Muda ni Mwalimu mzuri sana: Siasa ni kama upepo, hubadilika wakati wowote

Nilifikiri ungekuja ku challenge hili andiko umalizie na nonsense...hali imekuwa tete hahahaa
hili sio andiko gentleman,
ni nukuu za wenye historia zao, waliotumia muda wao vizuri na kwa usahihi na kwakweli wakatimiza wajibu na malengo yako ipasavyo, katika maisha yao mafupi waliyojaaliwa kuishi duniani na Mwenyezi Mungu,

Otherwise ideas za mtoa hoja ni kwa uchache sana na amejaribu kutumia faida ya kusoma vitabu vingi vizuri sana, and that is very good thing,

umeelewa gentleman?🐒
 
Jambo ambalo wenzetu wa Magharibi walipewa NEEMA NA MUNGU kulichunguza, kulifahamuni, kulielewa na kuliheshimu sana ni suala zima linaloitwa MUDA.
MALCOM LUMUMBA ,hapo ungemtaja kiranja wao mkuu Marekani! Western Europe wamekutwa na mabadiliko huku wakiwa kwenye usingizi wa pono!!


Marekani chini ya Trump ndiyo imeyaadapt haya mabadiliko ya kisiasa makubwa yanayoendelea hapa duniani kwa sasa ,ambayo kwa jicho la tai yalianzishwa na China na Urusi kupitia kile kinachoitwa Multipolar World.


Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100% mabadiliko hayaepukiki na hayazuiliki, ila mabadiliko huwa yanakuwa adapted kwa yule ambae hakujiandaa nayo!


Hata Nyerere naye aliadapt mabadiliko coz kwenye kipindi chake hakujiandaa na zile changamoto za yale mabadiliko. Mwinyi, Mkapa plus Kikwete nao pia waliaadapt mabadiliko kwenye nyakati zao coz nao hawakujiandaa ila walivuka!

Viongozi wote waliopita ukimtoa Magufuli, walitumia msemo huu, mwenye nguvu mpishe!! Viongozi wote wa mataifa makubwa wamekuja na wataendelea kuja.Kinachowaleta ni maslahi na siyo kingine.!

Wote tunakubaliana kuwa huwezi kuwakatalia hawa mabwana jambo lolote linalohusu maslahi yao coz hatuna huo msuli! Kinacho fanyika ni wewe chukua sehemu yako!


Naamini kama taifa tutavuka salama kwenye haya mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea hapa duniani iwe kwa jasho na damu coz hayaepukiki na sisi siyo kisiwa.

Swali : MALCOM LUMUMBA , ungekuwa wewe ndiyo Rais wa nchi halafu ule mswada umepitishwa, ungechukuwa maamuzi gani???
 
Muswaada ukipita, kiuchumi nini sisi huku chini ndio tutaumia zaidi. Tabaka tawala litakua la mwisho kuguswa. Labda itasaidia raia kuungana maana watafikiwa wengi
Sure mkuu, chamtemakuni tutakiona. Ila ndio ivyo itaharakisha sana anguko lao, maumivu ya kiuchumu yatawaunganisha sana raia.

niliku-PM, inshu fulani ingine.
 
Asante sana kwa bandiko hili kwangu ni bandiko bora la wakati huu, mwenye kupenda kujifunza atajifunza, linamfundisha mtu binafsi, taasisi na serikali.
 
Lugha nyepesi ndiyo inayomfanya Heche aogopwe zaidi kufanya mikutano kuliko Lisu. Lisu, huzungumza na tabaka la wasomi, wanaofikiria kesho. Heche anaelezea leo ya watu wa chini inavyoharibiwa.
Nimechomekea tu hapo.
Heche is better ila bado hajafikia level ya hao wawili.
Lissu kinachomgharimu ni hicho, anapendwa na wengi lakini lugha yake ni ya kisomi. Ndio maana kesi yake ilipooneshwa live alipata fans zaidi kwa sababu alikuwa mwalimu zaidi kuliko muonesha articles za sheria.

Hata sera ya katiba mpya kwa CHADEMA walishindwa kuiuza vile Mange aliiuza kabla ya October 29. Natumai CHADEMA kitengo cha mawasiliano imejifunza kitu

Elites ni wengi lakini wasio elites ni wengi zaidi hivyo, wajifunze language of the poor kama CCM ili kwenda nao sawa
 
Usipoteze muda wako la hili ndondocha...
Ni kulitwanga dongo na kupotea....
 
Kuna muda nafurahi MAMA YENU kuwa madarakani maana kuna wale matomaso ndani na nje ya CCM walifikiri katiba mpya sio kipao mbele au kitu cha ulazima. Pia wengine walikuwa wanasikia kuwa kuna wana mtandao akina kikwete ni cancer ya taifa hili.

Uyu mama amekuja kuweka mambo uchi kabisa, uko mbele ambako bandiko linasema MUDA, tutakuwa tunaongea lugha moja na kutenda ili kuleta mabadiliko sio nje tu ya ccm bali hata ndani ya ccm. SAMIA ameletwa ili kuamsha matamaso juu ya mambo ya msingi yanayohitaji maamuzi magumu.
 
Asante sana kwa bandiko hili kwangu ni bandiko bora la wakati huu, mwenye kupenda kujifunza atajifunza, linamfundisha mtu binafsi, taasisi na serikali.
Nakubaliana na wewe 100% kuwa hili ni bandiko bora kabisa. Tlatlaa anadai eti bandiko kwa uchache limetokana na Mkuu Lumumba kusoma vitabu...nimefurahi ameshindwa kabisa ku challenge andiko kwa uchawa wake nonsense.. chawa hawawezi kabisa gusa hii critical thinking.
 
Muda wa CCM kuondoka madarakani umefika, hivyo ni lazima haya yatokee ili CCM ianguke na huu pia ndio msingi wa
viburi vya watawala.

Kumbuka , ili mtawala aanguke, wakati mwingine ni lazima awe na kiburi cha ajabu, hatua ambayo watawala wetu sasa wameifikia hivyo ni swala la muda tu.

CCM itaanguka kama utawala wa makaburu wa Afrika kusini ulivyoondoka madarakani.
 
Swali : MALCOM LUMUMBA , ungekuwa wewe ndiyo Rais wa nchi halafu ule mswada umepitishwa, ungechukuwa maamuzi gani???
Mkuu Enzo kwanza amini nakwambia, mimi ningekuwa Raisi wa Tanzania nchi isingefika hapa ilipo leo.
=======================================================================
Nafahamu jinsi hili dude linavyofanya kazi NJE-NDANI, na sidhani hao wanaojiita watoto wa mjini kama kuna hata mmoja angenishinda mimi. Hata siku moja. Awe ni Rostam, Jakaya, Makamba, Kinana, Rugemalila, Mufti Mkuu au Kadinali, wasingenithubutu hata kuinua kidole. Never On Earth!!! Kiukweli mnapowalalamikia wahuni wa nchi hii na WANAMTANDAO huwa nawashangaa mno. Binafsi nisingewasazia hata mjusi anayekaa kwenye dari za nyumba zao.

Sema tu, UPELE HUWA HAUMKUTI MWENYE KUCHA........

====================================================================================

HAYA KUJIBU SWALI LAKO: Kwenye masomo ya usalama hasa STATE-CRAFT & STRATEGY nchi huwa inafananishwa na meli ya mizigo iliyopo baharini (This is allegorical). Ambapo tunafahamishwa kabisa kwamba Meli ya Nahonda(A Ship Belongs to the Captain), lakini bahari ni ya MUNGU (But the Sea belongs to GOD). Hapa akimaanisha kwamba wewe unaweza ukawa nahonda bora kabisa, mwenye manowari mpya, lakini uwezo wako huishia ndani ya meli yako tu. Kufika kwako salama kunategemea mwenye bahari kaamuaje wewe ufike. Akichafua tu bahari inakula kwako na ujuzi wako.

Sasa kwenye usafiri wa baharini kuna kitu tunakiita JETTISON IN MARINE INSURANCE, ambao huelezea nini nahodha anatakiwa kufanya kuzuia meli yote isizame na kuokoa maisha ya watu na baadhi ya mali za thamani zilizopo ndani ya meli.

Bahari inapochafuka jambo la kwanza Nahodha anatakiwa kufanya ni kuhakikisha anapunguza mizigo mizito isiyo ya thamani ambayo inaelemea meli. Hii mizigo kitaalamu tunaiita SCRAPPERS au SACRIFICED GOODS, ambayo hutupwa ili kulinda mizigo yenye thamani zaidi ndani ya meli. Hichi kitendo kitaalamu tunakiita JETTISON.

Wanausalama wa nchi za Magharibi (Judeo-Christian States) au watu waliobahatika kupata mafunzo ya usalama nchi za Magharibi lazima wanafahamu huu mfano naoenda kuuzungumzia. Mfano wa Jettison mara ya kwanza kabisa, unaonekana kwenye kitabu cha NABII YONA ambapo, yeye alitumwa na MUNGU aende Ashuru (Ninawi) lakini yeye akaenda Uhispania (Tashishi) kwa ukaidi ili ajifiche na uso wa MUNGU. Kumbuka, meli ilikuwa ni ya Nahodha wa Yona, lakini bahari ilikuwa ni ya MUNGU.

Baada ya ukaidi wa NABII YONA, MUNGU alichafua bahari na meli ikaanza kuzama. Jambo la kwanza kabisa nahonda alianza kufanya ni kutupa shehena ya mizigo baharini (Jettisoning), lakini wapi, bahari ikazidi kuchafuka tu. Mwishowe wakafahamu kwamba mle ndani lazima kutakuwa na mzigo ambao wakiutupa basi meli yote inaweza kupona. Uzuri YONA akasema ukweli, kwamba ametenda dhambi na mwenye bahari anamuwinda, hivyo akitoswa yeye majini lazima bahari itatulia.

Nahonda alitaka kumlinda YONA na ukaidi wake, lakini bahari ikazidi kuchafuka. Hivyo akawa na ETHICAL DILEMNA: Either let the whole ship sink by saving one rebellious prophet or sacrifice one rebellious prophet to save the lives of every person on the ship. Baadaye nahonda alikubaliana na ukweli akamkamata YONA na kumtosa baharini. Ghafla, baada ya YONA kutoswa baharini, dhoruba ikatulia na meli yote ikapona.
================================================================================

Sasa kwenye MARINE INSURANCE kuna kanuni iitwayo, SUE AND LABOUR ambayo inamwondolea Nahodha uwajibikaji wowote ule wa kisheria na kimaadili, endapo ataamua kutosa baharini bidhaa zisizo na thamani, zenye hatihati ya kuzamisha meli yote (SCRAPPERS & SACRIFICED) kwa kuongeza uzito wakati wa dhoruba kali. Mwisho wa siku mashirika ya bima yatachangia nusu kufidia gharama ya mizigo iliyotupwa baharini endapo itathibitika kwamba bidhaa zilizotupwa baharini (Jettisoned Goods) zina sifa zifuatazo:

1. Dangerous Goods (Bidhaa Hatari)
2. Heavy Goods (Bidhaa nzito sana)
3. Non-Essential Goods (Bidhaa zisizo na thamani kwa matumizi)
4. Perishable Goods (Bidhaa ambazo zinaharibika kwa haraka)

====================================================================================
TAFAKARI, CHUKUA HATUA...
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…