Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Leo tunaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe. Ili jambo likipita tunaweka kituo Bagamoyo na Kibaha, kila anaeingia Dar awe na kibari maalumu na sababu ya msingi.
 
Habarini wakuu poleni na majukumu pia poleni na changamoto ya huu ugonjwa wa covid19.

Moja kwa moja niende kwenye mada ,Uku mitandaoni kuna baadhi ya watu wanaotaka au kulalamikia serikali dhidi ya lockdown Dar ? Hivi kwanini watanzania wengi wanakua wazito kufikiri na ikumbukwe kuwa mgonjwa wa kwanza wa corona aliripotiwa Arusha ina maanakwamba corona sio dar pekee na pia wagonjwa wengi wameisha ripotiwa mikoa ya Mwanza n.k

Kwahyo hata kama ukisema ufunge Dar ni kazi bure bado kesi nyingi zitaripotiwa mikoani mfano kuna madereve waliokutwa na corona Uganda madereva wa Tanzania.

kama alivyosema raisi wetu mtukufu ukisema ufunge Dar kesho tena utafunga Arusha mara Mwanza na ukumbuke Dar ndio kitovu cha uchumi na pia sekta ya utaliii ambayo huchangia pato kubwa imefungwa sasa ukifunga Dar unategemea mapato ya serikali yatoke wapi

Afu badala ya kujikinga binafsi mnakaa kulaumu serikali baadala ya nyie mchukue taadhari mmoja mmoja na ungali mnajua kwa sasa hili janga halina tiba wengine hata maji ya kunawa wanayaweka ilimradi tu waonekane lakini hawazingatiii jamani siasa sio wakati wake sasa.

Nobody.
 
Mbona sijaona la maana kwa huu uzi?...mbona yale yake tu jaman! Msalimie mtukufu wako
 
Hao ni Chadomo wameshiba ruzuku hatukumbuki si wapiga kura wao
 
Njaa haina baunsa hao wanaotaka lockdow wana uhakika wa kula walau mwezi bila kufanya kazi sisi wazee wa hand to mouth mtatuua aisee, Halafu sasa ikishapigwa lockdown watu njaa ndani utaona hao activists tena wakianza kisaidia watu vyakula na camera kibao ili wazidi kujinua kisiasa wanaleta siasa kwenye Maisha ya watu waache kabisa, Kikubwa shughuli ziendelee na wananchi tuendelee kuchukua tahadhari kubwa
 
Nashauri DSM ifungwe ili nchi ishughulike na maambukizi kwa DAR, miko mingine iwe na ahueni kubwa, hili ni kuipa uwezo serikali ielekeze resources zote kwa dar na waushinde UGONJWA.

DAR tumenufaika sana na kuwa jiji kubwa na serikali kuota mizizi hapo, tukumbuke kila kwenye faida kuna hasara zake, iwapo faida za dar tunafaidi wana dar, tuwe waungwana hasara tuzibane dar pekee, sio ziachwe ziende nchi nzima.

Kuendelea kuw ana magari ,mabasi usafiri wa dar kwenda mikoa mingine ni kuilipua nchi kizembe sana

Nawasilisha
 
Huko walipoweka lockdown maambukizi yalienea au hayakuenea?

Kuna watu wasipotoka hawana ela ya kulisha familia kesho yake, wanalipwa kwa siku.

Kutangaza Lockdown Dar una maana private sector kwa sehemu kubwa ni kupunguza wafanya kazi.

Haya mambo wanaweza wenzetu ambao hawana njaa.

Ni kuomba rehema za Mungu tu.

Waafrika tuache ujuaji, ngoma iliwashinda mataifa makubwa na yenye uwezo wa kila namna.

Mungu ametusaidia waafrika maambukizi haya hayana athari kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifungie wewe na familia yako sisi tunachapa kazi usitufundishe uvivu

Binadamu tumepitia changamoto nyingi hili litapita pia
 
Kuendelea kuw ana magari ,mabasi usafiri wa dar kwenda mikoa mingine ni kuilipua nchi kizembe sana
Acha kupoteza muda Dar haifungwi
Mmeshaambiwa msisafiri pasopo ulazima
Mlitaka Dar ifungwe,watu wafe njaa ili mchochee maasi!tumewastukia
 
... ni wapi hakuna maambukizi muda huu Mkuu? Tulishaingia chaka basi tena hakuna namna! Tuchukue tu tahadhari na kumwomba Mungu.
 
Too late. Ugonjwa ushasambaa Tanzania Tanzania nzima. Cha muhimu baki nyumbani.
 
Nashauri DSM ifungwe ili nchi ishughulike na maambukizi kwa DAR, miko mingine iwe na ahueni kubwa, hili ni kuipa uwezo serikali ielekeze resources zote kwa dar na waushinde UGONJWA.

DAR tumenufaika sana na kuwa jiji kubwa na serikali kuota mizizi hapo, tukumbuke kila kwenye faida kuna hasara zake, iwapo faida za dar tunafaidi wana dar, tuwe waungwana hasara tuzibane dar pekee, sio ziachwe ziende nchi nzima.

Kuendelea kuw ana magari ,mabasi usafiri wa dar kwenda mikoa mingine ni kuilipua nchi kizembe sana

Nawasilisha
Too late raia kibao washakimbilia mikoani!!!
Kila mtu ashinde mechi zake
 
Back
Top Bottom