Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Sio hatar kuna watu wanacancer ya uzazi hawez kumpa mimba mwanamke au maradhi kama hiv kuogopa kuambukizana unaenda pandikiza zinachukuliwa mbegu zako halafu zinaingizwa kwa mwanamke
BEI ZAKE TISHIO
 
... mimba halali ni ile inayotungwa kwa manii kuingia tumbo la uzazi baada ya uume kupenya ukeni; hiyo ndio njia pekee aliyoumba Mola wetu kuendeleza kizazi na sio vinginevyo.
Hata hiyo ni sehemu ya kuendeleza kizazi kwa wanandoa wenye shida kutunga mimba kwa njia ya asali,manii na yai la mama vinarutubishwa nje ya mfumo wa uzazi halafu vinarejeshwa kwenye mfuko wa mama na mimba inakuwa kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi wale ambao hawajabahatika kuolewa au kuoa na wenye upungufu wa nguvu za kiume Basi nafikili hii itawasaidia.
Ivf haina uhusiano na kuolewa au upungufu wa nguvu za kiume.
Maana wengi wanaofanya ivf ni wanandoa na tena wapo vizuri kifedha,single wenye pesa zao maana gharama zake siyo chini ya 10m ya kibongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vizuri sana ila waangalie na garama ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu (wanyonge kwa mujibu wa JPM), nina ndugu yangu alipandikizwa Nairobi yaani vipimo na upandikizwaji tu iligarimu karibia 40, milioni... na alibahatika kupata mapacha baada ya kukaa kwenye ndoa mika 21 bila mtoto. Mungu akampa wa kike na kiume kupitia IVF..ila pesa ni ndefu sana.
Hata dar kuna private hospital wanafanya mpaka unampatia mtoto siyo chini ya 20m za Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nchini Tanzania itaanza kutoa huduma ya kupandikiza mimba kuanzia Januari mwaka 2020.​

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya MNH tangu Rais John Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi.

“Tumeshapeleka wataalamu nchini India kuangalia namna ambavyo huduma ya upandikizaji mimba (IVF) inavyotolewa katika hospitali za umma, ni miundombinu na vifaa gani vinahitajika,” amesema Profesa Museru.

Amesema kwa sasa mainjinia wameanza kukarabati jengo katika hospitali hiyo litakaloanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kabla ya jipya litakalojengwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila.

“Ununuzi wa vifaa unafanyika na mipango imeanza, tayari wataalamu wameshatayarishwa, tunatarajia katika miezi miwili ijayo tutaanza rasmi kufanya upandikizaji,” amesema Profesa Museru.

Amesema huduma hiyo itakuwa ya kulipia, “tutataka watu wailipie hatujajua itagharimu kiasi gani, hiyo ni mpaka wataalamu watakapofanya maamuzi lakini asiyeweza kulipia pia tutaingia kwenye mfumo wa huduma za namna hiyo.”

Amesema katika kituo hicho zitatolewa huduma za kupandikiza figo, vifaa vya kusaidia kusikia, kupandikiza mimba, ini, uloto na maabara ya kujifunzia ujuzi.

Hatua nzuri japo tumechelewa mno kuanza..kuhusu kupandikiza mimba ni jambo jema...ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutoka na shida ya watoto...sasa nadhani huduma hii ikija itarudisha furaha majumbani....

Kuhusu kupandikiza viungo nalo ni jema ila maandalizi ya sera na sheria lazima yafanyiwe kazi...maanake tutaanza kuibia figo...human organs trafficking...hapo lazima tujipange tena sana...
 
Kwa ukanjanja wangu kupandikiza mimba process yake ni very complex. Mimba inaweza kutungishwa kwa mwanamke mwingine na kupachikwa kwa mwanamke asiyeshika mimba. Au mwanauke asiye na uwezo au nguvu za kuzaa mbegu zake huchukuliwa na kupachikwa kwa mwanamke. Wataalamu humu toeni darasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ukanjanja wangu kupandikiza mimba process yake ni very complex. Mimba inaweza kutungishwa kwa mwanamke mwingine na kupachikwa kwa mwanamke asiyeshika mimba. Au mwanauke asiye na uwezo au nguvu za kuzaa mbegu zake huchukuliwa na kupachikwa kwa mwanamke. Wataalamu humu toeni darasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sorry mwanaume asiye na uwezo wa kutungisha mimba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom