Nafikiri sheria tunayotumia kwa sasa ya kuanza safari saa kumi na mbili (06h00) asubuhi ni sheria ya miaka ya nyuma na hivyo inaweza kuboreshwa kwani mambo yamebadilika sana
1. Fikiria safari za Morogoro to Dar unalazimisha basi liondoke 06h00; hivi kweli hicho kipande kina hatari gani hadi mabasi yazuiwe kuondoka labda saa kumi ya Alfajiri?
watu wanahitaji kuwahi kazini au biashara kariakoo na jioni warudi , tunadumaza uchumi!
2. Safari za kutoka Arusha au Moshi kwenda Dar/Moro una lazimisha basi liondoke saa kumi na mbili wakati hiyo miji karibia imeungana (kuna hatari gani?)
3. Natamani tufikie mahali tuwe na mabasi yanayosafiri usiku kwa vile vipande salama. Mf basi litoke Arusha 18h00 kufika dar 05h00) hapo ndio tutakuza uchumi na sio watu kwa mamia kushinda kutwa nzima barabarani badala ya kuzalisha
4. Kuruhusu mabasi yote saa kumi na mbili (06h00) kunafanya kuwe na mabasi mengi sana barabarani kwa wakati mmoja na hivyo kusababisha mashindano yanayoweza kuepukika au kupunguzwa.
TUngeweza kuanza na miji michache inayoonekana kutokuwa na hatari; Namaanisha mabasi yaruhusiwe kuondoka kuanzia saa kumi (04h00) ya Alfajiri
Sisi bado tupo kwenye karne ile ya primitive communalism na tunalazimisha kuwepo kwenye the world of high technology.
Kumbuka kuwa bado hatujawa na sheria ya kuruhusu kufanyika kwa baadhi ya Kazi 24hrs.
Mfano TRA, BANDARI,VIWANJA VYETU VYA NDEGE KUKOSA MIUNDO MBINU YA KUPOKEA NDEGE ZINAZOSAFIRI USIKU,LABDA VIWANJA VICHACHE TU.
Bado tuna zile Imani za zamani kuwa muda wa usiku ni muda wa uzazi na sio wa serikali au kufanya Kazi.
Nini kifanyike.
Viongozi wetu wakisafiri wawe wanaenda na wataalam ili kuiba idea na knowledge ili itusaidie.
Mfano. Suala la usafiri wa kwenda morogoro na baadhi ya mikoa ambayo ni Salama, iwe 24 hrs ilimradi ruti ndefu ziwe na madreva wawili.
Tuweke taa katika viwanja vyetu vya ndege,kuviboresha kuendana na international standards hasa hasa kuwe walau na sehemu mbili za kuruka ndege mbili kwa wakati mmoja,kutua napo iwe hivyo hivyo na sehemu za kupaki ndege na matengenezo, magari hata walau kuanzia 4 makubwa ya kuzima moto.
Kuruhusu ndege kutua usiku na mashirika ya ndege yaweze ku-encourage safari za usiku japokuwa najua usafiri wa ndege usiku bei yake ni ndogo kulinganisha na usafiri wa mchana.
Bara bara zetu kiukweli zina tatizo Sana,hakuna taa,msururu wa magari ya mizigo na yanatembea taratibu Sana,yanapaki bara barani mara kwa mara na pia mengine kuharibika bara barani,pia ni kama one way.
Ushauri
Tuanzie pale ambapo mwendazake ameishia,tuige idea yake tu, japokuwa kuna SGR, bado morogoro road itengenezwe hadi moro kwa njia zile zile nane,itasaidia sana maana kila weekend, kunakuwa na msururu wa magari mengi kwenda mikoani,huku magari makubwa nayo mara yaanguke,mara ajali,mara limeharibika,basi hapo kukaa bara barani kwa zaidi ya saa nne na kuendelea ni kawaida Sana. Tunakosa mapato kwa njia hyo.
Pia bara bara zetu walau serikali ianzie kuachana na kutengeneza bara bara za njia mbili, iwe ni sheria kuwa na njia sita kwenda mbele.
Mwisho ni kuwa bank, ATM,mpesa na tigo pesa ziwe nazo 24 hrs katika maeneo Kama hayo ya magari kama hapo mbezi itakuwa ni vizuri zaidi.