Ukiwa katika PR ama communications field , unachokisema hakina nguvu kama unakisemaje.
Sasa tatizo la CDM lipo katika kuchagua cha kusema na wanakisemaje. Lakini pia kufanya assumption kila mwananchi anajua kilichotokea 29 Oct au anajali sana. Ni kosa lingine pia kwa sababu kuna mikoa mingi hizo rapsha hazikutokea na kuna watu wengi ambao hawakuguswa directly lakini pia kuna kundi lililoikubali narrative iliyokuwa pushed na mass media
Imagine kwa hali unavyosema ipo, je inakuwaje Lissu yupo ndani almost mwaka lakini nguvu inayotarajiwa kumtoa ni ya nje zaidi kuliko wananchi husika.
Kama CDM ina nguvu na ushawishi huo ambao unadhani wanao. Kwa nini hakuna mitikisiko ama force kubwa kumtoa kutoka kwa wananchi ?..
Umeelewa point yangu sasa
Kama ningekuwa nipo ndani ya CHADEMA, nisingeongelea Katiba tu, ningejiumiza kichwa ni kwa nini watu wengi zaidi "wajali zaidi kilichotokea ama kinachopaswa kutokea"
Ndio maana sometimes siwaamini sana CDM kwa sababu kuna inconsistencies nyingi sana kwenye activities zao na sometimes wanabugi step au kubadili gia kirahisi. Pia Hit ikiwa kubwa ,viongozi huwa wanasaliti kambi kirahisi, rejea hali ya CDM baada ya uchaguzi wa 2020. Hii huwa inanipa mashaka kama kaburi lililopakwa chokaa, je ndani halina mifupa ya wafu ?....
Sipo CDM, sipo CCM , mimi ni mtanzania tu kwa hiyo sipo emotionally au mentally attached na hivi vyama. Nawe ukitoa kiasi hiyo attachment utaona picha halisi
I hope you do