Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Hii inatisha sana. Kumuua kijana mdogo aliyekuwa anajitafutia kwa ajili ya maisha yake na familia yake. Taarifa hii imenipa huzuni na simanzi kubwa na kwa kweli leo nimeshindwa kula. Hawa polisi wetu ni watu hatari sana. Nilikwishaapa kuwa mtoto wangu hawezi kuwa Polisi.
 
Pale wanakula na vibaka wa k/k
 
Hao ni majambazi,wasijue una pesa,
 
Wote wanailinda ccm.sio rahisi
 

Aiseeeh! Hawa watu ni wanyama.
 
Mkuu nimeogopa,nini kifanyike ili kuwaondolea mamlaka hawa jambazi wenye unifomu?[emoji24][emoji24][emoji24]
Mfumo wa jeshi la polisi, umekaa kijqmbazi jambazi, kubadirika ni vigumu, maana, Political authority ambayo ndio inafanya oversight ya polisi, ipo corrupt na inatumia polisi hawa hawa kuumiza wapinzani, watu wote wanaopinga na kuhatarisha u tawala wao, hii polisi imeoza kuanzia juu, recruitment yenye we ni mbovu,wanaajiliwa watu wasio na akili, vilaza, Kipindi cha Omary Mahita kama IGP, Chama cha CUF kilikuwa tishio,polisi ya Mahita na ccm, wakaja na propaganda, CUF imeingiza kontena la mapanga ili kuja kuua wakristo(CUF ilipendwa Sana na wa islam).
Sasa fikiria ujambazi aliofanya Maghu na basdae Samia, kutumia polisi kuumiza, kufunga, kubambikia kesi viongozi wa chadema, na wale walifanya madudu Yale kwa amri ya ikulu, sasa hv wanaendeshwa kwenye V8 za umma! Kwa polisi kila mtu anakula kwa urefu wa kamba, we nyonga mahari ulipo, as long as wananchi hawapigi kelele, serikali, itaangalia pembeni, maana hata hao serikalini wana deals zao, chafu zinazo washirikisha polisi,
Kuna wale polisi wanaotembea na pikipiki, nilishuhudia wanamkamata bodaboda, ukiwaangalia usoni,na afya zao, tofauti yao na vibaka wa mtaani, ni uniform tu, vijamaa vina sura ngumu, afya mgogoro, swaga za kihuni,kama vivuta bangi, badala ya kumpereka kituo cha karibu wakamchukua, na kwenda nae kusikojulikana.
Kwa, ufupi, Kati ya polisi watano wanne ni majambazi ndani ya uniform, ukijikuta mikononi mwa hawa jamaa, jifanye Fala kama hauna connection na wakubwa, wanaweza kukuchapa risasi, harafu kusiwe na kesi
 
Siku zote nasemaga wabongo ni makatili sana,huyo anayesemaga
Kuna amani ni muongo
Narudia kusena,kama unavipesa
Hakikisha hawa jamaa wasijuwe
Maana kuna kundi maalum wao kazi yao kuwatisha watu na kuwatemesha pesa...

Ova
 
Ni kwamba tuombe bajeti ya camera ..
Camera zifungwe vituoni ...bila hivyo watu watapata madhara sana


Taasisi nyingi za serikali wanakwambia ‘system’ haifanyi kazi mtandao uko chini unadhani police watashindwa kuzima hizo camera ili wafanye yao? Na hawashindwi kukata umeme kabisa ili watimize yao.
 
Jeshi la polisi ni jeshi la hovyo kuliko yote nchini. Sijui ni kwa nini linaendelea kufumbiwa macho. Maana linatakiwa kufumuliwa haraka na kuunda jeshi jipya, kutokana na kugubikwa kwake na kila aina ya uovu!!


Hii sio Tanzania tu. Duniani pote police asilimia kubwa ni washenzi.

Binaadam anapopewa Mamlaka/Nafasi ya kutenda Sawa na Mungu ni rahisi sana kupoteza njia yake nae kujiona Mungu kwa maana hagusiki wala hatishiki.

Bado wapo police wengi tu waadilifu na ndio maana hii kesi imetufikia.
 
South africa tu police wao wana corruption hatari

Ova
 
Naona wengi humu tunakuja na viapo vya kutoruhusu watoto wetu kuwa police na wengine shuhuda za kuukataa u police katika makuzi yao.


Ipo namna ya kurekebisha hili, tuwafunze watoto wetu uadilifu sio tu mwilini bali mpaka rohoni.

Tuwafunze core values of humanity.

Tuwaonyeshe njia sahihi huku tukiwa tayari kuwaadhibu wanapokengeuka.

Halafu tuwape nafasi za kuwa police ili kwenda kurekebisha Mfumo uliooza tayari kwa kuwatumia wao wenye maarifa na uadilifu kutoka kwetu.

Mabadiliko yoyote hayafanywi na malaika ama majini, ni sisi wenyewe kwa kuzingatia umuhimu na manufaa ya kufanya hivyo.

Tunawalaumu police humu ndani lakini hao Jamaa ni ndugu zetu na rafiki zetu huku majumbani.

Tabia zao ni Tabia zetu.

Kipimo cha uadilifu wao ndio kipimo chetu.

Wao na sisi hakuna tofauti ni vile tu wao wamepata nafasi/arena ya kutimiza ushenzi wao.

Hawajatoka mawinguni hao Jamaa, tulikua nao na wengine tuko tunawa groom taratibu then baadae tushushe vilio kama hivi.

Utu wa mtu hujengwa na watu.
 
Kweli kabisa kama huko wanawaingiza wasiyo wadilifu
Mnategemea nini
Askari akiwa siyo muadilifu si atakuwa anashirikiana na wahalifu

Ova
 
Jeshi la polisi ni jeshi la hovyo kuliko yote nchini. Sijui ni kwa nini linaendelea kufumbiwa macho. Maana linatakiwa kufumuliwa haraka na kuunda jeshi jipya, kutokana na kugubikwa kwake na kila aina ya uovu!!
Hapana.

Kutoa hoja kwamba 'Jeshi la Polisi' lifumuliwe halafu liundwe 'Jeshi' jipya siyo suluhu, kwa sababu, ninadhani tatizo linaanza kwenye jina "Jeshi".

Kimsingi ukishaita taasisi "Jeshi" maana yake ni taasisi ya mapambano ya kivita.

Sasa swali ni je, hii taasisi yenye jina la kijeshi linapambana na wananchi au linatoa huduma kwa wananchi?

Jibu ni kwamba tunahitaji Huduma za Kipolisi (Police Services) na siyo Jeshi la Polisi (Police Army).

Tatizo lilianzia kwa mkoloni ambaye aliunda Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwanyamazisha wazalendo waliokuwa kinyume na wakoloni, na Jeshi hilo likarithiwa na Serikali, na hatimaye kazi zake zikabadilika kidogo na kuwa Jeshi la kupambana na raia badala ya kutoa huduma kwa raia ambalo ndilo lengo la Serikali.
 
Umeeleza mengi lakini na mimi nina la kusema.

Jeshi la Polisi limeundwa na sheria.

Kazi kuu ya taasisi hii ni kusimamia utekelezaji wa sheria.

Sasa wanaoajiriwa huko, kigezo cha elimu ni kwamba anatakiwa awe amepata daraja la nne (division 4) kidato cha nne.

Sasa hata ukimfunza mtoto vyema, pia inabidi umuombe afanye vibaya mitihani ili apate daraja la 4 ili awe polisi.

Hatimaye mtoto huyu ataenda kule kupata kazi, na hatoweza kutafsiri zile sheria kwa sababu hana uelewa wa masuala ya Kitaifa achilia mbali sheria.

Bado shida itakuja palepale tu kuzalisha polisi wasio na weledi
 


Tulia unisome vizuri. Husikimbilie kujibu kabla ya kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…