Muda hautoshi na Maxence Melo

Muda hautoshi na Maxence Melo

Mzee analipendezesha sana jukwaa la historia. Huyu ni hazina kwa taifa letu maana anaifahamu vizuri na kwa undani historia ya nchi yetu tokea kipindi kabla ya harakati za uhuru, wakati wa harakati zenyewe na baada ya hapo.

Unfortunately kuna watoto humu huwa wanamjibu hovyo hovyo na kumkejeli sana. Uzuri ni kuwa mzee ana busara wala huwa ha panic na huwajibu vizuri tu kwa hoja na kistaarabu.

Pongezi nyingi sana mzee wangu Mohamed Said. Wewe ni hazina kubwa kwa taifa letu.
Ni kweli mkuu
 
MUDA HAUTOSHI NA MAXENCE MELO WA JF

Leo nyumbani kwangu nimempokea kijana ambae siwezi kuwa na maneno ya kutosha kumweleza.

Ameifanyia Tanzania makubwa.

JF imenifanya mimi nifahamike kwa kusomwa ulimwengu mzima walipo wazungumzaji wa Kiswahili.

Katika kunisoma huku ndiko wengi wakaijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyka ambayo si wengi walikuwa wanaijua.

Sina cha kuwalipa.

MM amefika kwangu kunikabidhi cheti changu na zawadi nzuri sana ya simu.

View attachment 1977049
Mohamed Said shikamoo baba
 
Upunguze udini.
Sang'...
Ningekuwa mimi nazungumza ''dini'' watu wasingefika hapa JF kunisoma.
Nilichofanya mimi ni kurejesha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika baada ya kufutwa.

Ikasadifu kuwa wengi katika wale waliopigaia uhuru wa Tanganyika ni Waislam.
Hiki ndicho kinachokuchoma wewe.

Na katika hili hauko pweke wako wengi mfano wa wewe wanataka historia hii isiwepo.

Udini maana yake ni kuwakandamiza wale ambao si wa imani yako.
 
MUDA HAUTOSHI NA MAXENCE MELO WA JF

Leo nyumbani kwangu nimempokea kijana ambae siwezi kuwa na maneno ya kutosha kumweleza.

Ameifanyia Tanzania makubwa.

JF imenifanya mimi nifahamike kwa kusomwa ulimwengu mzima walipo wazungumzaji wa Kiswahili.

Katika kunisoma huku ndiko wengi wakaijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyka ambayo si wengi walikuwa wanaijua.

Sina cha kuwalipa.

MM amefika kwangu kunikabidhi cheti changu na zawadi nzuri sana ya simu.

View attachment 1977049
Mungu ibariki Jf
 
Hongera sana Mzee wetu Mohamed Said kwa tuzo hiyo bora ambayo imetokana na maarifa kedekede umeyoyamwaga kwenye hadhira ya JF bila kutuchaji gharama yoyote na kwa hakika jina lako litakumbukwa hapa Nchini kwa uandishi wenye tija kihistoria.
 
Hongera sana mzee wetu, baba yetu, na hazina yetu hapa jf na tz kwa ujumla, ata unavyowajibu vijana wasio na adabu unadhihirisha hekima kuwa sana ambayo inatakiwa kuwa soma kwetu sote, Mungu azidi kukulinda na kukupa maisha marefu zaidi mzee wetu, tunabarikiwq nawe hapa jf.
 
Hongera Mohamed ,na Mimi nilikijua kitabu chako na kununua kupitia JF .

Hivi jina lako la Sydney lilitokana na nini?

Baada ya uhuru wa Tanganyika Dosa Aziz na Abdulwahid Sykes walifanya kazi gani na kwanini hawakuwa sehemu ya serikali Kama mawaziri nk.

John Rupia alikufa mwaka gani?
 
Sijui na mimi zawadi ya ndizi ataniletea lini Melo.
Ngoja niendelee kusubiri
 
Amefanya jambo la maana mno, japo nina uhakika kuna wahafidhina wameghafirishwa sana na hiki kitendo.
Mtu kama Mzee Mohamed Said ilibidi atambulike kuanzia ngazi ya kitaifa na apewe heshima zake stahiki.
Mzee muungwana sana na msema kweli.
Japo inaonekana kuwa anaegemea dini flani lakini nani asiyekuwa na upande?
 
Hongera sana mzee wetu, baba yetu, na hazina yetu hapa jf na tz kwa ujumla, ata unavyowajibu vijana wasio na adabu unadhihirisha hekima kuwa sana ambayo inatakiwa kuwa soma kwetu sote, Mungu azidi kukulinda na kukupa maisha marefu zaidi mzee wetu, tunabarikiwq nawe hapa jf.
VL,
Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom