Nini imesababisha hali hii kwa Watanzania wengi ? Inawezekana daraja la chini halina ugumu wa maisha labda kama Kenya? Ni elimu? Ni state propaganda ya nchi imekuwa smart sana? Nini hasa sababu??
Vipo vitu vingi sana ila nitahighlight vichache
Ujamaa uliondoa individualism, watu wakaacha kufikiria kama individuals na kuanza kuona usisi na kutegemea serikali kwa kila kitu. Huku wafanyabiashara na matajiri wakipigwa vita kama wahujumu uchumi ilhali wenye vichache wakaonekana wazalendo.
Hii ilifanya umaskini uonekane ni tunu na ni kawaida, extreme dependency kwa government "maendeleo ya hisani na si kwa stahiki" Kwa hiyo presha kwa viongozi katika kuuondoa ikaondolewa
Elimu mbovu, mtanzania wa kawaida hafundishwi basic business or economics. So hajui hata uchumi unaendaje, ni tofauti na Kenya ambapo home economics inafundishwa. Inawasaidia kujua serikali inapataje mapato na ina_spend vipi na ina maana gani . Hivyo wanajua jukumu lao ni nini lakini la serikali ni lipi ndio maana kwenye mgomo wao wa mafuta unaona wapo detailed kuhusu kodi zinazopigwa ila watanzania wataumia "serikali itupunguzie bei ya mafuta".
Hawajui hata serikali inaongezaje wala kupunguza bei ya mafuta na ukiongezwa poor reading culture. Bhasi tunakuwa na uninformed & data blinded society
Kuna role ya imani za DINI & USHIRIKINA. Watu kuamini katika Better days na siku mbaya zinazosababishwa na shetani. So yakitokea yoyote kuna ile comfort "Mungu atatulipia, Mungu ataleta ridhki", hii inaondoa individual responsibility ya kuondoa vitu kwa sababu MUNGU YUPO NA ATATENDA KIMIUJIZA. Na ikishindikana wataenda kwa mganga. So ile hali ya kuishurutisha serikali ifanye A B C ni ngumu kwa sababu tayari unaamini destiny yako ishaandikwa na supreme power hii inatengeneza mazingira ya viongozi kutokuwa accountable.
Hata kijamii binti akibakwa au akiuliwa, watu wanakaa chini wanayamaliza, sheria za nini na aliyefariki harudi na pengine "Mungu amepanga"
Bado kuna integration ya serikali na Chama aliyoifanya muasisi. Na hii ndio inaila taifa hadi leo, aliamini katika kutengeneza chama imara kama msingi wa uimara wa nchi badala ya kutengeneza wananchi strong ambao watapambania nchi. So mambo yalivyogeuka, Simba wakaanza kuongoza kondoo wanavyotaka kiurahisi kwa sababu mentally and emotionally washakuwa disarmed
Issue ya malezi traditional ndio ikatumaliza kabisa, kiongozi wa familia "baba", hasemwi, hupaswi kumjibu hata akikosea, anaweza kukukufanya chochote anachotaka na ukimya wako ndio obidience. Na hizi zipo applied kwa jamii nzima. Sasa kama mtu huwezi kum_face baba yako, utaweza kum_face kiongozi mkubwa wa nchi. Hata viongozi wanalijua hili ndio maana kwenye utetezi wao lazma " Maadili, heshima, tamaduni, malezi" Vitawekwa kwa sababu wanajua ukigusa hapo, umegusa kwenye core ya mtanzania yoyote yule. Kwa hiyo kiongozi akikosea, usimseme kwa lugha yoyote. Ongea nae kistaarabu, kwa heshima, upole na ustahimilivu, atakusikiliza. Yani mtu amekosea ila inabidi umfate kwa unyenyekevu. Hii ni tofauti na nchi kama Kenya
Kwa hiyo Topic ni ndefu ila inahitaji kitabu kizima na kichambuliwe. Natural nimejitahidi kukujibu