mkoa ule(inavyoonekana huenda makao makuu ya Polisi walipata taarifa za dili lile). Polisi ni hatari, kaa nao mbali kama umebeba pesa cash.
.
 
Sasa milioni 60 ni hela ya kufanya ue watu kweli?
 
Sijatetea ukatili wa Polisi ...
Soma kwa makini
 
Usisite kutupa muendelezo mdau
 
Umesahau na wanaopiga wananchi wasiokua na mafunzo ya kupigana maeneo kama kwa Gwajima.
 
HII KESI BANA KUNA YULE MSHENZI ALIEMTISHIA WAZIRI WETU WA RREDIO TV NA BASTOLA SIJUI KAMA AMEACHIWA ..ALIJUMUISHWA KWENYE MAUWAJI..MSHENZI YULE
 
Yule wa Nape ni yupi katika hao
 
Akiyemtolea Nape bastola,bilashaka siyo huyo, inasemekana yupo kitengoni anapiga mzigo kama kawa.
 
Mchawi lugha
 
Harafu huyo greyson alikufaje?
Greyson wakat kesi inaanza yeye ndo alikuwa wa kwanza kukamatwa,hvyo wakubwa wakamuua akiwa mahabusu ili kuficha ushahidi
Wakasingizia eti kajiua kwa kujinyonga na tambara la dekio
BaBA greyson wakat anapokea mwili wa mwanae alisema haamin kabisa kama mwanae alijiua na alisema kuna kitu na waliomuua na wao litawakuta jambo
 
Jeshi la polisi ni jeshi la hovyo kuliko yote nchini. Sijui ni kwa nini linaendelea kufumbiwa macho. Maana linatakiwa kufumuliwa haraka na kuunda jeshi jipya, kutokana na kugubikwa kwake na kila aina ya uovu!!
 
Na baadaye kidogo, Dk Msuya anasema alimsikia Kalanje akisema huyo anawachelewesha, akachukua tambala akamziba yule kijana pua na mdomo.

Anasema baada ya Dk Msuya kuona vile aliamua kutoka nje akawaacha Karanje na wale wenzake na yule kijana akiwa amelala chini.

Lakini baada ya muda mfupi, Kalanje alimuita Dk Msuya akamuuliza, "tayari?" huku akimuonyesha yule kijana pale chini.[emoji2827][emoji2827][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulikuwa mwaka gani huu
 
Naona hata Barakoa hajavaa tofauti na wenzake.
Kwakuwa anajua yeye ndiye mshitakiwa namba 1

Amejaa hofu kupita wenzake.


Labda niwafundishe kitu kimoja.

Ukiuwa Binadamu hasa asiye na hatia kwa kumwonea ni lazima utajulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…