Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Kwa Kuna tukio gani sijaelewa
20220126_085439.jpg
 
Shujaa kwako na umeficha matako yako hapo kwenu!!!!nenda kaunge juhudi kwa kujilipua wapasue bichwa lako.
watanzania tunakaupumbavu flani cha kushabikia ujinga. mtu akiwa na akili timamu hawezi shabikia ujinga ka huo
 
CCM imeingiaje hapa?? Roho mbaya ni Tabia ya Mtu
hawa ndo wale mvua ikinyesha wanasema tunamshukuru raisi kwa mvua kunyesha, Chuki ifike mahali tuzipunguze mtu anaingiza lisilo husika kisa tu kichwani mwake anachuki dhidi ya chama flani
 
Policcm hao. Ukimzoesha mbwa kukufuata Kuna siku utaingia nae msikitini......mliwazoesha kuuwa na kutesa Wapinzani na kuwapora Mali zao, mkashangilia. Endeleeni kushangilia sasa, na wataendelea sana kufanya unyama
Na ipo siku watawageukia hao hao waliowazoesha na kuwafutilia mbali time will tell
 
we ni mtu wa hovyo so utaandika hovyohovyo tu na akili yako ni mgando so huwezi fikiria kwa marefu

sikuhizi sijui watu wako na shida ganii. yani kama wamedata vile, mtu anashabikia ujinga tena wakuondoa uhai wa mtu kisa hajaguswa yeye
Stress na njaa zimepanda kichwani.
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

View attachment 2095921

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo
Hao ndio sampuli ya kina Kingai, Jumanne, Mahita, Makonda, Sabaya, nk nk. Kwao utu wa mtu si kitu. Kitu ni maslahi binafsi yasiyodumu hata muongo mmoja. Na hiyo ndio sura ya jeshi la Polisi ndugu zangu. Ukisikia raia wanayokumbana nayo, machozi yatakutoka. Na bado utaambiwa uchunguzi haujakamilika mpaka baada ya miaka 5! Mpaka Mahakama....Kuna tatizo kubwa la mifumo. Sio ya kikoloni wala sio yetu wenyewe, yaani uchotara.
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

View attachment 2095921

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo
Wangekuwa raia wasingekuwa hai saivi. Police wakifanya kosa ni mahakamani ila raia ni risasi.
 
Huyo cpl kaingizwa matatani itakuwa alikuwa ni shoferi wao kwenye kupiga dili wanyongwe hadharani mama....ee
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

View attachment 2095921
Hizi huwa ni tasrifa za kuounguza hasira za wananchi.
Hivi wale mapolisi walio mtapeli prof. Maeda pale USA RIVER tukaambiwa wamesimamishwa kazi si juzi tulimuona Jumanne ambae ni Oc Cid akitoa ushahidi wa mchongo kwenye kesi ya Mh. Mbowe na kujitambulisha kama mkuu wa upelelezi Arumeru?
Hawa polisi wamekuwa wa ajabu sana.
 
Umesema:
.......Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.....

Ukaendelea:
..JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.....

ULITAKA ACHUKUE HATUA GANI, TUMEHURU?
 
Hii imenifanya nifikiri zaidi na nikajikuta napata maswali:-
1. Huko mahabusu alikua pekeyake..??
2. Wakati anataka kujinyonga kwanini mahabusu wengine hawakutoa taarifa..??

What if wamemnyonga ili kupoteza ushahidi??
...na amejinyonga na nini wakati wakati kila kitu wanaacha kaunta, ikiwemo mikanda, kabla hawaingja Mahabusu?
 
Halafu karibu wote Ni maafisa wakubwa tu. Mrakimu wa polisi sio mtu mdogo, Sasa Kama wenye nyota tatu wanapora vijihela vidogo Kama hivi, tutegemee Nini kutoka kwa koplo ambaye kamba yyake Ni fupi?
Hatari sana mzee

Haya mambo yapo sana

Ya dhuluma,uporaji

Ova
 
Back
Top Bottom