Mtwara: Mwalimu atiwa mbaroni kwa kujihusha na mapenzi ya jinsia moja

Mtwara: Mwalimu atiwa mbaroni kwa kujihusha na mapenzi ya jinsia moja

Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Nanyani iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara, Mohamed Ally Kajao (34) na Dickson Paul Tamba (27), mjasiriamali, mkazi wa Mkuti Chini Machinjioni wilayani Masasi, kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Februari 12, 2025 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Issa Suleiman, amesema tukio hilo lilifanyika Januari 2025 katika nyumba ya kulala wageni (jina limehifadhiwa) ambapo Dickson Tamba aliruhusu kuingiliwa na Mohamed Ally Kajao, kisha kunakili picha mjongeo (video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Pia Jeshi hilo linamshikilia mlinzi wa Kampuni ya Kiwango Security, mkazi wa Magomeni wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kike (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne mkazi wa Magomeni. Pia linamshikilia na Mkulima Ahmad Mohamed (39) mkazi wa Libobe wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike (04) mkazi wa Libobe.

Ameongeza kuwa kwa kipindi cha kuanzia Januari 1, 2025 hadi Januari 31,2025 kupitia doria, misako na operesheni iliyofanyika kwa kipindi hicho Jeshi la Polisi mkoani humo lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 23 kwa tuhuma za kujihusisha na kubaka, kupatikana na pombe haramu ya moshi (gongo), wizi, kuchoma nyumba moto, kupatikana na nyara za serikali pamoja na kupatikana na dawa zidhaniwazo kuwa ni za kulevya aina ya bangi.

SOURCE JAMBOTV INSTAGRAM PAGE
Gazeti limeona litumie neno Mwalimu Ili kupata attention wakati hapo yupo na mtu mwingine 😁😁
 
Young girls of 4 and 10 years old wamelawitiwa but nobody cares kuliko old dudes with 34 and 27 years banging each other. Mmerogwa haaa.
Hey LIKUD you think your kids are safe cause wapo government schools heheeee tukisema mnatutukana kweli kweli as if mnajua uhalisia. haya kiko wapi
Bolotoba
 
Mgalatia kaliwa na kobazi

Amri ya papa inafanyiwa utekelezaji sijui, dini ni usanii

Mgalatia kaliwa na kobazi

Amri ya papa inafanyiwa utekelezaji sijui, dini ni usanii
Sasa tukikazana kupoint fingers kwenye dini fulani inasaidia nini? Mpaka leo hatuoni kuwa hili ni janga la jamii yote?? Utasemaje hili ni la dini fulani? Badala tufocus kwenye kuondoa tatizo, tuko busy na kukejeli dini!! Mitaani ushoga unazidi kuenea na hakuna dini iliyoachwa nyuma kwenye hili. Tuwalinde sana vijana wetu jamani.
 
Wale tunaowaamini watulelee na wakuwafundisha wanetu ndo balaa.....

Mungu atulindie vizazi

Wazazi tuwe makini

Mwalimu km huyo unafikiri watoto wadogo wa kiume kwa ke watapona kweli
 
Back
Top Bottom