Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Kama unataka lockdown si ukae kwako ujifungie wewe na familia yako kwani nani atakuzuia.
Yaani watanzania wafe kwa njaa kisa Corona hebu tutumie akili kidogo tu kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawaijui kesho yao itakuwa vipi.

Sasa mnavyolazimisha lockdown wewe utawapelekea chakula au kisa baadhi yenu mnaotaka Hilo jambo mko vizuri kiuchumi na mmeajiriwa serikalini hali ya kuwa huko vijijini watu kula tu imekuwa shida halafu unataka wafungiwe wenzio ndani huu ni upumbavu uliopitiliza

NI KWELI CORONA INAUA NA LAZMA TUCHUKUE HATUA ILA LOCKDOWN NI JANGA KUBWA KULIKO CORONA

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali inafanya nini..wawape watu chakula..nchi ni watu au wanataka kuongoza "Ghost towns"
 
Mpaka sasa serikali imeshaonyesha ulinzi wa raia dhidi ya Corona awataki kujivika hayo majukumu.

Solution ni kwamba ‘abiria chunga mzigo wako’ hakuna namna.
Ndugu Mike2k, hakuna mtu anajali afya yako. Jiongeze mwenyewe. Huu ndo ukweli.
 
Back
Top Bottom