Muda wa Che Malone kukaa bench umefika

Muda wa Che Malone kukaa bench umefika

Nakusaidia tu kama hautaki kuona makosa kwenye mpira kaangalie mbio za Baiskeli kule hakuna makosa ya kujirudia rudia.
Mpira wa miguu sifa yake ni uwepo wa makosa ambayo ndio msingi wake.
Nitajie beki mzuri nchi hii kuliko Che Malone kwa sifa zote unazo taka.
1.Libero
2.Sweeper
Aina zote za beki wakati na sifa zao hakuna kama Che Malone Labda mpira una angalia ukiwa na mawazo kichwani.

#Jicho la kitaalamu sio jicho la kishabiki....!!! Mfano wakati Tanzania tuna sema Baka wa Yanga ni beki Bora nchini.Aliye kuwa kocha wake Nabi akiwa Far Rabat wakati ana hitaji beki wa kati aliomba timu imesajili Inonga na akisema ndio beki Bora kwa Sasa Tanzania, Je hakumuona Baka ambaye alimfundisha ?
Ukifatilia Interview ya Nabi ameongea kitaalumu Sana kuhusu ubora wa Inonga na sio Baka wetu.
Sasa basi tuna shida ya kuelewa mpira na misingi yake.
Tambala mbovu njoo umtetee tena Fondoh Malone.
Kila mechi anarudia kosa kiasi kwamba maadui wameshajua upuuzi wake.
Hatuwezi kuheshimu jina, tunaheshimu uwezo bila kujali jina.
 
Hata ile mechi dhidi ya Sfaxien hapa dar alifanya makosa ya kipuuzi ni vile tu wale jamaa hawakufunga . Hapo hamna beki labda abadilike ila sio beki tegemeo.
Hapana walifunga walifunga.
 
Chemalone apumzishwe kwanini awe anarudia makosa yaleyale Kila Mara.
Hamza naye ajifunze kufanya marking, mfungaji alikuwa peke yake badala ya kumkaba akawa anamuangalia mpaka alipopokea mpira.
Huu mchezo wa back pass tulishausema lakini wanapenda nandio unasababisha magoli ya hovyo.
Mkuu kurudisha nyuma sio tatizo lakini unarudisha nyuma mpira katika mazingira gani?
 
Huyu beki wa simba amekuwa na makosa mengi ya kijinga ambayo yamekuwa yakiigharimu timu.

Jana kasababisha goli kwa kosa la ajabu na lisilo ingia akilini kabisa.

Kwenye mechi ya Algeria aliokoa mpira kwa kupiga kichwa cha kindezi akasababisha goli, bado hatujaongelea makosa yake ambayo yamefutwa na goli kipa na mabeki wenzie.
Hiyo nimetoa kama mifano lakini ni huyu jamaa anafanya makosa karibia kila mechi.

Watu wana husisha makosa yake na kujiamini kupita kiasi lakini sio kweli bali ndo uhalisia wake ,kwa sababu makosa yake yamekuwa yakijirudia karibia kila mechi.

Sasa nadhani ni muda wa kuanzia bench labda ataanza kufanya majukumu yake kwa umakini.
Uchovu amecheza match nyingi mnoo bila kupumzika. Wenzake wanaumia na kupumzia. Yeye back to back
 
Uchovu amecheza match nyingi mnoo bila kupumzika. Wenzake wanaumia na kupumzia. Yeye back to back
Mkuu makosa yanayo fanywa na Chemaloni hayana uhusiano wowote na uchovu bali yana sababishwa na kutokuwa makini kwenye majukumu yake ,na ameanza kufanya makosa tangu msimu wa kwanza anakuja lakini watu walikuwa wana mpotezea kwa kudhani angebadilika lakini wapi.

Kiufupi malone kwa sasa sio beki wa kuaminika na kutegemewa kabisa.
 
Kwanza nadhani hauna uelewa mkubwa kwenye Eneo la mpira maana umetoa tuhuma za Moja Kwa moja kwake.
Mechi ya Simba na Constantine alijifunga Hamza ni beki mbaya ?
Malone ana kawaida ya kujiamini akiwa na mpira, na hii sio kosa ni kwa sababu ana control nzuri mguuni, Jana alijaribu kupiga chenga ikishindikana Ika naswa Simba ikafungwa.
Je kosa Hilo limeondoa ubora wake ? Jibu ni Hapana kwa sababu kupiga chenga ndani ya box la Simba amefanya mara nyingi Sana na ana fanikiwa na kupongezwa. Kwa Nini kocha alimtoa ? Jibu ni kwa sababu Baada ya kupinga chenga ikashindikana akasababisha goli alipata presha kubwa muda mwingi hakuwa mchezoni.Ili kutunza ubora wake kocha aliamua kumtoa Ili kumpa muda wa kukaa sawa Kwa mechi zingine.
Mwisho TUNAPO toa maoni tuwatendee haki wale tunao watolea maoni kwa sababu wao hawapati nafasi ya kujibu hoja zetu.

Mwisho nitajie makosa ya Malone kwenye mechi Tano ndani ya ligi na makosa mawili tu kwenye mechi za Kimataifa Ili nipate mwanga wa udhaifu wake.
Nadhani jana uliipta nondo nyingne ya che maleone
 
Nadhani imefika wakati sasa Marlone aondoke kabla Simba haijalizwa vibaya..Mistakes zimekuwa za kujirudia tena kwenye mechi muhimu.Kama kuvumiliwa ameshavumiliwa vya kutosha ,kwanza anapenda sana kugeuzia ndani hii ni hatari sana kwa afya ya timu.Maadui wamepress yeye bado anarudisha mpira nyuma..akili za kiwaki kabisa.
 
Zile beki zote za Simba Zina shida wakikutana na timu inayopress kwa nguvu mda wote zinapoteana vibaya sana,,kwanza hawana Kasi ukiwapelekea moto mara kwa mara wanajichanganya vibaya sana wote na Hamza ni wazito Tena yule charabou ndio ovyo kabisa!
 
Mimi nimecheza mpira siyo wa kutazama tu. Kwa mfano, kocha alikuwa anasema, ni kosa kubwa kugeuzia ndani, ni lazima ugeuzie nje na ukishindwa toa mpira nje ili wenzako wasogee mjipange upya.

Makosa anayofanya Malone ni ya kitoto si ya kufanywa na mtu mwenye jina kama lake. Kwanini hakugeuzia nje bali akageuzia ndani kwa pasi fupi? Tofautisha kati ya confidence (kujiamini) na over confidence (kujiamini kupita kiasi). Over confidence ina hasara pia. Malone akiendekeza over confidence atakuwa anachomesha tu!

Malone alikuwa na uwezo wa kugeuzia nje na kupiga volley au kutoa nje ila volley ndio ilikuwa sahihi
Kwani pale alikuwa anageuza au alipiga pasi bahati mbaya ikawa fupi ikanaswa
 
Mwalimu atakuwa ameona namna anavyofanya makosa, kwa vyovyote vile akiendelea kumuamuni, michezo inayofuata ni hatari.
 
Kama si Hongo kwa refa, Jana akustahili kuendelea na mchezo, Red card ya wazi ilimuhusu.
Bahati ni mechi za shirikisho hakuna anaye jali kwakua Zina hadhi ya Ndondo cup.
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu,pole sana
 
Back
Top Bottom