Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

Huyo aliyeuza nyama ya porini,bila kibali,ndio umtetee,ukisikia kibali,ni pamoja na nyama kupimwa na daktari wa wanyama,kua alikufa kibudu,na alikufa na maradhi gani,na pia kama kachinjwa,je hakuwa na maradhi ya kuambukiza binadamu?
Wewe unamtetea muuaji,je kama nyama ina maradhi,na yakaambukiza binadamu,wewe na wenzako wengine,utalaumu serekali,kwa kutoweka sheria ya vibali,baada ya kukaguliwa nyama kabla ya kuuuzwa na kufanywa kitoeo.
Kwani mangapi mbali na hilo la nyama, yanaonesha u double standards wa sheria zetu? Vyakula hivi vyote vya mitaani vinapimwa? Samaki wa baharini je? Wote wanapimwa?
 
Sheria gani zinawahusu masikini peke yao!! Vigogo wa CCM ndiyo wanaongoza kwa ujangili nchini, lakini huwezi kusikia wamehukumiwa vifungo jela, hata pale wanapokamatwa na vielelezo!
Hao wanakuwa na kibali.Ukisikia kibali ni nyama ipimwe na daktari wa wanyama,kama iko salama kwa mlaji.Wewe wafikiri,kunasomeshwa madaktari wa wanyama kwa kazi gani?Mojawapo katika kazi zao,ni kupima mnyama,kama hana maradhi ya kuambukiza kwa binadamu,kabla ya kufanywa kitoeo.Huyo aliyeuza nyama bila kibali,anataka kuambukiza watu maradhi,kutoka kwa wanyama.
 
Wewe kama ni Mpemba hakuna ulijuwalo kuhusu nyama pori.

Wenye Leseni za mabucha ya wanyama pori ni wachache sana Tanzania nzima, ila wawindaji wanatumia vibali halali ni wengi.

Binafsi huwezi kunifunga kwa kesi ya kipuuzi kama hiyo, nyama nimenunuwa kwa wawindaji ambao wamewinda kihalali na huu ni msomi wa uwindaji.

Nyama pori tunauziana mtaani kwa ajili ya kitoweo sawa na muuza utumbo au muuza mchicha hakuna kwenye Leseni ya kufanya hizo biashara.

Isitoshe siwezi kukaa kijiji Jirani na game reserve halafu nisile nyama pori wakati hivyo vitoweo katupa Mungu mwenyewe.

Ni sawa na watu wa pwani au ziwani uwaambie kuvuwa Samaki wavuwe kwa kibali ni upuuzi mtupu.
Kumbe wewe hujui,unafikiri wavuvi wanavua bila leseni.Wapo pia samaki wana sumu baharini,lakini wenyeji wanawajua,huwa wanatayarisha kwa uangalifu,wakikosea tu,wanakula sumu.
Wewe utakuwa unaishi maeneo yasiokuwa na wanyama pori,hata ng'ombe,ukitaka kuuza mpaka apimwe.
 
Kwani mangapi mbali na hilo la nyama, yanaonesha u double standards wa sheria zetu? Vyakula hivi vyote vya mitaani vinapimwa? Samaki wa baharini je? Wote wanapimwa?
Tumia akili.Nyama zikiuzwa holela,na kusmbukiza maradhi binadamu,wewe na wenzako,ndio mtakuwa wa kwanza kulaumu serekali.Nyama lazima ipimwe,mnyama kafa ana maradhi ya kuambukiza,au siyo.
 
Mwana kulitafuta mwana kulipata
E2ELd3pWEAAaxin.jpg
 
Tumia akili.Nyama zikiuzwa holela,na kusmbukiza maradhi binadamu,wewe na wenzako,ndio mtakuwa wa kwanza kulaumu serekali.Nyama lazima ipimwe,mnyama kafa ana maradhi ya kuambukiza,au siyo.
Sawa, suala si ni maradhi? Kwani samaki wanaovuliwa kila siku hawawezi kuwa contaminated na bacteria wa magonjwa mlipuko kwa binadamu? Mara ngapi watu wanakufa kwa kula samaki wenye sumu? Why ni kwa wanyama pekee?

Lini umesikia watu wakifa kwa kuambukizwa ugonjwa kwa kula nyamapori? Unaona namna usivyoishughulisha akili yako?
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.

Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya Tandala – Kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya Tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya Tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ahmad Magenda, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

"Niombe mahakama yako itoe adhabu kali kwa washtakiwa wote ambao wanafanya makosa kama haya ya kuhujumu wanyapori ambao ni vivutio kwa watalii, sanjari na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Magenda.

MWANANCHI
Jaji ni mpuuzi,sheria zilizopotwa na wakati zifutwe hata kama anashitakiwa kwa.kukutwa na nyara za serikali
 
Kumbe wewe hujui,unafikiri wavuvi wanavua bila leseni.Wapo pia samaki wana sumu baharini,lakini wenyeji wanawajua,huwa wanatayarisha kwa uangalifu,wakikosea tu,wanakula sumu.
Wewe utakuwa unaishi maeneo yasiokuwa na wanyama pori,hata ng'ombe,ukitaka kuuza mpaka apimwe.
Kwani pweza ana sumu gani? Wote tunajua hana sumu ya kuua, so why watu walikufa kwa kula pweza? Unaweza kujibu hili?
 
Hao wanakuwa na kibali.Ukisikia kibali ni nyama ipimwe na daktari wa wanyama,kama iko salama kwa mlaji.Wewe wafikiri,kunasomeshwa madaktari wa wanyama kwa kazi gani?Mojawapo katika kazi zao,ni kupima mnyama,kama hana maradhi ya kuambukiza kwa binadamu,kabla ya kufanywa kitoeo.Huyo aliyeuza nyama bila kibali,anataka kuambukiza watu maradhi,kutoka kwa wanyama.
Sasa kwani samaki wanaovuliwa pale Feri hawawezi kuwa na maradhi yanayoweza hata kuua binadamu? Why na huko wauzaji wasipime samaki wanaowauza kisheria?
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.

Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya Tandala – Kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya Tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya Tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ahmad Magenda, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

"Niombe mahakama yako itoe adhabu kali kwa washtakiwa wote ambao wanafanya makosa kama haya ya kuhujumu wanyapori ambao ni vivutio kwa watalii, sanjari na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Magenda.

MWANANCHI
Mbona bandari hawagungwi?
 
Anaewinda apate kitoweo anasekwa jela 20 years. Wauza bandari na mbuga zetu wanakenua tu wakiendelea kula na kodi zetu huku wakitembelea V8 na kujenga partments huku pia wakiendelea kusinzia na kujambiana bungeni wakipulizwa na AC kwa jasho la walalahoi.

Shenzistan, nchi ya ajabu sana hii.
Ndio maana N
 
Mdogo wake rostam mnakumbuka ile kesi yake ya nyara za taifa mwaka 2019?
 
Back
Top Bottom