Muda wa Che Malone kukaa bench umefika

Tambala mbovu njoo umtetee tena Fondoh Malone.
Kila mechi anarudia kosa kiasi kwamba maadui wameshajua upuuzi wake.
Hatuwezi kuheshimu jina, tunaheshimu uwezo bila kujali jina.
 
Hata ile mechi dhidi ya Sfaxien hapa dar alifanya makosa ya kipuuzi ni vile tu wale jamaa hawakufunga . Hapo hamna beki labda abadilike ila sio beki tegemeo.
Hapana walifunga walifunga.
 
Mkuu kurudisha nyuma sio tatizo lakini unarudisha nyuma mpira katika mazingira gani?
 
Uchovu amecheza match nyingi mnoo bila kupumzika. Wenzake wanaumia na kupumzia. Yeye back to back
 
Uchovu amecheza match nyingi mnoo bila kupumzika. Wenzake wanaumia na kupumzia. Yeye back to back
Mkuu makosa yanayo fanywa na Chemaloni hayana uhusiano wowote na uchovu bali yana sababishwa na kutokuwa makini kwenye majukumu yake ,na ameanza kufanya makosa tangu msimu wa kwanza anakuja lakini watu walikuwa wana mpotezea kwa kudhani angebadilika lakini wapi.

Kiufupi malone kwa sasa sio beki wa kuaminika na kutegemewa kabisa.
 
Nadhani jana uliipta nondo nyingne ya che maleone
 
Nadhani imefika wakati sasa Marlone aondoke kabla Simba haijalizwa vibaya..Mistakes zimekuwa za kujirudia tena kwenye mechi muhimu.Kama kuvumiliwa ameshavumiliwa vya kutosha ,kwanza anapenda sana kugeuzia ndani hii ni hatari sana kwa afya ya timu.Maadui wamepress yeye bado anarudisha mpira nyuma..akili za kiwaki kabisa.
 
Zile beki zote za Simba Zina shida wakikutana na timu inayopress kwa nguvu mda wote zinapoteana vibaya sana,,kwanza hawana Kasi ukiwapelekea moto mara kwa mara wanajichanganya vibaya sana wote na Hamza ni wazito Tena yule charabou ndio ovyo kabisa!
 
Kwani pale alikuwa anageuza au alipiga pasi bahati mbaya ikawa fupi ikanaswa
 
Mwalimu atakuwa ameona namna anavyofanya makosa, kwa vyovyote vile akiendelea kumuamuni, michezo inayofuata ni hatari.
 
Kama si Hongo kwa refa, Jana akustahili kuendelea na mchezo, Red card ya wazi ilimuhusu.
Bahati ni mechi za shirikisho hakuna anaye jali kwakua Zina hadhi ya Ndondo cup.
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu,pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…