Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Dah ajira za watu wengi sana zimepotea maana akiwa na 25 aliweza miliki hizo pesa huyu angefika 40yrs angekuwa kaajili vijana wengi
 
Makosa mfanye nyie halafu aulizwe waziri!?

Huyu IGP ni jambazi tena sugu,achukuliwe hatua maana watu wengi sana wamekufa na kudhulumiwa kupitia yeye
 
inamana habari kamili nikanunue gazeti la mwananchi au raia mwema
hilo gazeti la kwanza habari imejitosheleza kabisa, kama unatumia simu zoom usome kwenye maandishi mekundu baada ya heading jinsi plan ilivyofanyika.

au rudi 1st post moderators wameiweka sawa.
 
Polisi wameanza kuchezea kesi, aliyejinyonga mahabusu ni afisa wao, hapo mahabusi alikuwa peke yake? Mahabusu imekuwaje na mazingira ya mtu kujinyonga? Haki ya huyu mfanyabiasha itapotea tusipoliangalia ili suala, wanatengeneza story sasa
Watasema yule aliyejinyonga ndo alimuua jamaa... Ajabu ni kwamba ishu ya Mbowe Sirro aliweza kuiongelea japo kesi ipo mahakamani, lakin ishu ya polisi walio chini yake anaona ni ishu ya waziri
 
Huyo muhudumu wa benki naye atambulike.
 
===
Maofisa saba wa Jeshi la Polisi, wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Mtwara kwa tuhuma za kumpora mfanyabiashara mmoja wa madini TZS 70 milioni,

Taarifa zinasema kuwa baada ya kumpora mfanyabiashara huyo kisha wanadaiwa kumuua kwa kumchoma kwa Sindano ya sumu na kuutupa mwili wake Bahari ya Hindi.

Taarifa zaidi zinatanabaisha kuwa hata hivyo, wakati polisi hao wakiwa mahabusu mkoa Mtwara wakisubiri kufikishwa Mahakamani,

Maajabu mengine toka kwa polisi hao wauaji eti mtuhumiwa mwenzao mwenye cheo cha Mkaguzi wa msaidizi wa Polisi,

Grayson Gaitan Mahembe huyu anadaiwa kujinyonga Januari 22, 2022 akiwa ndani ya chumba cha mahabusu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimesambaa maiti ya askari huyo tayari imeshasafirishwa kutoka Mtwara na kupelekwa nyumbani kwao Tabata Segerea jijini Dar es Salaam kwa maziko.

Wanaodaiwa kushikiliwa na polisi kwa mahojiano ni Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Polisi wa Wilaya (OC-CID) Mrakibu wa Polisi (SP) aliyetajwa kwa jina moja la Kalanje,

Mkuu wa kituo (OCS) Charles Onyango, Nicholaus Kisinza wa kitengo cha intelijensia na wakaguzi wanne wa Polisi.

Juhudi za Mwananchi kupata undani wa sakata hilo ziligonga mwamba baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mark Njera kutokuwa tayari kulizungumzia.

Licha ya mwandishi kumfuata ofisini kwake, RPC huyo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo hadi atakapoitisha mkutano na waandishi wa habari.

Hata hivyo, RPC Njera hakuwa tayari kueleza ni lini ataitisha mkutano huo wa waandishi wa habari

Naye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillus Wambura alipoulizwa kwa simu alimtaka mwandishi kurudi kwa RPC Njera.

“Hii issue (suala) hata kama ingekuwa kubwa kwa vipi ni issue ya mkoa, msemaji wa mkoa ni Kamanda.

“Nadhani kama Kamanda atakuwa na press (mkutano na wanahabari) sijui kama atakuwa tayari kuongea na chombo kimoja kimoja, sidhani.

Kwa hiyo endeleeni kucheki kama atakuwa na press itakuwa lini,” alisema DCI Wambura.

Vyanzo mbalimbali vya uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, vinadai mauaji hayo yanadaiwa kufanyika katika hospitali ya Jeshi la Polisi Mtwara mjini Oktoba mwaka jana, lakini taarifa za mauaji hayo zikavuja kuanzia wiki iliyopita.

Mazingira ya tukio hilo yanafananishwa na mauaji ya wafanyabiashara watatu wa Mahenge mkoani Morogoro, Sabinus Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva taxi Juma Ndugu walioua kwa risasi Januari 14|2006.

Wafanyabiashara hao,walikamatwa na Polisi eneo la Sinza Palestina jijini Dar es Salaam wakibambikiwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, na kisha kupelekwa msitu wa Pande na kupigwa risasi.

Tayari Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam ilishamhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, aliyekuwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni na jitihada za kujinasua na kitanzi zimekuwa zikigonga mwamba.

Taarifa za mauaji Mtwara
Taarifa zinadai kuwa Oktoba mwaka jana, mmoja wa watuhumiwa saba wanaoendelea kushikiliwa, alikwenda kwa Kaimu mkuu wa Upelelezi mkoa (RCO), na kumjulisha kuwa huko Nachingwea kuna mfanyabiashara ameuza madini.

“Huyo mkaguzi alimfuata bosi wake na kumweleza hayo kwamba huyo jamaa (marehemu) ana pesa nyingi inaonekana ameuza madini.

Walitengeneza mazingira kwa kushirikiana na watuhumiwa wengine na kumkamata,” kilidai chanzo kimoja.

Chanzo hicho kimedai kuwa baada ya kumkamata, polisi walifanya upekuzi katika nyumba yake na kumkuta na Sh70 milioni na kumchukua pamoja na fedha hizo na kwenda naye Mtwara mjini ambako walimweka mahabusu kwa siku tatu.

“Baada ya siku tatu walimwachia bila masharti lakini wakawa wamebaki na zile pesa zake sasa alipotoka akakutana na ndugu yake, akamwelezea huyo ndugu yake akamwambia kama wamekuachia twende ukadai vitu vyako,” ilielezwa.

Inadaiwa kuwa alivyofika polisi, Mkuu wa kituo (OCS), Mkuu wa Upelelezi Wilaya (OC-CID), Kaimu RCO naMkuu wa Intelijesia (RCIO) wakamkamata tena na kumshikilia kwa mahojiano huku ndugu aliyemsindikiza akibaki nje.

“Huyo ndugu yake baada ya kuona jamaa hatoki alienda kumwangalia kule ndani polisi akakuta kama wanahojiwa hivi akarudi nje lakini baada ya muda alipata SMS (ujumbe mfupi) kutoka kwa ndugu yake akimjulisha kuwa ameachiwa.”

Hata hivyo, tangu siku hiyo mfanyabiashara huyo hakuonekana tena hivyo ndugu wakawa wanaendelea kufuatilia kwa kuwa mara ya mwisho alikuwa mikononi mwa polisi, hivyo wakawa wana shuku kuwa kuna jambo huenda limemtokea.

“Wanasema damu ya mtu ni nzito. Imekuwa siri tangu Oktoba lakini wiki iliyopita ndio kukaanza fununu kwamba polisi walimuua na ndipo uchunguzi ukaanza hadi kuwalenga hao maofisa wa Polisi,”kilieleza chanzo chetu.

Taarifa hizo zinadai kuwa mmoja wa maofisa wa polisi mwenye cheo cha mkaguzi wa Polisi ambaye naye ni mtuhumiwa, alipobanwa na makachero inadaiwa alifunguka kila kila, nani walioshiriki na mwili walipoutupa baharini.

“Ndio sasa ikagundulika kumbe siku ile hata ile SMS kwamba ameachiwa haikutumwa na marehemu bali mmoja wa watuhumiwa.

Baadaye walimchukua hadi hospitali ya polisi huko ndio walimchoma sindano ya sumu”
Inaelezwa kuwa askari aliyejinyonga akiwa mahabusu, ndiye anatajwa kuwa alinyoosha maelezo ya tukio zima lilivyokuwa, nani wahusika na wapi mwili ulipotupwa, lakini amejinyonga baada ya kufanikisha uchunguzi huo.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka Mtwara zilieleza kuwa tayari mabaki ya mwili wa mfanyabiashara huyo, yamepatikana na unafanyika uchunguzi wa vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kama ni mwili wake ili upelelezi uende hatua ya pili.

Source : Mwananchi
 
Kwa polisi utasikia wamekutwa hawana hatia. Marehemu alikuwa na tatizo la pumu.
 
Watasema yule aliyejinyonga ndo alimuua jamaa... Ajabu ni kwamba ishu ya Mbowe Sirro aliweza kuiongelea japo kesi ipo mahakamani, lakin ishu ya polisi walio chini yake anaona ni ishu ya waziri
Polisi inahitaji kufumuliwa na kuundwa upya. Hili ni moja tu ambalo limetufikia, je mangapi yanayokea na hayawi reported
 
ukiachilia kukubandikizia kesi nzito wajinga hawa walivo na tamaa wanakuua kweli na unapotea hivi hivi nashukuru Mungu hawa kenge dili limebuma ...

yaani hata mimi wangenipatia nafasi mwaka 2020 wangeniua ni Mungu tu alikua hajataka

nawachukia Polisi jamani sijui hata nielezeje
 
Nazidi kuamini kuwa huku duniani kuna binadamu wana roho mbaya sana:

- Kijana kahangaika kuchimba madini kapata hela inajitokeza mibaba yenye familia zao tena imeshafanya kazi miaka mingi polisi na ukute yana.

heshima zao kuanzia ndani ya familia zao, koo zao, mitaani kwao, misikitini/makanisani kwao, kwenye jamii kwa ujumla n.k. inaenda
kumnyang'anya pesa zake. Na kwa kuwa tamaa imezidi inaenda mpaka nyumbani kwa kijana Nachingwea kuchukua hata kile kidogo
kilichobaki.

- Kama hiyo haitoshi wanaenda kufanya ukatili na mateso yasiyosemekana kwa kijana wa watu kwa kumpiga sindano ya sumu ili kupoteza.

ushahidi. Haki ya Mungu hakuna kitu kimeniumiza na kuniharibia siku yangu kama kujua huyu kijana aliuwawa kikatili kiasi hiki. Si
wangechukua tu hela wamwachie uhai wake basi kijana wa watu angehangaika upya na maisha? Hivi leo wanarudishaje uhai wake? Je
wategemezi wake wapo kwenye hali gani? Hivi milioni 70 kweli ziwafanye mtoe roho ya mtu? Halafu askari wenyewe wapo zaidi ya saba.

maana yake mgawo si zaidi ya milioni kumi kwa kila mmoja je ndio gharama ya kuto uhai wa mtu? Serious unamdunga mtu sindano ya sumu.

ili upate milioni kumi tu? RIP kijana mhangaikaji umepitia mateso makali kwa sababu ya tamaa na roho mbaya ya watu waovu kabisa.
- Hili limejulikana wazi je ni watru wangapi wamepoteza maisha kwa mtindo huu au zaidi ya huu?

Ukweli mchungu kwa viongozi waliopo madarakani jeshi la polisi linatakiwa kufanyiwa mageuzi (sio lazima kulivunja) makubwa sana kwani askari walio wema wanachafukliwa na askari walio waovu. Na mkiendelea kufunga macho ipo siku kama sio nyie basi hata ndugu zenu watakuja siku moja kukutana na dhaham la hawa jamaa.

Hebu mtafuteni IGP Mangu (kama sikosei mara ya mwisho alipewa ubalozi au ofisa ubalozi nje) aliyehudumu kwa muda mfupi sana kwenye nafasi yake awasaide kuwavusha kwenye kipindi cha mpito.

Huyu Mangu mimi namkubali binafsi kwa sababu alikataa kupelekeshwa na wakuu wake tenda kile kipindi kigumu hasa ili atende kinyume na sheria badala yaje alisimamia taaluma yake wakaishia kumnyang'anya cheo chake.
 
imekuwa too much watu kuuwana yani ukilala ukiamka unasikia watu watano mara wawili mara watat umara sijui wangapi yani kuuwana kumezidi mipaka Mungu atufungue ufahamu wetu
 
Ndo maana braza Hamza akaamua kufanya yake.
Wakampa na cheo Cha ugaidi.
Sasa utokee kichaa kama wewe walioua wengine, unakwenda kulipa kisasi kwa wengine!!!kwanini wasipasue bichwa lako na kupewa cheo cha juu kabisa cha mujahidin???

Hata kama ulikuwa na maumivu ya msingi kwa kudhurumiwa na polisi utaonekana mbwa tu mbele ya jamii.
 
unawachukia ila wenzako wanaishi vizuri kisa wao, Usimchukie mtu ambaye huwezi hata muumba chukia tabia zake mbaya tu
 
Hicho kipindi cha mwenda ndicho kipindi cha jk sio??

Ambacho ungeweza kubakwa na usifanye chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…