Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Hakuna maana ya kufunga mipaka ugonjwa ushasambaa

Mkuu hapa tufanye Dar, Zanzibar, Mwanza, Morogoro, na kote kuliko athirika.

Enyi serikali mmeshauriwa haya kabla ya ugonjwa kuingia. Mkashauriwa haya wakati ugonjwa uko Dar kwa nini hivi?

Mnataka hadi wafe wangapi?
 
Mkuu pambana na familia yako..hii ni vita,usitegemee ushikiwe akili jiongeze.
 
Asitoke wala asiingie mtu ndani ya jiji hili kwa muda wa siku 15, kwa kufanya hivi tutajiepusha na madhara makubwa sana yanayoweza kuwakumba mababu na mabibi zetu huko mikoani.
Magari ya mizigo tu ndio yaruhusiwe kupita, tudeal na huu ugonjwa humu humu mpaka tuukomeshe kabisa, ni rahisi zaidi kuliko ukisambaa huko mikoani, tutakuja kulaumiana sana hapo baadae, ni ngumu kuamini, ila RC ndio kashikilia uhai wa WaTanzania milioni 60 kwa sasa, yeye ndiye ataamua tufe au tuishi.
Na hapa ndio tunaona umuhimu wa kushiriki katika siasa, tusikubali watu wachache wakahodhi madaraka yote, ni hatari sana!

=====================================
Naomba ifanywe kwa dharura: Napendekeza kuanzia Jumamosi iwe ni marufuku mtu kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa/ barakoa/ scarf - JamiiForums
 
Back
Top Bottom