Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

Ni kuwapa Mzigo wananchi kulisha bure watu Magerezani

Hizi sheria reforming watu watolewe huko Magerezani ....mambo ya Kikoloni yaliyopitwa na wakati

Busara zitumike TAWA TANAPA TFS nk
Haki haiombwi mkuu. Umeongea kijyonge na kirahisi mno, ilhali mtu ameshakula mvua 20 tayari. Tutaendelea kuongea mpaka lini? Lini tutafanya vitendo?
 
Hii serikali ina sheria za kipuuzi sana. Wageni kutoka nje mfano Waarabu, na watawala ndiyo wanajiona wana haki ya kula wanyama wa porini.

Ila sisi wanyonge tukijaribu tu kuua hao wanyama kwa ajili ya kitoweo, tunaishia kufungwa vifungo virefu magerezani. Huu ni upumbavu.
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.

Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya Tandala – Kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya Tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya Tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ahmad Magenda, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

"Niombe mahakama yako itoe adhabu kali kwa washtakiwa wote ambao wanafanya makosa kama haya ya kuhujumu wanyapori ambao ni vivutio kwa watalii, sanjari na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Magenda.

MWANANCHI
Kutakua kuna lingine nyuma ya pazia
 
Picha ya tandala tafadhali, aliyemfungisha mtu miaka 20.
Jike:
1693910065534.png


Dume:

1693910113289.png
 
Hii serikali ina sheria za kipuuzi sana. Wageni kutoka nje mfano Waarabu, na watawala ndiyo wanajiona wana haki ya kula wanyama wa porini.

Ila sisi wanyonge tukijaribu tu kuua hao wanyama kwa ajili ya kitoweo, tunaishia kufungwa vifungo virefu magerezani. Huu ni upumbavu.
Soma habari vizuri,huyu hakuwa na kibali,hao wengine unaowataja itakuwa wana vibali,huyu angekuwa amekata kibali yasingemfika haya.Mnatakiwa muwafahamishe wananchi,kuwa ukifanya biashara ya wanyama pori uwe na kibali,na ukakate kibali na leseni, mahali fulani,ni sawa na dereva aendeshe gari bila leseni,au mfanyabiashara asiwe na leseni,au ufanyekazi ya udaktari bila leseni,uwe na duka la dawa bila leseni,wategemea nini,kama sio kuvunja sheria.
 
Back
Top Bottom