Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Nafikiri sheria tunayotumia kwa sasa ya kuanza safari saa kumi na mbili (06h00) asubuhi ni sheria ya miaka ya nyuma na hivyo inaweza kuboreshwa kwani mambo yamebadilika sana
Fikiria safari za Morogoro to Dar unalazimisha basi liondoke saa 12 asubuhi hivi kweli hicho kipande kina hatari gani hadi mabasi yazuiwe kuondoka labda saa kumi ya alfajiri?
Watu wanahitaji kuwahi kazini au biashara kariakoo na jioni warudi , tunadumaza uchumi.
Safari za kutoka Arusha au Moshi kwenda Dar/Moro una lazimisha basi liondoke saa kumi na mbili wakati hiyo miji karibia imeungana (kuna hatari gani?)
Natamani tufikie mahali tuwe na mabasi yanayosafiri usiku kwa vile vipande salama. Mf basi litoke Arusha 12 jioni lifike Dar saa 11 alfajiri hapo ndio tutakuza uchumi na sio watu kwa mamia kushinda kutwa nzima barabarani badala ya kuzalisha
Kuruhusu mabasi yote saa kumi na mbili kunafanya kuwe na mabasi mengi sana barabarani kwa wakati mmoja na hivyo kusababisha mashindano yanayoweza kuepukika au kupunguzwa.
TUngeweza kuanza na miji michache inayoonekana kutokuwa na hatari; Namaanisha mabasi yaruhusiwe kuondoka kuanzia saa kumi ya Alfajiri