Yaliyomo:
UTOTO NA UWAJIBIKAJI WA MZAZI KATIKA MALEZI YA MTOTO
MTOTO NA ELIMU
MTOTO NA JAMII
TABIA NA MATENDO
MTOTO NA MTAZAMO WA MAISHA
ATHARI ZA MALEZI DUNI

Utoto hauepukiki lakini je watoto wengi wanafurahia utoto wao?
Hali ya kuwa mtoto ni hatua mmoja wapo ya maisha ya mwanadamu. Mwanzoni mwa maisha ya utoto ndipo ambapo akili ya mtoto hunasa na kujifunza vitu vingi kwenye jamii. Jukumu la malezi ya watoto huwa ni la baba,mama na jamii kwa ujumla.
Watoto wana haki ya kupata uangalizi na usimamizi bora kwa ajili ya maisha yao ya badae ,na hili linahusisha kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mtoto anapokua shuleni ,nyumbani na jamii.
Utoto unapaswa kufurahiwa na kuthaminiwa na mtoto mwenyewe na jamii kwa ujumla ili kutengeneza kizazi bora chenye tija katika jamii yao ijayo.
Je wazazi wengi huwajibika katika malezi ya mtoto?
Jukumu la malezi ya watoto mara zote kwenye jamii zetu limeonekana kuwa la mama kwa asilimia kubwa lakini utandawazi, kukua kwa sayansi na teknolojia kumebadilisha hili ambapo wanawake wengi wameingia kwenye shughuli za kujikwamua kiuchumi ambapo wanatumia muda wao mwingi na muda mchache nyumbani kwa ajili ya watoto.
Ni kweli wanawake wengi kwa dunia ya sasa ni waajiriwa ama wameamua kujiajiri,na hili limepelekea jukumu la malezi ya watoto kubebwa na wasaidizi wa kazi nyumbani.
Malezi ya watoto wanayopokea kutoka kwa wasaidizi wa kazi za nyumbani yana athari kubwa kwenye ukuaji na maisha ya mtoto.
Tunapaswa kubadilika hapa tukiwa kama walezi ama wazazi kwa kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya watoto katika vitu mbalimbali ikiwemo shule, lishe na maisha yake nyumbani na kwenye jamii na changamoto wanazo kumbana nazo. Hii itaboresha maendeleo yao na kujenga hali ya kuthaminika na kujiamini kwa mtoto.
Watoto wana haki ya kusikilizwa, lakini je ni lini ulimpa sikio mtoto juu ya yale yanayomsibu au mawazo yake na mtazamo juu ya maisha yake?
Wazazi wengi wameonekana kukosa muda kabisa wakuwa karibu na watoto wao kitu ambacho kinawanyima watoto uhuru wa kusema changamoto wanazo kumbana nazo katika maisha yao ya kila siku. Hali hii imeongeza matukio mengi ya unyanyasji kwa watoto.
Baba ana mchango mkubwa kwenye malezi ya mtoto lakini mara zote siye anayeshinda nyumbani muda mwingi hivyo kwa wakati tulio nao muda na uangalizi wa watoto limekua jukumu la wasidizi wa kazi.
Hivyo malezi anayopokea mtoto yana athari kubwa sana katika maisha yake ya baadae kuanzia elimu yake, uelewa, muingiliano wake kwa jamii,afya yake ya akili,mtazamo wake na maono yake juu ya maisha, tabia na matendo yake, afya yake kiujumla na ukuaji.
MTOTO NA ELIMU
Maendeleo ya mtoto kwenye elimu yanategemea na ufuatiliaji wa mzazi katika hili
Je mara ya mwisho mzazi kufuatilia maendeleo ya mtoto wako shuleni ilikua lini?
Kutokutenga mda kwa wa wazazi wengi kwa ajili ya watoto kunawafanya kuto kufuatilia kwa wakati maendeleo ya watoto wao shuleni na wengi wao ma wengine wameliacha jukumu hili kwa walimu, wasaidizi wa kazi na mtoto mwenyewe.
Watoto wengi wanaofanya vizuri kwenye elimu ni wale ambao wazazi wamewekeza muda katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni. Kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni yanawezesha kubaini changamoto wanazo kumbana nazo watoto shuleni na kushirikiana kuzitatua kwa wakati.
Baadhi ya watoto wamekua wakipitia unyanyasaji kutoka kwa walimu, majirani, wasaidizi wa kazi za nyumbani ama watoto wenzao kitu ambacho huchangia maendeleo mabovu ya mtoto mashuleni iwapo atakosa sehemu sahihi ya kuwasilisha tatizo lake au mtu wa kutambua mabadiliko yake kwa wakati sahihi.
Kuna mwanga kwenye ufuatiliaji.
MTOTO NA JAMII
Malezi yetu ya leo yana athari katika muingiliano wa watoto wetu kwenye jamii, mtoto anayepata muda wa kutosha na wazazi wake ni tofauti na mtoto ambaye maisha yake muda mwingi anautumia na msaidizi wa kazi za nyumbani katika kuiendea jamii.
Visa vya vya magonjwa ya akili kama msongo wa mawazo na uoga vimeongezeka zaidi nyakati hizi ukilinganisha na zamani. Sababu kubwa ni kukosa uangalizi wa karibu na msaada wa kutosha katika kutatua changamoto anazokutana nazo iwe binafsi au katika jamii.
Watoto wanaokosa muda na wazazi wao wengi hukosa hali ya kujiamini na uthubutu katika kutenda baadhi ya vitu kwenye maisha yao sababu yakukosa motisha na muongozo sahihi, na hali hii huendelea hadi pindi mtoto anapokua na huleta uoga na msongo wa mawazo ,watoto wa mitaani kuongezeka na kukithiri kwa tabia mbaya na vitendo viovu kwenye jamii dhidi ya watoto.
TABIA NA MATENDO
Tabia na matendo ya kila siku ya mtoto huathiriwa na Malezi yao.
Watoto wanaokosa malezi na muda wa kutosha na wazazi wao huwa na hali ya maamuzi yao binafsi na wengi wao huwa hawapendi kushirikisha mambo yao kwa watu wengine na hili huendelea hata pale atakapokua mkubwa.
Hali hii huathiri zaidi matendo yake wakati wa kutataua changamoto au matatizo atakayokua anakumbuana nayo kwenye maisha.Wengi wao huchukua maamuzi ambayo wao wanaona ni sahihi bila kuomba ushauri kwa wengine.
Kumekuwa na ngezeko la matukio ya vijana kujinyonga ama kuua na hii ni sababu ya kukosa malezi na muda wa kutosha kutoka kwa wazazi wake na kupekea kuwa wabinafsi wa kufanya maamuzi na kutumia njia ambazo si sahihi kutatua matatizo.
MTOTO NA MTAZAMO WA MAISHA
Malezi yanaathiri maono ya watoto juu ya maisha. Waswahili wanamisemo
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!!!!! ,Samaki mkunje angali mbichi.
Mtazamo wa mtoto juu ya maisha huanza kutengenezwa tokea mwanzo ,utotoni na huenda hivyo hadi pindi anapokua kijana hadi utuuzima na maisha yake yote.
Kukosa muda wa kutosha na wazazi ama kulelewa na msaidizi wa kazi za nyumbani ama kujilea kwa watoto wengi hujenga namna anavyo utazama ulimwengu.
Wengi wao hutazama vibaya ulimwengu kama mahali ambapo kumeshindwa kumpatia furaha na ni sehemu ya watu wasiojali hali zao na pia maisha ya wengine.
Hili kwa upande wa pili limepelekea watoto nao wakikua kutowajali wazazi wao na familia zao wakati ambao wanahitajika kutoa msaada wa ukaribu sana.
ATHARI ZA MALEZI DUNI
unyanyasaji kwa watoto
Unyanyasaji kwa mtoto unaweza kufanywa na jamii inayo mzunguka ,walezi wao pia watoto wenyewe katika familia .Malezi duni na kukosekana kwa ukaribu wenye tija baina ya mzazi na mtoto kunapelekea kukithiri kwa tabia za unyanyasaji kutokana na kutokuwepo mtu sahihi wa kumsimamia , kueleza shida zake na kumtatulia changamoto zake kwa namna moja au nyingine katika maisha yao.
Kuongezeka kwa watoto wa mitaani.
Mgawanyiko na kukosekana ushirikiano katika familia.
Msongo wa mawazo.
Visa vya ubakaji na ulawiti kwa watoto vimekua vikiongezeka siku hadi siku kutokana na ukosefu wa ulinzi kwa watoto ,ukaribu na muda kati ya wazazi,walezi na watoto wao.
Muda ni kitu muhimu zaidi kwenye malezi ya watoto wetu, ni jukumu la kila mzazi ama mlezi kuwapa muda mwingi watoto wao katika malezi bila kusahau furaha na nyakati za kukumbukwa katika maisha ya kila siku ya mtoto na kuwafundisha watoto juu ya umuhimu wa familia.

Upvote
2