Muda wa kuanza safari za mabasi uangaliwe upya

Saa 12 kamili ni kama sheria, hata Flight nyingi zinaruka muda huo
Usiingilie fani za watu (flight) ambayo huna Elimu nayo wala usifananishe mada ya MABASI na Ndege;
Flight zinaruka 06h00 kwa sababu
1. viwanja vyetu vingi havina miundo mbinu ya kusupport ndege kuruka /kutua usiku au niseme havina taa kwenye run way.
2. Vindege vingi vidogo vilivyopo nchini vina engine moja ambayo sio salama kuruka usiku hivyo haviruhusiwi
 
Nimeandika flight nyingi zinaruka saa 12 asb… Wewe taja sababu z kuruka…suala la mie kuingilia fani za watu linatokea wapi?

au kujua muda wa ndege kuruka inahitaji kuwa kwny field hiyo?
 
Una mawazo mazuri ila hapo namba 4 hata yakiruhusiwa mabasi mfano ya Mwanza tu yaondoke saa 12 asubuhi bado yatashindani tu maana kushindana ni ugonjwa uko kichwani kwa madereva Wengi wa mabasi inabidi wapimwe saikolojia zao.
Suluhisho moja wapo ni sgr kukamilika
 
mkivamiwa barabarani mtaanza kulalamika ,mkipata ajali mfululizo mtalalamika pia
 
Nimeandika flight nyingi zinaruka saa 12 asb… Wewe taja sababu z kuruka…suala la mie kuingilia fani za watu linatokea wapi?

au kujua muda wa ndege kuruka inahitaji kuwa kwny field hiyo?
kwa taarifa yako ndege nyingi kubwa za safari ndefu huruka USIKU na ndege za safari fupi kama lisaa moja huruka mchana
Simple logic: hivi una haja ya kupanda ndege ya kwenda zanzibar kutokea Dar saa sita usiku ufike saa sita na dkk 20
au upande ndege kilimanjaro saa nane usiku ufike dar saa tisa ya usiku???
Muwe mnafikiria basi kabla ya kuandika!
 
Hivi povu lote la nini?

Rudi kasome comment yangu vyema uielewe

Nimeeleza ndege zetu nazo huwa zinaruka saa 12 asbh kama Mabasi. Hii ni fact…sikuwa na personal opinion sasa Wewe unaibuka na ufafanuzi wa nini?


Akili yangu imewaza mie nataka ndege ziruke usiku wa Manane badala ya pia kuhisi pengine logic yangu Ndege ziruke saa 3 asbh ili kuepusha adha ya kuamsha watu saa 10 alfajir wakati anaweza kuamka saa 12 asbh akaja kupanda ndege


 
Sisi bado tunaamini usiku ni muda wa nchi nzima kulala ndo maana hoja kama hii yakurekebisha muda wakusafiri hakuna anayeiwaza..

Kuna mambo mengi tungeweza kuyafanyia maboresho kulingana na kasi ya dunia ila sisi bado tumelala.

Hatutaki kutumia vichwa vyetu kutatua changamoto bali tunataka kutumia vichwa kukwepa changamoto.

Sasa kwa hali hiyo tutachelewa sana kupatia ufumbuzi wakudumu matatizo yetu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hivi povu lote la nini?

Rudi kasome comment yangu vyema uielewe

Nimeeleza ndege zetu nazo huwa zinaruka saa 12 asbh kama Mabasi. Hii ni fact…sikuwa na personal opinion sasa Wewe unaibuka na ufafanuzi wa nini?
Tatizo lako unafanisha ndege inayotoka Dar to Kilimanjaro kwa dakika 60, na BASI linalotoka Dar to Arusha kwa masaa 11
hii ni sawa na mtu anaye fananisha Kuku na mbuzi???
Na kwa taarifa tu: ndege zinaruhusiwa kuruka masaa 24 kama ndege yenyewe na kiwanja kimekidhi vigezo ila kwa sababu ndege nyingi ndogo na viwanja vingi havikidhi vigezo ndio sababu unaona zinaruka saa kumi na mbili asubuhi
 
Wote mna hoja nzuri..na wote mko sahihi..enhe kwahiyo tumekubalianaje sasa?
 
Sisi bado tupo kwenye karne ile ya primitive communalism na tunalazimisha kuwepo kwenye the world of high technology.

Kumbuka kuwa bado hatujawa na sheria ya kuruhusu kufanyika kwa baadhi ya Kazi 24hrs.

Mfano TRA, BANDARI,VIWANJA VYETU VYA NDEGE KUKOSA MIUNDO MBINU YA KUPOKEA NDEGE ZINAZOSAFIRI USIKU,LABDA VIWANJA VICHACHE TU.

Bado tuna zile Imani za zamani kuwa muda wa usiku ni muda wa uzazi na sio wa serikali au kufanya Kazi.
Nini kifanyike.

Viongozi wetu wakisafiri wawe wanaenda na wataalam ili kuiba idea na knowledge ili itusaidie.
Mfano. Suala la usafiri wa kwenda morogoro na baadhi ya mikoa ambayo ni Salama, iwe 24 hrs ilimradi ruti ndefu ziwe na madreva wawili.

Tuweke taa katika viwanja vyetu vya ndege,kuviboresha kuendana na international standards hasa hasa kuwe walau na sehemu mbili za kuruka ndege mbili kwa wakati mmoja,kutua napo iwe hivyo hivyo na sehemu za kupaki ndege na matengenezo, magari hata walau kuanzia 4 makubwa ya kuzima moto.

Kuruhusu ndege kutua usiku na mashirika ya ndege yaweze ku-encourage safari za usiku japokuwa najua usafiri wa ndege usiku bei yake ni ndogo kulinganisha na usafiri wa mchana.

Bara bara zetu kiukweli zina tatizo Sana,hakuna taa,msururu wa magari ya mizigo na yanatembea taratibu Sana,yanapaki bara barani mara kwa mara na pia mengine kuharibika bara barani,pia ni kama one way.

Ushauri

Tuanzie pale ambapo mwendazake ameishia,tuige idea yake tu, japokuwa kuna SGR, bado morogoro road itengenezwe hadi moro kwa njia zile zile nane,itasaidia sana maana kila weekend, kunakuwa na msururu wa magari mengi kwenda mikoani,huku magari makubwa nayo mara yaanguke,mara ajali,mara limeharibika,basi hapo kukaa bara barani kwa zaidi ya saa nne na kuendelea ni kawaida Sana. Tunakosa mapato kwa njia hyo.

Pia bara bara zetu walau serikali ianzie kuachana na kutengeneza bara bara za njia mbili, iwe ni sheria kuwa na njia sita kwenda mbele.

Mwisho ni kuwa bank, ATM,mpesa na tigo pesa ziwe nazo 24 hrs katika maeneo Kama hayo ya magari kama hapo mbezi itakuwa ni vizuri zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…