Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

hakuna shida kwa kijana wa 25yrs kumiliki 33mili tena mfanyabiashara ya madini..

kumbuka wengine wakimaliza lasaba tu wanaingia mtaani kutafuta, wengine form four inatosha... machimboni lolote linaweza kutokea kadili ya uhangaikaji wako na bahati..
 
RPC Mtwara aliutangazia umma kwamba kuna askari 7 wamepandishwa kizimbani wakishtakiwa kwa kosa la kumuua kijana mfanyabiashara wa madini musa hamisi huko mtwara.

Aidha kuna taarifa kwamba askari mmoja aliyekuwa mmoja wa watuhumiwa hao alijinyonga wakati wakiwa mahabusu kabla ya kupandishwa kizimbani.

Kwanini taarifa ya huyo RPC haikueleza kwamba walikamatwa na kuwekwa mahabusu askari 8 ila mmoja alijinyonga wakiwa mahabusu hivyo saba tu ndio wamepelekwa mahakamani.

Halafu kuna taarifa kwamba huyo aliyejinyonga (kama kweli alijinyonga au alinyongwa na wenzake) alikuwa na taarifa za kina kuhusu hilo sakata.

Halafu inawezekana vipi mtuhumiwa ajinyonge akiwa mahabusu?

Isije ikawa mambo ya kupoteza ushahidi kama ishu ya kina zombe.

RPC mtwara inabidi awajibishwe
 
Ila jeshi la polisi inabidi libalike, baadala ya kulinda raia wao wamekua sehemu ya kuua raia.
 
Hawawezi kuwa wapumbavu kiasi hiki,kwamba wamuue mtu kwa milioni tano kila mtu.

There is something behind that amount of money.
Hiv polis unawachukuliaje ndugu? Yaan ni wapumbavu mno tena zaidi ya hata neno lenyewe, polis anauwezo wa kukuua kwa ajili ya 5k, sijawah kumkubali askar polis maisha yangu yote, yaan siwapendi kiiiinyama.
 
Katika nchi yetu hii kumkuta kijana wa miaka 25 ana milioni 33 si jambo dogo, kijana alikuwa ni mfanyabiashara wa madini lakini huenda vitu kama mtaji wa boashara alipigwa jeki na mzazi.

Huenda kijana huyo ni mtoto wa mtu mzito kama Rpc wa mkoa flani, Ocd, mwanajeshi mwenye cheo, mwanasiasa, n.k.

Kiufupi huenda kuuawa kwa kijana huyo mdogo kulifanywa bila kujua mzazi wake ni nani, Uchungu wa mtoto anaeujua ni mzazi aisee!! kuna watoto sio hata wa kuwagusa maana kitachokukuta hata kazi yako unayoona inakulimda haitakusaidia.
Umeshaenda kwa wakulima wa vitunguu na Miwa ama mchele. Kuna vijana ni matajiri wa kutupwa wanamiliki pesa nyingi sana milioni 33 ni pesa ndogo mno kama una goli la maana. Ila ukweli kuna watu wengi sana wanakufa mikononi mwa haya mapolisi majizi. Kwa hili hata RPC wamtoe tu.
 
Jeshi Linakwenda Kumuua Mtu Mmoja Kwa Silaha Nzito Kisa Millions 70
Ambazo Raia Mwema Kazitafuta Kwa Jasho Lake
Ndiyo Maana Baadhi Yao Ukiona Wana Nyumba 5
Gari, Biashara, Wanalima Kumbe Kazi Kubwa Uporaji Wa Raia
 
Kwani ilikuwaje hadi huyo kijana kufa, uzi hauna nyama.
 
Mama Samiah yuko busy kubeba vibuyu na mikuki bila kusahau kutafuta ulinzi wa kiganga, ili hali watu aliowapa dhamana ya kulinda raia na mali zao ndio wa kwanza kuwashambulia na kuwaua raia

Sisi kama taifa tumepoteza dira chini ya uongozi wa huyu mama
Mauaji ya polisi hayajaanza leo toka enzi za Kina Zombe Mama ndio alikua Rais kipindi hicho ?...enzi za Magu wapo polisi waliweka pembe za ng'ombe kwa mstaafu na kuchukua rushwa ya 100m matukio yao ni mengi kwa awamu tofauti inatakiwa uwe na kumbukumbu tuu...
 
kuna police alikuwa anaitwa Benadi kama sikosei.kikosi chao kilikuwa na askari kazaa pale Morogoro ila nisingependa kuwataja.
hawa police walikuwa wakifanya unyang'anyi wa kiujambazi kwa wa2 wengi sana.Ila uyu benad ambae aliingia kazini kwa kipaji cha kucheza mpila alipatwa na shida ya kuifiwa na mke wake.Ila cjajuwa kilichomuuwa mkewe.
kutokana na kifo cha mkewake ambae alikuwa anafanya kazi SUA uyu askari akaamuwa kuokoka.
Sasa basi katika kuokoka kwake ilimbidi aanze kutubu matendo yote ambayo alikuwa wakiyafanya.
Apo ndio alikuwa anaamuwa kuyasema adhalani matendo ambayo alikuwa wakiyafanya na askali wenzake.siwezi kuelezea sana mambo ambayo walikuwa wakiyafanya ila hayatofautiani na aya waliyofanya askali wa mtwala akina Zombe.
Mwisho waliamua kutangaza kama yule askali amechanganyikiwa na wakampeleka dodoma milembe ila bado mshikaji alikoamaa na msimamo wake na kuamuwa kuandika vijalada kuutangazia uma kwa matendo yao waliyokuwa wakiwafanyia rahia hasa wafanya biashala wenye hela.
Mwisho kabisa uyu askali walimkuta amejinyonga ila kwanye mazingila yanaonyesha kuwa aliuwawa ila kwakuwaa upelelezi wanafanya wao hivyo walifanikiwa kumpoteza.
Kati ya maaskari waliobaki ni yule ambae niliona you tube amejitengenea kabuli.Nazani damu za wasio na hatia zishaanza kumtafuna...
Nazani damu za watu wasio na hatia.. 76 nazani anaitwa.
naomba nisiongee sana maana zama za jiwe bado zinaendelea...Matendo yanayo tendeka sasa c mageni kwenye idala hii[emoji24][emoji22]!!!
m
Huyo benadi....kina zombe..hayo mambo walikua wanafanya zama za magu???.

Mbona umemaliza andiko lako kikolo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Said Mwema ndo alikua IGP makini.
Siro na Mahita ndo ma IGP wa hovyo sana.
 
Hawa ndio magaidi sasa. Unamuua raia badala ya kumlinda?.
 
1643171342274.jpg

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2018 huyo kijana aliuwawa ndani ya mahabusu ya kituo cha polisi mtera mpwapwa dodoma huko na askari aliemuua alikuwa anaitwa mwita,adhabu aliyopewa huyo askari ni kuhamishwa pale kituoni na ni mtumishi wa jeshi la polisi mpaka leo JESHI LA POLISI CHINI YA IGP SIRRO LIMEOGA DAMU ZA WATANZANIA
 
Back
Top Bottom