Mufti Mkuu wa Omani afika kumuona Rais Samia Hassan katika Kasri ya Al Alam

Mufti Mkuu wa Omani afika kumuona Rais Samia Hassan katika Kasri ya Al Alam

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
14 June 2022
Muscat, Oman

By: ONA
1655210285911.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ampokea Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alipofika katika makazi ya wageni mashuhuri (VIP) Kasri ya Al Alam kuonana na rais Samia Suluhu Hassan .

Mazungumzo ya Mh. Rais Samia Hassan na Mufti Mkuu wa Oman yaligusia masuala mbalimbali yanayogusa jamiii.

Katika mazungumzo hayo rais aliongozana na Dr. Pindi Chana, waziri wa Utalii , Dr. Khalid Salum Mohamed, waziri wa SMZ Ujenzi, usafiri na mawasiliano, balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, naibu waziri mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki .

Tanzanian President receives Oman's Grand Mufti Tuesday 14/June/2022​

Muscat: President Samia Suluhu Hassan of the United Republic of Tanzania received at her residence place in Al Alam Palace here today His Eminence Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili, the Grand Mufti of the Sultanate of Oman.

The Tanzanian President and the Grand Mufti of Oman exchanged cordial talks and reviewed matters of common interest.

The meeting was attended by Saud Hilal Al Shidhani, Ambassador of the Sultanate of Oman to the United Republic of Tanzania. It was also attended from the Tanzanian side by Dr. Pindi Chana, Minister of Natural Resources and Tourism, Dr. Khalid Salum Mohamed, Minister of Works, Transport and Communications and Ambassador Mbarouk Nassoro Mbarouk, Deputy Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation
 
14 June 2022
Muscat, Oman

Rais Samia Suluhu Hassan akutana na viongozi wanawake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipata wasaa wa kukutana na viongozi wakuu na watendaji wanawake waliopo katika sekta ya umma na ile ya binafsi waliofika katika Kasri ya Al Alam kuonana naye.

1655210796512.png

Mazungumzo hayo baina ya mheshimiwa rais Samia Hassan na viongozi hao wanawake yalilenga katika kubadilishana uzoefu na pia nafasi ya wanawake katika kuchangia maendeleo. Viongozi hao waliofika kufanya naye mazungumzo ni, wanawake wa kutoka Oman na Tanzania


Tanzanian President meets Omani, Tanzanian female presidents and CEOs

The Tanzanian President met a number of Omani and Tanzanian female presidents and CEOs in the public and private sectors.

"Her Excellency Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, met a number of female presidents and CEOs in the public and private sectors in the Sultanate of Oman and Tanzania, at Al Alam Palace, to discuss the importance of strengthening cooperation relations in various fields and the role of women in development and increasing trade and investment exchange," Oman News Agency (ONA) said in a statement.
 
Shughuli nyingine aliyofanya mheshimiwa rais Samia Hassan ni kutembelea jumba la Royal Opera House

1655212759112.png

Mheshimiwa Rais Samia Hassan alipofika katika ukumbi / jumba la Royal Opera House, Muscat Oman


Majumba haya ni muhimu kwa ajili ya shughuli za maonesho, sanaa ya uigizaji jukwaani na pia kudumisha tamaduni , simulizi kwa kufanya maigizo zilizochota maudhui toka katika riwaya, uvumbuzi, Sayansi, hadithi na historia.


https://rohmuscat.org.om/en/Pages/default.aspx
 
Haya maisha yana usiri mkubwa juu ya yatakayokutokea mbele hujui huoni wala husikii kuwa mbeleni utakuwaje au nini kitakutokea.
 
Majumba haya ni muhimu kwa ajili ya shughuli za maonesho, sanaa ya uigizaji jukwaani na pia kudumisha tamaduni , simulizi kwa kufanya maigizo zilizochota maudhui toka katika riwaya, uvumbuzi, Sayansi, hadithi na historia.

Opera Musical House zingekuwepo Tanzania na Zanzibar zingetumika kuonesha umahiri na pia kuwa vituo vya kujifunza na kuibua vipaji. Tunayo ile Little Theatre pale St. Peter's Oysterbay Dar es Salaam lakini tunahitaji kumbi kadhaa kubwa za kisasa

Dar Choral society and orchestra
 
14 June 2022
Muscat, Oman

Mheshimiwa Rais Samia Hassan akiwa ndani ya ukumbi / jumba la Royal Opera House, Muscat Oman

 
14 June 2022
By: ONA
View attachment 2260529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ampokea Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alipofika katika makazi ya wageni mashuhuri (VIP) Kasri ya Al Alam kuonana na rais Samia Suluhu Hassan...
Ziara hii ya mh. Raisi wetu itakuwa fundisho kubwa kwa mtizamo hasi kwa waarabu na wataliban kuhusu mwanamke.

Nadhani sasa wataelewa kuwa mwanamke anawesa kushika nafasi za juu kabisa za uongozi na maamuzi na nchi ikaenda kwa amani, umoja furaha na maendeleo

Wataacha sasa kufikiri kuwa mwanamke hapaswi kusoma shule tofauti na za dini, na mwanamke sii chombo cha kukaa ndani , kuamuliwa nini cha kufanya na wanaume, kuwa mwanamke ni binaadamu kama binaadamu mwingine mwenye utashi na anayeitaji dialogue za hoja sio mabavu
 
Mbona huo msafara kama wazanzibar ni wengi?
wafanya.png

Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania wakimsikiliza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Wapo wengi tu kutoka bara kuanzia maofisa wa wizara ya nishati, shirika la TPDC, TCCI Tanzania Chambers Commerce and Industries listi ni ndefu, sema vyombo vya media Tanzania hawajafuatilia sana mambo

2-1-1-scaled.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Waziri wa Nishati January Makamba wakati akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye masuala ya Nishati (Oil and Gas) kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman kupitia Wizara ya Nishati na Madini (Sekta ya Madini) ya nchi hiyo katika hafla iliyofanyika Al Bustan, Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.
 
21-1-scaled.jpg


Mkataba wa Makubaliano katika ya Jumuiya ya Watoa huduma katika Sekta ya mafuta na Gesi (AGAS) na Jumuiya ya watoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi Zanzibar ZAOGAS pamoja na Jumuiya ya watoa huduma za Mafuta kutoka Oman (OPAL) katika hafla iliyofanyika Muscat Oman Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara ya Zanzibar Ali Amour katikati ni Mwenyekiti wa ATOG Balozi Abdulsamad Abdulrahim na kwa upande wa Oman ni Mkurugenzi Mtendaji wa OPAL Abdulrahman Al Yahya
 
Japo tunauzwa Ila daaah mi niwe positive tuuu , waturuhusu tuoe huko 😊
 
Back
Top Bottom