Muda sahihi wa kumuaga mtu aliyekufa ni wakati yuko hai, sio kwenye jeneza. Msimamo wangu mpya

Haya TUANZE KUKUAGA WEWE MUDA HUU

Ulale mahali pema peponi matunduizi
Tukiwa hai ndio muda sahihi wa kuagana. Kama kuna kitu kizuri cha kuambiana au kusaidiana ni wakati tuko hai. Mtu akifariki anatakiwa kuhifadhiwa kwa haraka, ili waliohai waendelee kuagana. Umakini mkubwa unaopelekwa kwa maiti ungepelewa kwake wakati yuko hai ungekuwa na faida kubwa sana.

Mfano akiwa hai ulimchukia, kafa unampenda unalia hadi unagalagala chini. Hapo unamchanganya hadi ibirisi.
 
Mungu akupe haja ya moyo wako,ukifa kataza pia ndugu zako wasikuzike!
 
Hukumwona? Angalia tena:

View attachment 3119553
Anayesema yote, anasema yote yapi inaonekana kuna mambo alikuwa anaongelea. Maana ukisema Yote kwa ujumla basi hata Mungu ni ubadili. Maana yote hapo inakuwa kama kokoro.
Labda kama ukionyesha anazungumiza yote kuishi na kufa.
 
Kuaga ni neno tu! Lengo hasa la pale ni kuuona/ kumuona kwa mara ya mwisho.
Mnakuza mambo tu hapa. Utamuaga vipi mtu aliye hai kama sio kutaka kukamatana uchawi.
 
Mungu akupe haja ya moyo wako,ukifa kataza pia ndugu zako wasikuzike!
Kuzikwa ni amri ya Mungu. Mwanadamu uu mavumbi hakika mavumbini utarudi. Ndio maana Mungu mwenyewe aliendesha mazishi ya Musa. Akiwa mwenyewe na maiti ya Musa akaizika mlimani.
 
Yaani hao wagonjwa unaenda kuwaambia kwa heri naona unakaribia kufa? Kwani kifo usababishwa na uginjwa tu? Vipi kuhusu ajali za namna nyingi tu, ikiwemo kutandikwa risasi kama yule dada Acquilina? Hauwezi kuagana na mtu kuwa atakufa baada ya muda mfupi wakati hujui siku wala saa wala sehemu.
Ms R
 

Hii tabia ya kuaga tumecopy kwa Wazungu kwa sababu hatutumii akilizetu kufikiri (kila kitu ni copy paste).
Baadhi ya watu huenda kuaga ili wapate cha kusema baadae, alikonda, ali.......nk nk nk
Kimsingi kuaga kuna wahusu ndugu wa karibu kabisa na hii hutumika pia kuondoa utata unaoweza kujitokeza baadae kuwa, aliyezikwa sio mwenyewe nk nk nk Waislam wanalijua hilo na kulitekeleza kwa vitendo.....
 


Tatizo utakuwa unawatembelea wagonjwa kwa Dhana hiyo na hapo ni kuchuria wagonjwa
 
Kuzikwa ni amri ya Mungu. Mwanadamu uu mavumbi hakika mavumbini utarudi. Ndio maana Mungu mwenyewe aliendesha mazishi ya Musa. Akiwa mwenyewe na maiti ya Musa akaizika mlimani.
Kwakua hukuwepo wakati Musa akifa basi chukua fursa hii kukiri kwamba habari hii ni ya kufikirika na ni myth
 
Kuaga ni neno tu! Lengo hasa la pale ni kuuona/ kumuona kwa mara ya mwisho.
Mnakuza mambo tu hapa. Utamuaga vipi mtu aliye hai kama sio kutaka kukamatana uchawi.
Kwa maana nyingine namaanisha hizo huruma tujifunze kuwafanyia wakiwa hai.

Mfano mimi ndugu yangu aliumwa, nikajizungusha kwenda kumuona akiwa hai bila sababu ya msingi. Akaruhusiwa, yuko jirani tu lakini nikawa nahairisha siku nasema naenda jioni nauliza mtoto wake wananiambia muda mfupi umepita wamemleka mochwari amefia ndani dakika chache zimepita.

Sasa uzito wa kijinga wa kuwaona watu wenye matatizo wakiwa hai unapelekea kuwa na unafiki mwingi wakati wa misiba.
 
Tatizo utakuwa unawatembelea wagonjwa kwa Dhana hiyo na hapo ni kuchuria wagonjwa
Mtu yeyote awe mzima au mgonjwa anauwezekano wa kufa sekunde yoyote. Muda wowote unaokutana na mtu utumie kama muda wa thamani na kumpa heshima zote maana hakuna haja ya heshima kwa kitu qmbacho hakiwezi kutambua unachokifanyia wakati ulikuwa na fursa ya kufanya hivyo akiwa hai.
 
Ni kweli, wabongo tunapenda vimaneno vya kichinichini na umbeya, wengine wanaaga kama uchunguzi tu, ndio maana wanatamani hata wapige picha kirisi maiti ili wasambaze. Waislam kwa hilo nawaunga mkono.
 
Wacrist wana complicate mambo sana, tangia lini gogo likaagwa!!? Khaah!,
 
acha watu waone mtu akiwa amefariki ili wajifunze nao wajue inakuwaje inajenga ujasiri pia.
 
tunaaga sio kwa ajili ya marehemu,ni kwa ajili yetu kwamba tumemuona sura halisi ndugu yetu kwa mara ya mwisho akiwa amelala.
 
Wacrist wana complicate mambo sana, tangia lini gogo likaagwa!!? Khaah!,
You're such a shit! usimpinge mtu kutokana na dini yake maana hata wewe ungezaliwa ktk ukristo unge- behave hivyohivyo na ungeona upo sahihi kama vile unavyoona sasahivi upo sahihi!..

usahihi wa mwanadamu upo kama havunji sheria za nature tu!
kuona mtu aliefariki inaweza kutokea muda wowote haijalishi ktk mazingira gani,unaweza kuachiwa mgonjwa umuangalie na akafia mikononi mwako!.
kifo kipo ktk mazingira yetu na ni maisha yetu so kukiona sio kitu cha ajabu,kua kiakili sio unakua mwili tu!.
 
Uko sahihi kqbisa. Kiwango cha juu cha ukomavu wa kimaisha ni kuheshimu maamuzi ya mwingine. Ndio maana hata mimi nimefanya kuwa jambo binafsi.
 
Hapa tunachokiongelea ni kumuaga maiti na co kuiona maiti, kuaga na kuona ni vitu 2 tofauti, alafu unaposema hata mimi ningekua uko ningefanya nyie mfanyavyo, nasema nisingefanya kwa7bu huwa sifanyi jambo eti kwavile wengi wanaufanya, mimi nafanya jambo baada ya kutafuta ukweli wa jambo husika.

Usifuate mkumbo tafuta ukweli wa mambo unayoyafuata, Elimu haina mwisho mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…