Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Zombe alichomoka
Zombe alikuwa mshz tu

Ova
Zombe alichomoka kwa umahiri wa Wakili tu, kwa sababu watuhumiwa wenzake wote walimtaja kuwa ndiye aliyetoa maelekezo kwa njia ya simu ya kawaida.

Kwamba kila lililofanywa kwa hao marehemu ilikuwa ni maagizo yake, na aliyekuwa akipewa maagizo hayo ni Bageni, ambaye kwa sasa anasubiri kunyongwa.

Lakini, Vodacom waligoma kupeleka ushahidi wa maongezi ya simu ya Zombe na Bageni, walisema ilipita miezi 6 walishaharibu kulingana na utaratibu wa mitambo yao.

Zombe aliponea hapo, na kwa sasa anakula matunda yake ya ustaafu.

hivi ajafa....?
 
Mpaka sasa hivi Bwana Mdakuzi bado sijajua point yako ni ipi,hiyo Kesi ya Zombe hao wote kina Saad,Lema,Koplo Bakari nk nilifanya nao kazi Oysterbay kabla hata Bageni hajaja kuwa OC CID,kipindi OC CID ni Mkumbo ambaye sasa hivi ni Kamishna wa Intellijensia,kwa hiyo ninaifahamu A to Z. Hukumu ya Kesi Kuu Jaji aliuambia upande wa Mashtaka wamlete muuaji ambaye ni Koplo Saad Ally kwani ndie ambaye Silaha yake ilitumika siku ya tukio full stop. Bageni amekuja kuhukumiwa baada ya Jamhuri kukata Rufaa. Hukumu ya Kesi zote mbili ipo kwenye tovuti tanzilii pitia kwa Kumbukumbu
Point yangu ni kwamba kwenye kesi za askari wa Jeshi la Polisi kuua raia, tusitarajie sana hukumu ya kuadhibu askari.

Na kesi ya ACP Abdallah Zombe na wenzake 11 ni moja ya mifano ambao nimeona unafanana mno na kesi hii ya Mtwara.

Ova
 
So sad,hii dunia Basi tu.Binafamu wamekuwa zaidi ya Simba.Kwangu nilishatangaza kwa wanangu sitaki waje wafanye hiyo kazi ata siku moja.Ni kitu kibaya Sana.
 
Extremely dangerous event.
Frankly speaking from the bottom of my heart, Jeshi la Polisi Tz na TISS ni Makundi ya Kigaidi hapa nchini . Habari hii inatisha sana kupita kiasi, na hiyo ndio namna yao ya utendaji kazi. Completely taasisi hizi zimepoteza kabisa uhalali wa kuwa Majeshi ya Serikali ya nchi, ni makundi ya kigaidi.
Kwa hali hii namshauri Rais wa nchi hii akae na wataalamu huru wa masuala ya Sheria/Katiba pamoja na wataalamu huru wa masuala ya Ulinzi na Usalama ili wamshauri namna nzuri zaidi ya kulivunja Jeshi la Polisi na TISS, kuwapokonya silaha zote walizokabidhiwa pamoja na Kutangaza Hali ya Hatari kwa muda Fulani huku ukiandaliwa utaratibu mwingine mpya ulio mzuri zaidi na bora wa kuunda upya taasisi hizi.
Wazo lako ni jema.

Umeshauri bila kuelewa ukuu wa mamlaka na nguvu Serikali iliyonazo.

Unakumbuka maasi ya Tanganyika Rifles mwaka 64?

Nini Serikali ilifanya baada ya jaribio hilo kuzimwa?

Kulivunja jeshi la Polisi ama Tiss ili kuondosha staff wake wote, ni jambo rahisi sana kama kung'oa ubua Serikali ikiamua.

Serikali ina uwezo wa kufukuza wote bila kubakisha hata mmoja kwa kukodi Polisi trainers na staff wengine kutoka ughaibuni kushika nafasi zao kwa muda itakaouona unafaa na hakuna madhara yoyote ya kiusalama yatakayotokea.

Mwaka 64 Jwtz(then TR) walipomletea dhihaka Nyerere alifukuza wote na kukodi wanajeshi kutoka Nigeria kuja kulinda nchi, waliorejeshwa walifanyiwa vetting upya.

Na katika kurejeshwa, walikuwa wakiitwa mmoja mmoja kwa barua binafsi na siyo tangazo, na walioonekana vinara ama kuhusika kwa namna moja ama nyingine walifukuzwa mazima ama kutiwa jela na hakuna kitu walifanya.

Nadhani huu uozo unaofanywa na vyombo hivi vya dola vyenye dhima ya kulinda uhuru wa wananchi na mali zao, kuna baraka toka kwa viongozi wa kitaifa.

Wasingekuwa wanaridhishwa na hali iliyopo sasa ya sikio la kufa lisilosikia dawa, wasingelifumbia macho ili hali mambo yote ya hovyo wanayotendewa wananchi yanaendelea na yapo wazi wakati uwezo wa kufanya dharula ya mageuzi wanao.
 
sidhani kama atakujibu sijawahi kuona askari akimponda mwenzie awa watu wamenyweshwa sumu mbaya sana. all in all wapo waadurifu akiweno baba yangu.

ambae zaidi ya kumiliki baiskeri na pikipiki ya jeshi hana cha maana. kijumba chake kina karibia kudondoka muda wowote,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji24][emoji24][emoji24]

ukilinganisha na watoto wa juzi namba J...wana magari na nyumba za ufahari.

nahisi kengemajikwetu ulikuwa namba E au F. vile vile wewe jamaa una kauadirifu sana ndio maana uliweza kuachana na jeshi la majambazi.​
Kijana,mimi ni namba E ya mwisho hivyo hata Depo yetu tulimalizia namba E kisha wengi walipata namba F,niliacha Kazi nikiwa na nyota moja (Assistant Inspector),kuhusu Kalanje alikuwaje tukiwa kazini jibu ni kwamba alikuwa Askari wa kawaida,sasa huko kwenye kupanda Vyeo na kuwa na maamuzi ndio wengi huwa wanabadilika hivyo sijui maana mimi nilipoacha kazi nilikuja zangu Nje ya Nchi kufanya kazi hivyo sijui na yeye alivyoanza kupanda Vyeo alikuwaje.
Hata huyo ACP Mgonja aliyetoa Ushahidi nae ni Depomate wetu. Yote kwa yote hii ni AJALI KAZINI kama zilivyo ajali nyingine tu
 
Mkuu babu yangu pia aliwaambia watoto wake hivyohivyo pia kiufupi agizo kutoka juu hatutakiwi kua mapongo
Babu yangu pia Ali laani hii kazi kwenye ukoo mzima tuliwai kua na askari police mmoja ila mwisho wake ulikua mbaya Babu yetu marehemu alipenda kuita kazi ya kolokoloni....................

Niseme wazi police wengi ni watu wa dhulma sana sanaa nimekaa na brother angu nimeshuhudia mengi sanaa na akafukuzwa kazi na kuishia maisha ya kutangatanga.......

Hiki kisa kina sikitisha na kuhuzunisha sanaa uroho, wa pesa na Mali Hawa ndio walinzi wetu wa amani....
 
Cjajua babu zetu walitendewa nin na mapongo ila ila tu itoshe kusema wale jamaa ni zaid ya wanyama ungia mikononi mwao na usiwe na watu wakukupigania nimewah kushuhudia kwa macho yangu nikiwa kwa mahabusu zao ni vile tu nilikua na backup ya wanene nyuma yangu ila wahuni wanyonge chamoto wanakiona
 
Kama unakaa kimya pindi uonevu unafanyika basi na wewe ni muovu tu.
Huwa wanaogopa kuuwawa na wenzao pindi watakapo sema ukweli, kama huyo afande aliyekutwa kajinyonga Mahabusu ya police, ameponzwa kwa kusema ukweli wa tukio zima!!
 
Kijana,mimi ni namba E ya mwisho hivyo hata Depo yetu tulimalizia namba E kisha wengi walipata namba F,niliacha Kazi nikiwa na nyota moja (Assistant Inspector),kuhusu Kalanje alikuwaje tukiwa kazini jibu ni kwamba alikuwa Askari wa kawaida,sasa huko kwenye kupanda Vyeo na kuwa na maamuzi ndio wengi huwa wanabadilika hivyo sijui maana mimi nilipoacha kazi nilikuja zangu Nje ya Nchi kufanya kazi hivyo sijui na yeye alivyoanza kupanda Vyeo alikuwaje.
Hata huyo ACP Mgonja aliyetoa Ushahidi nae ni Depomate wetu. Yote kwa yote hii ni AJALI KAZINI kama zilivyo ajali nyingine tu
dah hongera sana nahisi mliingia mkiwa na elimu from form 6 and above. historia yako inafanana na rafiki wa baba yangu ambae walifanya wote kozi ya polisi mwaka 88-89 wao ni namba D ile ya kati kati sio ya mwanzo na sio ya mwisho. huyu rafiki yake alivyoona jeshi lina mzingua ukizingatia kipindi hicho mishahala ilikuwa midogo.

ujambazi nje nje. manjagu walikuwa wanafanya😭😭😭 huyo rafiki wa baba yangu ambae nadhani alisomeaga mambo ya financial alitimkia zake Marekani akajiunga na jeshi huko.

mkuu kama kuna kichance huko ebu tusaidieni na sisi tulio huku nyumbani msisahau mlipo toka🙏​
 
Kitendo hiki kilichofanywa na hawa askari wa Mtwara na wale wa Zombe wakati ule, na wengi wa aina kama hiyo ni sehemu ndogo ya ushenzi, uonevu, ukatili na uovu mkubwa unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia wake nchi nzima. Ni bahati tu kwamba kesi hii imefika hapa kwasababu ya nguvu ya mkono wa kiongozi kigogo mmoja serikalini,vinginevyo hii nayo ingeishia chinichini kama zilivyo kesi nyingi zingine zilizopita.

Jambo la kusikitisha ni kwamba matendo ya kiovu yanayofanywa na jeshi la polisi ni 'reflection' ya jamii nzima ya kitanzania ilivyo kwa sasa, lakini ukigeukia sekta zingine mambo yako hivyo hivyo - yaaani ni ukatili, uonevu na uovu kwa kwenda mbele. Matendo ya polisi hawa hayana tofauti na wayafanyayo maofisa wa TRA wanapowafanyia dhuluma wafanya biashara, hayana tofauti na baadhi ya walimu, wahadhiri wa vyuo vikuu wanaotoa alama na ufaulu kwa rushwa ya fedha na ngono kutoka kwa wanafunzi, hayana tofauti na raia wa kawaida mashuhuda wa ajali badala ya kuwaokoa majeruhi wa ajali ya gari lakini badala yake wanawapora majeruhi hao fedha zao, simu zao wakiwa mahututi, hawana tofauti na mwananchi aliyetumiwa fedha kwa simu kwa makosa na hata pale anapoambiwa kwamba rudisha au toa ushirikiano hataki na harudishi fedha hizo, hawana tofauti na maofisa ardhi wanafanyia kila aina dhuluma wananchi kuhusu haki zao za ardhi. Hawana tofauti na viongozi wanaoendesha Ma -V8 wasio na shida na wala wasioathirika na mgao wa umeme, upungufu wa maji lakini wala hawana hata chembe ya huruma na wananchi wanaotaabika na shida zinazoweza kutatulika kwa haraka.

Wanaotoa mawazo ya kulivunja jeshi la polisi, inabidi pia watafakari kuvunja TRA, NHIF, Halmashauri zetu, maana hizo ni vichaka vilivyojaa uonevu na kila aina ya uovu kila kukicha.
 
Kijana,mimi ni namba E ya mwisho hivyo hata Depo yetu tulimalizia namba E kisha wengi walipata namba F,niliacha Kazi nikiwa na nyota moja (Assistant Inspector),kuhusu Kalanje alikuwaje tukiwa kazini jibu ni kwamba alikuwa Askari wa kawaida,sasa huko kwenye kupanda Vyeo na kuwa na maamuzi ndio wengi huwa wanabadilika hivyo sijui maana mimi nilipoacha kazi nilikuja zangu Nje ya Nchi kufanya kazi hivyo sijui na yeye alivyoanza kupanda Vyeo alikuwaje.
Hata huyo ACP Mgonja aliyetoa Ushahidi nae ni Depomate wetu. Yote kwa yote hii ni AJALI KAZINI kama zilivyo ajali nyingine tu
lakini kingine baba. ujue hii insure imebumburuka tu. enzi za mishahala kiduchu ujambazi ulikuwa unafanywa tena na wanausalama. kuanzia hiyo miaka yenu mnaajiliwa 1999 kurudi nyuma.

majambazi walikuwa wanatumia silaha kali za moto ambazo zilikuwa zinamilikiwa na serikali. kwa nchi yetu kama unavyoijua kuna baadhi ya silaha mtu binafsi awezi kuimiliki labda awe fisadi miongoni mwa mafisadi.

na nchi yetu hakuna kitu kigumu kama kupata kibari cha silaha yoyote hata hizo zenye uwezo mdogo.

ila zama hizo za uvamizi watu walikuwa na silaha za kivita. 😭😭😭

askari walikuwa na maisha magumu sana. nakumbuka niliwahi kusimuliwa na mzee wangu kuwa waliwahi kumpoteza depo mate mwenzake kwenye tukio la ujambazi ambao huyo depo mate walivamia benki hapo posta. askari waliopo zamu akiwemo baba wakapokea taarifa za benki hiyo kuvamiwa.

bahati haikuwa nzuri kwa wavamizi kwani asilimia 90 walikuwa askari.

kikosi cha askari kilichoenda kuokoa kiliongozwa na baba yangu. walitoa rai kuwa watekaji wajisarimishe lasivyo nguvu ya ziada itatumika endapo watakaidi😭😭😭

yakatokea majibishano ya risasi. Polisi waliwazidi nguvu watekaji wakafanikiwa kuwamiminia Risasi. baada ya hali kuwa shwali.

baba anasema alipo enda kukagua zile maiti za watekaji hakuamini alipo muona depo mate wake. walio maliza chuo cha polisi pamoja. wakapangiwa Dar es salaam pamoja na nyumba wakawa wanaishi nyumba moja.

kibaya zaidi kilicho muuma sana baba ambacho hadi leo anakikumbuka silaha yake ndio iliyotumika kumshambulia rafiki yake.😭😭😭.

siku hizi hali ni shwari sana​
 
Back
Top Bottom