Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Ukipuuza ushauri wa kitaalamu au usubiri hadi Serikali itakapoweka karantini, kama unavyoshauri, utaambukizwa na kupoteza maisha.

Ni wajibu na jukumu la kila mwananchi kulinda afya yake.
Kwa maneno yako una maanisha mwananchi asiitegemee serikali maana haina hadhi ya kuaminiwa wala kutegemewa na wananchi!!

Korona ilianza baada ya serikali kukaidi kuzuia ndege na kufunga mipaka, sasa hivi hali imekua mbaya mnasema mwananchi ajilinde je wakati wa kuzuia ndege mlitaka wananchi wazizuie?

Korona imetupa picha halisi ya serikali yetu!!
 
Bata za Dar tule wote yakiaribika watunyanyapae hatutaki tufe wote.
 
Hatukubali, na nyie mletewe kama sie tulivyoletewa

Kwani sie hii corona tulizaliwa nayo?

Mwenge hauruki kijiji, jiandaeni

Sent using Jamii Forums mobile app

Kabla hujajibu tafakari kwanza mkuu.

Wewe ni member mkongwe na linapokuja suala la msingi ni vema ukajitenga na wanafunzi ambao kwao kuandika chochote sio jambo la ajabu.

Tushirikiane tuangalie jinsi ya kuzuia maambukizi zaidi.
Hii hali tusipoisaidia serikali hata kwa ushauri unadhani tutaishia wapi?

Unaposikia nchi za wenzetu watu 2000 au zaidi wanakufa ndani ya saa 24 ujue sio ugonjwa wa mzaha.

Tuungane pamoja mkuu.
 
Naona serikali inawaachia wale wenye hofu ya kupata Corona wakimbie na familia zao kwenda huko vijijini kwao kwanza. Nimeona jana wanapimwa Corona wote wanaosafiri kituo cha ubungo stand ya mkoa. Wale watakaobaki ndio wanaweza kupitiwa na lock down. .
 
Kwako Mkuu wa mkoa wa Dar au mamlaka ya juu (rais)

Kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 na takwimu zinazotolewa kila siku na Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, ni dhahiri kuwa jiji la Dar limekuwa kitovu cha ugonjwa huu hapa nchini. Kila siku idadi ya wagonjwa inapanda kwa kazi sana.

Nashauri mamlaka husika mfuate ushauri wangu ili kupunguza kazi ya maambukizi nchi nzima.

Ikiwapendeza au ikiwezekana ushauri huu ufanyiwe kazi mapema iwezekanavyo kwa kuwa kila siku mabasi na vyombo vya abiria vinaingiza na kutoa watu kwenye hilo jiji.

Naomba kuungwa mkono.

Nawasilisha.
Kwa akili zako unafikiri serikali haijui inachofanya EBU TUPUNGUZE UJUHAA

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Ukipuuza ushauri wa kitaalamu au usubiri hadi Serikali itakapoweka karantini, kama unavyoshauri, utaambukizwa na kupoteza maisha.

Ni wajibu na jukumu la kila mwananchi kulinda afya yake.

Nakubaliana nawe ila elewa maana yangu; NINAPOSHAURI KUFUNGWA KWA JIJI NAMAANISHA WATU WALIOKO DAR WAENDELEE KUFANYA KAZI (KWA TAHADHARI) WASITOKE NJE YA DAR NA WALIOKO NJE YA DAR WASIENDE DAR.

Kwa maana hiyo kuenea kutadhibitiwa Dar na maambukizi hayatasambaa kwa kasi sana.

Pia kuhusu vyakula, magari ya mizigo yanaweza kupeleka vyakula na ni rahisi kuyanyunyizia madawa kabla na baada ya kuingia/kutoka Dar.
Hivyo hivyo na mizigo ya biashara Inawezekana ikapelekwa mikoani kuwa utaratibu huo wa magari ya mizigo ambayo ni rahisi kuyadhibiti.
 
Acha usumbufu, tuko busy na maombi![emoji16][emoji16][emoji16]
mc_makunza_B_Fy_K4F2nG.jpg
 
Hapa ni kujiongeza wakuu. Mkisubiri serikali ya huyu baba ohooo....

Wewe na familia yako mkiweza kubaki nyumbani bakini. Wenye njaa waacheni wakatafute.
 
Nakubaliana nawe ila elewa maana yangu; NINAPOSHAURI KUFUNGWA KWA JIJI NAMAANISHA WATU WALIOKO DAR WAENDELEE KUFANYA KAZI (KWA TAHADHARI) WASITOKE NJE YA DAR NA WALIOKO NJE YA DAR WASIENDE DAR.

Kwa maana hiyo kuenea kutadhibitiwa Dar na maambukizi hayatasambaa kwa kasi sana.

Pia kuhusu vyakula, magari ya mizigo yanaweza kupeleka vyakula na ni rahisi kuyanyunyizia madawa kabla na baada ya kuingia/kutoka Dar.
Hivyo hivyo na mizigo ya biashara Inawezekana ikapelekwa mikoani kuwa utaratibu huo wa magari ya mizigo ambayo ni rahisi kuyadhibiti.
Ushauri wako ni mzuri ila kama tulivyoshauri ndege zizuiwe tukapuuzwa wenda ukapuuzwa na wewe.
 
We bila kuitaja chadema domo huwa linanuka??
Ujinga huo
Mkitaka lockdown, ongeeni na CHADEMA waseme kwasababu shughuli za kawaida hazijazuiwa na wao wanaingia kwenye shughuli za kawaida za kukijenga chama. Walahi kesho haitafika bila kutangazwa total of total lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umelazimishwa kuja dar?? Ebu baki zako uko kwenu ngopyoro uone km kuna atakaye angaika na wewe.
Aliye Dar asitoke nje ya Dar. Na aliye nje asiingie, utaratibu wa wageni kutoka nje ya Tanzania wa kuwekwa chini ya uangalizi kwa siku kadhaa uendelee, Mambo mengine ndani ya dar yaendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom