Muda ni Mwalimu mzuri sana: Siasa ni kama upepo, hubadilika wakati wowote

Muda ni Mwalimu mzuri sana: Siasa ni kama upepo, hubadilika wakati wowote

Bahari inapochafuka jambo la kwanza Nahodha anatakiwa kufanya ni kuhakikisha anapunguza mizigo mizito isiyo ya thamani ambayo inaelemea meli.
MALCOM LUMUMBA ,ukitumia jicho la tai mbona nahodha alichukua hatua na anaendelea kuchukua??

Kinachoisumbua nchi yetu kwa sasa ni matumizi kidogo ya akili coz inaonekana nchi inaongozwa kwa maamuzi ya kihisia zaidi!


“Your mind is the starting point of all war and all strategy. A mind that is easily overwhelmed by emotion, that is rooted in the past instead of the present, that cannot see the world with clarity and urgency, will create strategies that will always miss the mark.” ―

Robert Greene, The 33 Strategies of War
 
MALCOM LUMUMBA ,ukitumia jicho la tai mbona nahodha alichukua hatua na anaendelea kuchukua??

Kinachoisumbua nchi yetu kwa sasa ni matumizi kidogo ya akili coz inaonekana nchi inaongozwa kwa maamuzi ya kihisia zaidi!


“Your mind is the starting point of all war and all strategy. A mind that is easily overwhelmed by emotion, that is rooted in the past instead of the present, that cannot see the world with clarity and urgency, will create strategies that will always miss the mark.” ―

Robert Greene, The 33 Strategies of War
Huyu aliyeropoka kwamba "Polisi walirushiwa mawe" hakutakiwa awepo pale.

Kwenye kikao Bibie kaletewa kabrasha anaambiwa kwamba jamaa hafai.

Bibie kaanza BIG-BABBY TANTRUMS za kulia na kujifungia chumbani hataki kuongea na mtu.

Kisa, wanamdharau, kaomba aletewe ghahawa anywe peke yake ndani.

Kuona hali ni mbaya, ikabidi waliite lile lizee la Cold-War kazi maalumu ambalo halitaki kustaafu.

Lile lizee kufika na kuzungumza naye ndiyo kulazimisha hiki kituko kuwekwa pale ambapo unakiona leo.
========================================================================================

Huyu ni MWENZAO, MAKE NO MISTAKE...
​
 
daima maisha hayana extra time,
fanya upasalo kutenda maishani kikamilifu, kwa usahihi, kwa wakati na kwa muda muafaka, vinginevyo hutakua na historia 🐒
Angalau hujaziita porojo nonsense gentleman
 
MALCOM LUMUMBA ,ukitumia jicho la tai mbona nahodha alichukua hatua na anaendelea kuchukua??
Makosa yalianza kwa kutosikiliza Wananchi kwa mazoea tu kwamba ndivyo walivyo.
Matatizo yalipotokea jambo la kwanza ilikuwa kuwajibika! Hakuna aliyewajibishwa ikieleza hakuna majuto
Hatua zinazochukuliwa hazina ''vote of confidence'' kutoka katika Umma! House of cards

MALCOM LUMUMBA kasema '' muda''
 
Mwaka 2024 ungefanya majadiliano na makada wa CCM na Maafisa Usalama wa Tanzania kwamba kuna siku watanganyika wanaweza kufanya vurugu za kutisha, na serikali kufanya mauaji makubwa ya kutisha kwa raia wake, wanufaika wakubwa wa mfumo kama Kikwete, Rostam, Harbinder, pamoja na walinda malango wa mfumo kama Mkuchika, Luhavi, Mombo, Sirro, Mafwele, Nkunda, Makonda na wengine wangekucheka na hata kukuita mwendawazimu. Hayo mambo yaliaminika ni ya Rwanda, Kongo, Somalia, Kenya, Burundi na Sudan, sisi watanzania amani ni haki yetu ya kuzaliwa hivyo hayawezi kabisa kutokea.

Mwaka 2020 ungeonana na kina Humprey Polepole, Bashiru Kakurwa, John Kijazi, Diwani Msuya na wafuasi wao wengine, na kuwaambia kwamba huu uchaguzi ambao mnatumia nguvu sana kuuvuruga na hii mifumo mnayoitengeneza itakuja kuwaumiza na Raisi Magufuli hawezi kuvuka 2021 ungeonekana Mwendawazimu. Nakumbuka mwaka 2019 kuna Mzee aliwahi kuniambia kwamba Uchaguzi wa 2020 hautakuwa na vurugu kwasababu pande zote hasimu zina cha kupoteza, na wanafahamu fika kwamba wakilianzisha basi wanaweza wakamshindwa JPM kwasababu alikuwa ni mtu asiyeogopa kumwaga damu. Raisi kufia madaraka ni jambo ambalo Tanzania lilikuwa haliwaingii kabisa kichwani watawala, zaidi-zaidi raisi kufariki kwa kifo chenye utata. Ugonjwa mkali kuwaruka watu wa MBAGALA na kumfikia yeye aliyekuwa kwenye SAFE-ZONE QUARANTINE.

Aliniambia vita ya JPM itakuwa baada ya uchaguzi, wakati ametulia, amejisahahu na kudhani kwamba ameshashinda kabisa vita hapo ndipo atashambuliwa vibaya. Huu ni wakati mzuri kwasababu joto la uchaguzi huwa linakuwa limeshuka na kile kohoro na kimuhemuhe cha ushindi kinakuwa kimewakaa watawala kichwani. Kama ambavyo alisema Shakespeare "Beware of the Odes of March" JPM alichomoka, na hakuna aliyeamini mpaka leo. Mimi niliposikia nikaona labda huyu Mzee anasema tu, lakini yalipotokea alikaa kimya na katika kumuuliza kwangu hajajibu mpaka leo kama hakuwahi kuongea na mimi. Nilifahamu kwamba kuna watu WAKO MBELE YA MUDA.

=============================================================================
Kuna msemo uko kwenye kitabu cha "The Art of War" ambapo Sun Tzu aliandika hivi "After Crossing the river, you should get far away from it". Jambo ambalo MAMA YENU na wenzake halijawaingia vizuri kichwani. Wameshavuka mto, lakini bado wamejenga mahema kwenye ukingo wa mto.

Mwaka 2021, mwezi MAY, ungemfuata Membe, Makamba, January, Nape, Rostam, Ridhiwani, Kikwete na kuwaambia kwamba kufika MAY 2026, watu wataikumbuka Tanzania na JPM na kutamani hata ule ukatili wake urudi kuliko hii serikali yenye matumanini ambayo imegeuka kuwa serikali inayochukiwa na kudharaurika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, sidhani kama kuna mtu angeamini. Ungemwambia Membe na January, binadamu ambao walikuwa na tamaa kali ya Uraisi wa JMT, kwamba miaka michache ninyi mtageuka kuwa wahanga wa hii serikali ambayo mnaamini uwepo wake ni tiketi zenu kisiasa, basi wangekuona una wazimu na kichaa. Membe na Makamba, walivuka mto, lakini bado wakajenga mahema kwenye ukingo wa mto (YAKAWAKATUKA WOTE)

Wachache ndani na nje ya mfumo mbali na kumchukia JPM, walipovuka mto waliondoka kabisa lile eneo na kufahamu hatari yake. Marehemu Lukuvi mbali na madhaifu yake, alikuwa moja kati ya watu waliousoma mchezo wiki chache tu baada ya JPM kufa, kwamba nchi inaenda kupoteza mwelekeo. Mbali na ujehuri (Kidada cha kihehe), tamaa za kupenda fedha na roho ya choyo, Lukuvi was an extemely competent and effective bureaucrat. He understood how systems work. Alifahamu fika kwamba MAMA YENU is a bad Gambit. Alivuka mto, akaenda mbali ya ukingo, lakini tamaa zikamrudisha pale-pale. Angekuwa na hekima angestaafu, maana alikuwa na ukwasi, heshima na mali. (YAKAMKUTA)

Mwingine ni Tundu Lissu, alimsoma MAMA YENU mapema kabisa na kumpa jina Malkia Mdanganyifu Mwenye Maneno Mazuri. Aliingia kwenye mtafaruku mkali, lakini huyu ni moja kati ya binadamu wachache mno hapa nchini Tanganyika mwenye uwezo wa kuyatazama mambo kama yalivyo, hata kama ni machungu. Hii sifa watanganyika asilimia 99% hawana. Bwana amevuka mto, na akaondoka kwenye ukingo. Mpaka sasa kuna jitihada za kumrudisha ukingoni lakini hazijafanikiwa.
=============================================================================

Mwezi April 2022, akipokelewa Marekani na wabunge na msululu mkubwa wa vigogo wa dunia, MAMA YENU ungemwambia kwamba kuna siku hawa hawatataka kuzungumza nawewe asingekuamini. Marekani alipokelewa na Makamu wa Raisi Kamala Harris kwa bashasha na upendo. Kwenye mkutano wa WTO na IMF alipokelewa na Kristalina Gorgieva kwa kumbato kubwa la upendo. Akapokelewa na Ngozi Okonjo-Iweala kwa furaha kubwa mno. MAMA YENU, wafuasi wake na dunia ikaamini kwamba yeye ni viwango vya kina Kamala Harrs, Kristalina Gorgieva, Ngozi Okonjo-Iweala na Mia Motley. Lakini mwaka 2026 inakuwa ngumu kuamini kwamba MAMA YENU yuko kiwango kimoja na wahuni wa ukanda huu kama Rutto, Musseveni, Kagame, Munangagwa na Tinubu.

===================================================================================
Jambo ambalo wenzetu wa Magharibi walipewa NEEMA NA MUNGU kulichunguza, kulifahamuni, kulielewa na kuliheshimu sana ni suala zima linaloitwa MUDA. Hii ni rasilimali ya bure ambayo hairudi mara mbili. Hii rasilimali huleta kitu kinachoitwa MABADILIKO (Changes). Kitaalamu hakuna mwanadamu ambaye anaweza kupinga mabadiliko. Awe MWEMA au Awe MBAYA, lazima atakutwa na MABADILIKO.

Wenzetu wazungu walichotushinda ni hapa tu: NIDHAMU KWENYE MUDA, kwasababu wanafahamu muda huleta kitu kinachoitwa MABADILIKO katika nyanja zote za maisha: Binafsi, Kijamii, Kisiasa, Kiroho, Kiuchumi na Kitamaduni. Hivyo basi kuweza kukabiliana na MABADILIKO yanayoletwa na MUDA, wenzetu wakabuni kitu kinaitwa MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLANNING). Wenzetu walifahamu kwamba hawawezi kuzuia MABADILIKO lakini wanaweza kuyaratibu (MANAGE). You cannot stop changes, but you can manage and mitigate them.
================================================================================

Tanzania tumefika hapa tulipo kwasababu ya haya yafuatayo:
1. Hatutambui kwamba MUDA (An Independent Unit) ni rasimali inayoshikilia rasilimali zote.
2. Hatuukomboi MUDA/WAKATI (Sisi ni bora liende, ponda mali kufa kwaja)
3. Mabadiliko yanayoletwa na MUDA/WAKATI huwa yanatukuta tumelele usingizi wa pono.
4. Tunaamini kwamba utajiri wa nchi ni rasilimali watu na rasimali asilia pekee.
5. Hatufahamu kwamba, kama binadamu taifa nalo lina MUDA wa kuishi na kufariki.

Ndiyo maana wenzetu baada ya kufahamu haya, wakaanzisha taasisi za PREDICTIVE SCIENCES ambazo zina wataalamu ambao kazi yao kubwa ni kuweza kutengeneza PREDICTIVE MATHEMATICAL MODELS zilizojikita kwenye Wealth (Economy), Health and Weather ambayo wanasayansi wanaviita viashiria vikubwa mno vya maisha ya binadamu kwa miaka ijayo. Mwaka 2007, Prof David Orrell alindika kitabu kiitwacho
"Apollo's Arrow: The Science of Prediction and The Future of Everything" ambacho kimechambua vitu vingi sana na kuonesha jinsi gani MABADILIKO yanaweza kumvamia binadamu hata yule ambaye amejipanga vizuri kwa kutaka kutabiri nini kitatokea.

Hichi kitabu kilileta ushawishi mkubwa sana nchini Marekani, hadi kupelekea baadhi ya vyuo vikuu na taasisi kukifundisha kama kozi maalumu na hata baadaye idara nyeti za nchi zikaanza kufuatilia mapendekezo yake. Ukweli mchungu hata ambao Proff David Orrell anasema kuhusu MABADILIKO ni kwamba huwa hayagondi hodi. Akitolea mifano mingi kama Venezuela ya Hugo Chavez na majanga ya hali ya hewa yaliyoikumbwa nchi hiyo mwaka 2001. Kitu kama hichi msomi Philipp Coggan ambaye ni mchumi na mwandishi wa habari nguli kutoka The Financial Times/The Economist anasema kwamba huwezi kubashiri uchumi kwa asilimia 70% sahihi, mabadiliko huja bila hodi.
=================================================================================

Hivyo nini kifanyike hata kama hatuwezi kubashiri kwa usahihi nini kitakachotokea ???

Ni lazima tujipange, ili MABDILIKO yakifika tusichanganyikiwe na kuleta taharuki. Watawala wasiokuwa na ufahamu na uelewa huwa wanajidanganya kwamba watazuia mabadiliko. Kilichotokea 29 OKTOBA 2025 ni sehemu ya mabadiliko. Bahati mbaya serikali haikujipanga endapo jambo kama lile lingetokea, ikaadhimu kuua watu wake kikatili kwasababu ilichanganyikiwa (Panicked) kwasababu ilikutwa imelela usingizi wa pono.

Hili la vikwazo limewakuta vibaya, mmelala kwenye ukingo wa mto. Sasa imetokea taharuki kubwa ambayo badala ya kupunguza tatizo, inaonesha wazi kabisa kwamba serikali haina mbinu mbadala zaidi ya kuhonga madini na rasilimali. Hatujajipanga, na tumelela kando ya mto.

Hebu fikiria ikatokea kweli Marekani imepitisha ule MUSWADA kuwa sheria. Tanzania mmejipanga namna gani kukabiliana na hizi changamoto ??? Binafsi nasema ombeni sana isitokeaa, maana ikitokea, sijui aiseeeh.

=================================================================================
ENIWEI najua mada hii ni ngumu, lakini naamini wahusika wataelewa nachokisema.

Lakini ombeni sana maana yajayo yanafurahisha.

View attachment 3596335
​
Alafu anatokea mtoto wa buku mbili anakwambia mwenye bandiko hili hana elimu🤣🤣🤣🤣
 
Huyu aliyeropoka kwamba "Polisi walirushiwa mawe" hakutakiwa awepo pale.

Kwenye kikao Bibie karetewa kabrasha anaambiwa kwamba jamaa hafai.

Bibie kaanza BIG-BABBY TANTRUMS za kulia na kujifungia chumbani hataki kuongea na mtu.

Kisa, wanamdharau, kaomba aletewe ghahawa anywe peke yake ndani.

Kuona hali ni mbaya, ikabidi waliite lile lizee la Cold-War kazi maalumu ambalo halitaki kustaafu.

Lile lizee kufika na kuzungumza naye ndiyo kulazimisha hiki kituko kuwekwa pale ambapo unaliona leo.
========================================================================================

Huyu ni MWENZAO, MAKE NO MISTAKE...
​
Ooh yeah, codes zimezingatiwa.
 
Mtu mzima unaonesha ujinga hata kuandika hujui, hakuna capitalization na hata hoja yenyewe ni perfect example ya mtu aliyekula conspiracy theories za Telegram na WhatsApp mpaka zikaharibu uwezo wa kufikiri logically. Unachanganya Islam, communism, India, Iran, New York politics, Al-Qaeda, ukoloni, Zanzibar, Sahel, na “civilized world” kama blender ya mtu aliyechanganya bangi na YouTube shorts.

Kwanza huyo Zohran Mamdani unamuita “Mamdani muhindi/iranian communist Muslim mastermind” . Jamaa ni Ugandan-born mwenye roots za South Asian family, na “Kwame” si conspiracy yako ya Marvel universe. East Africa especially Uganda na Tanzania historically zina majina za Kiafrika across communities kutokana na mazingira ya walikozaliwa. Lakini kwa sababu brain yako imeamua “Muhindi hawezi kuwa na jina la Kiafrika,” sasa umejenga entire geopolitical theory juu ya assumption zako za vijiweni.

Na hiyo line yako ya “Muslims are communists” ndiyo inachekesha zaidi. Communists historically waliua na kufunga dini INCLUDING Islam . Soviet Union, Maoist China, Albania walikuwa anti-religion kabisa. Islam na communism zina conflicting foundations economically and philosophically. Lakini wewe umeona watu wawili usiowapenda then ukaamua kuwafanya same thing. Hiyo ni intellectual bankruptcy.

Halafu hii victim complex yako ya “wanajiita victims huku wanafanya fatwa” inaonyesha hujawahi hata kusoma maana ya fatwa . Fatwa si death sentence ya Hollywood movies. Fatwa mara nyingi ni scholarly opinion ya kidini kuhusu issue fulani. Lakini wewe umelearn Islam kupitia memes za Facebook na headlines za Fox News-level paranoia.

Na hii fantasy yako ya “Muslims wamejipanga miaka 100 kuanzisha caliphate Tanzagiza” bigot idiot touch grass. Tanzania ina Muslims na Christians tangu kabla hata state ya kisasa haijazaliwa. Watu wana biashara, ndoa, siasa, neighborhoods mixed for generations. Lakini kwa sababu Waarabu wamewekeza bandari au Wahindi wana biashara, ghafla umeona “secret Islamic takeover.” By your logic, Wachina nao wanaanzisha Chinese caliphate kwa sababu wana infrastructure projects Africa.

“Muslims wana financial muscle ndiyo wanashinda vita” kumbe sasa issue si theology, ni jealousy disguised as civilization theory . Ukiwaona watu wanafanikiwa biashara, instead ya kujifunza biashara unaanza kusema “they are organized to destroy us.” That’s loser mentality 101. Communities nyingi za Wahindi, Waarabu, na Pakistanis historically ziko biashara East Africa because walikuwa kwenye trade routes for centuries. History si conspiracy.

Halafu hii nonsense ya “ukoloni ulikuwa ku-save Africa from Islam” ndiyo imefika peak clownery. Europeans wenyewe waliandika wazi motives zao: resources, labor, trade routes, territorial control, imperial competition. Leopold hakwenda Congo “kuokoa civilization”; alienda kukata mikono za watu for rubber profits . British hawakuchora mipaka Africa sababu ya Yesu vs Muhammad anime battle. Walikuwa wanagawana wealth and power.

Na hii “civilized world vs Islam” rhetoric yako ni recycled post-9/11 propaganda ya watu wasioweza kutofautisha extremists na asilimia kubwa ya ordinary Muslims wanaotaka kula, kulipa bills, na kuishi maisha yao. Ukiwa intellectually serious, unaanalyze extremism kupitia geopolitics, failed states, foreign interventions, poverty, militia networks etc. Lakini wewe umeamua entire religion ya 2billion people ni hive mind ya secret conquest . Hiyo si intelligence; hiyo ni fear wrapped in pseudo-history.

Most embarrassing part ni confidence yako. Unaongea kana kwamba umeunlock hidden truth wakati actually una-repeat talking points za fringe internet boomers wenye profile picture za simba na bendera . Hakuna “laser-focused Islamic masterplan” hapa; kuna wewe kushindwa kuelewa dunia complex then brain yako inatafuta single villain wa kulaumiwa. Weak minds love simple enemies
Umefanya uchambuzi ulionyooka kumkosoa huyo kubwa jinga Kijakazi

Huyo jamaa hata mkewe akichukuliwa mkewe na wahuni wakina secretarybird na Maghayo atatupa lawama kwa Muslim na communism Wanataka kusambaza Uislamu katika familia yake
 
Mkuu fanya kutoa na effects matokeo kwetu sisi raia wa kawaida iwapo mswaada wa USA utapita. Tujue namna ya kujipanga mapema
Mswada unatamka ''kupitia mahusiano kati ya Marekani na Tanzania'' . Hii si vikazo vya uchumi (economic sanctions). Mswada unaeleza maeneo yasiyoathirika ikiwemo huduma za kibinadamu na usalama.
Usalama ndipo tulipoponea kwasasababu Tanzania ilikuwa ''stable' katika ukanda. Marekani inatumia kwa Usalama.

Kinachokusudiwa ni vikwazo kwa wanaohusishwa na matukio. Wahanga watawekewa vikwazo vya kusafiri na vijisenti vinaweza kuwa ''freezed''. Hawa wataonja joto ya jiwe moja kwa moja kwasababu hata Familia zao zitaathirika.

Mtu wa kawaida utalionja joto ''indirectly'' kutokana na kuathirika kwa baadhi ya maeneno.
Marekani ndio wenye Bretton Wood Institution iliyoanzisha World Bank (WB) na Internationa Monetary Fund (IMF)

Ukopaji unaweza kuathirika na kuathiri miradi ya ndani inayotegemea pesa. Mtiririko utaathiri ajira za Watu kwa mnyororo hadi mama ntilie ingawa anaweza asione athari moja kwa moja

Marekani ina masoko makubwa ya Mitaji. Wawekezaji watakuwa na wasi wasi na huenda wakahitaji ''ulinzi'' wa dhamana zao kwasababu tayari tutaonekana ''unstable country''. Uwekezaji ukiathirika na unagusa hadi chini

Misaada itapotea hasa ile inayopitia serikalini. Kumbuka misaada hiyo ni sehemu ya ''fedha''
Tunatumia Dollar kwa shughuli za biashara za nje na hata ndani. Dollar ikiathirika kidogo tu Tsh inakuwa matatani. Sina uhakika lakini inflation hatuwezi kuiondoa katika equation na ina athari kwa watu wa kawaida

Kubwa zaidi mswada unapelekwa kama sheria na kufutwa lazima urudi katika mabunge.
Ingalikuwa executive order ya Rais hiyo inafutwa mara moja pengine na Rais ajaye. Hapo napo kuna tatizo
 
Mswada unatamka ''kupitia mahusiano kati ya Marekani na Tanzania'' . Hii si vikazo vya uchumi (economic sanctions). Mswada unaeleza maeneo yasiyoathirika ikiwemo huduma za kibinadamu na usalama.
Usalama ndipo tulipoponea kwasasababu Tanzania ilikuwa ''stable' katika ukanda. Marekani inatumia kwa Usalama.

Kinachokusudiwa ni vikwazo kwa wanaohusishwa na matukio. Wahanga watawekewa vikwazo vya kusafiri na vijisenti vinaweza kuwa ''freezed''. Hawa wataonja joto ya jiwe moja kwa moja kwasababu hata Familia zao zitaathirika.

Mtu wa kawaida utalionja joto ''indirectly'' kutokana na kuathirika kwa baadhi ya maeneno.
Marekani ndio wenye Bretton Wood Institution iliyoanzisha World Bank (WB) na Internationa Monetary Fund (IMF)

Ukopaji unaweza kuathirika na kuathiri miradi ya ndani inayotegemea pesa. Mtiririko utaathiri ajira za Watu kwa mnyororo hadi mama ntilie ingawa anaweza asione athari moja kwa moja

Marekani ina masoko makubwa ya Mitaji. Wawekezaji watakuwa na wasi wasi na huenda wakahitaji ''ulinzi'' wa dhamana zao kwasababu tayari tutaonekana ''unstable country''. Uwekezaji ukiathirika na unagusa hadi chini

Misaada itapotea hasa ile inayopitia serikalini. Kumbuka misaada hiyo ni sehemu ya ''fedha''
Tunatumia Dollar kwa shughuli za biashara za nje na hata ndani. Dollar ikiathirika kidogo tu Tsh inakuwa matatani. Sina uhakika lakini inflation hatuwezi kuiondoa katika equation na ina athari kwa watu wa kawaida

Kubwa zaidi mswada unapelekwa kama sheria na kufutwa lazima urudi katika mabunge.
Ingalikuwa executive order ya Rais hiyo inafutwa mara moja pengine na Rais ajaye. Hapo napo kuna tatizo
Ahsante sana kwa elimu.

Hapa ni kufunga mkanda hasa
CCM sio kabisaa
 
Nafahamu jinsi hili dude linavyofanya kazi NJE-NDANI, na sidhani hao wanaojiita watoto wa mjini kama kuna hata mmoja angenishinda mimi. Hata siku moja. Awe ni Rostam, Jakaya, Makamba, Kinana, Rugemalila, Mufti Mkuu au Kadinali, wasingenithubutu hata kuinua kidole. Never On Earth!!! Kiukweli mnapowalalamikia wahuni wa nchi hii na WANAMTANDAO huwa nawashangaa mno. Binafsi nisingewasazia hata mjusi anayekaa kwenye dari za nyumba zao.

Sema tu, UPELE HUWA HAUMKUTI MWENYE KUCHA........
Duh!....Ila naamini usingeuwa mtu au kumpeleka Uhamishoni.
 
Umekumbusha kitu adhimu sana na mfano mzuri ni industrial revolution ilibadilisha nguvu ya dunia. Mabadiliko ambayo mataifa yaliyochelewa kutokwenda kwa mabadiliko ya viwandani historia ilionesha yalibaki nyuma.

Kuna mahali nilisoma wajuzi watafafanua zaidi, walionesha ya kwamba; mifumo mingi huanguka si kwa sababu haina nguvu bali ilichelewa kuutambua wakati sahihi. Yaani ilichelewa kutambua kuwa mazingira tayari yamebadilika.

Na historia ikitazamwa huwa inasema kwamba kila zama huwa zina teknolojia yake, fikra zake, kizazi chake n.k

Kwa bahati mbaya tatizo la mamlaka za kwetu zinadhani kuwa utulivu au kutumiwa nguvu na kulazimishwa utulivu kwenye mabano tuseme utulivu wa sasa basi ndiyo usalama wa muda mrefu. Wanaamini kwa kuwa mfumo unasimama basi upo salama.

Tunakoelekea si pazuri. Inabidi ieleweke kuwa mabadiliko ni sheria ya kijamii, ndiyo kanuni na nidhamu yake huwezi kupambana nayo. Njia iliyo bora ni kuyaratibu.
 
Back
Top Bottom