Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

Mkuu Kwa wale hatujui nyama ya tandala tuwekee japo picha😂😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣
 
Yaani wanyama wanapigwa risasi na watalii na kuacha mizoga ila masikini akibeba anahukumiwa jela why?

Yaani kama hakima anaweza kumfunga mtuhumiwa kwa kukutwa na nyama pori basi hana huruma kabisa huyo

Kuna majizi yameiba hela zetu na yameporomosha majengo ila bado wanapigiwa salute 🫡 kutwa
 
Sijajua tandala ndo mnyama gani, lakini hukumu ni ya hivyo sana.

Mnyama akiua binadamu fidia milioni moja.

Binadamu akiua mnyama fidia milioni 20.

Tuendelee kuwaheshimu wanyama. [emoji23]
 
Kumbe ilikuwa figisu? Mbona Polisi walitangaza kuwa ana milki siraha na nyara kinyume cha Sheria
 
Kweli mkuu kama yule Mchina juzikati hapo alipigwa Fine ya Laki mbili tu. Huu ni uonevu.
Zipo kesi nyingi tu,tena wanakutwa na maliasili za kutosha.....tukisema RUSHWA ipo mahakamani Kwa hili hawawezi kukataa
 
Siwezi kushangaa sababu kuna uwezekano aliyetoa hukumu hajawahi kuingia hata selo ya polisi

Lakini kama watoaji hukumu wangekuwa wameshaingia jela au walau selo jpo kwa week hakika hizi hukumu za miaka 20+ kwa kesi kama hii zisingekuwepogo

Maana jela kunatisha sidhani kama kuna mtu anaeujua msoto wa jela akawa anatamani mwenzake akamalizie maisha kule
 
So what if caught? But others get caught and released
Hapo ndiyo mnapofeli,eti umekamatwa na Jinai, utetezi wako ni eti mbona kuna wengine wanafanya Jinai lakini hawa kamatwi,na hata wakikamatwa wanaweza achiwa police au Mahakamani,utafungwa mapema sana! Wwe jiteteee wwe Kama wwe na Jinai yako!! Jinai maana yake halisi ni kua Umekinzana na Sheria!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…