Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Wanapoteza muda na hela bure.

Ajiri madume ya mbegu yasiyojulikana yakae pale iwe kazi kuwamwagia tu, ukimwagiwa unakwenda anaingia mwingine naye anamwagiwa kuna watu wanamatank ya mbegu.
unawaza tofauti na maana hiyo wanalionayo muhimbili jaribu kuchimba kdg utaelewa
 
Mkiambiwa muende na wake zenu clinic pind wanapokuwa wajawazito mnaingia mitini.
 
... mimba halali ni ile inayotungwa kwa manii kuingia tumbo la uzazi baada ya uume kupenya ukeni; hiyo ndio njia pekee aliyoumba Mola wetu kuendeleza kizazi na sio vinginevyo.
Shukuru Mungu hujapata changamoto ya uzazi
 
Safi sana wale wanawake waliokua wanaringia vizazi hapa mjini mtaheshimiana sasa wema fursa hii mdogo wangu neno la ugumba kwako mwisho sasa
 
Kumbe wee hujaelewa tunachokizungumzia... Sio inshu ya kwenda kupandikiza nasemea utayari wa mwanaume. Mwanamke anaweza kupandikaza kwa ajili ya malengo yake ya ndoa
Naona hata wewe huelewi? Mtu kama anataka kukupa mtoto kwa nini apoteze hela kwenda kupandikiza wakati anaweza kuipata hapohapo kwako?
 
Naona hata wewe huelewi? Mtu kama anataka kukupa mtoto kwa nini apoteze hela kwenda kupandikiza wakati anaweza kuipata hapohapo kwako?
Sasa kila nikikutana nae navaa mpira.
rejea post yangu ya kwanza "mipira lazima itatumika sana" lazima atumie mbinu mbadala kuipata mimba kutoka kwangu
 
Sasa kila nikikutana nae navaa mpira.
rejea post yangu ya kwanza "mipira lazima itatumika sana" lazima atumie mbinu mbadala kuipata mimba kutoka kwangu
We nae huelewi hata unachokisimamia, kama unatumia mpira mwanamke anakuleteaje mimba? Atakuambia imeingilia wapi? Na huyo mwenzio unayemuunga mkono hoja yake amesema itumike mipira ili watu wasibambikwe. Kifupi hueleweki yaani.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nchini Tanzania itaanza kutoa huduma ya kupandikiza mimba kuanzia Januari mwaka 2020.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya MNH tangu Rais John Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi.

“Tumeshapeleka wataalamu nchini India kuangalia namna ambavyo huduma ya upandikizaji mimba (IVF) inavyotolewa katika hospitali za umma, ni miundombinu na vifaa gani vinahitajika,” amesema Profesa Museru.

Amesema kwa sasa mainjinia wameanza kukarabati jengo katika hospitali hiyo litakaloanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kabla ya jipya litakalojengwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila.

“Ununuzi wa vifaa unafanyika na mipango imeanza, tayari wataalamu wameshatayarishwa, tunatarajia katika miezi miwili ijayo tutaanza rasmi kufanya upandikizaji,” amesema Profesa Museru.

Amesema huduma hiyo itakuwa ya kulipia, “tutataka watu wailipie hatujajua itagharimu kiasi gani, hiyo ni mpaka wataalamu watakapofanya maamuzi lakini asiyeweza kulipia pia tutaingia kwenye mfumo wa huduma za namna hiyo.”

Amesema katika kituo hicho zitatolewa huduma za kupandikiza figo, vifaa vya kusaidia kusikia, kupandikiza mimba, ini, uloto na maabara ya kujifunzia ujuzi.
 
mke wa obama hajawai beba mimba ko nae alitumia IVF tunakoelekea mabinti zetu wataingiwa na pepo la kutobeba mimba ili kuwavutia wanaume
 
Labda Da' Wema Sepetu, Lady Jei Dii wanaweza kupata faraja
 
Uboreshaji wa mbegu za kiume?
Ni Jambo jema kwa wale wenye matatizo ya kutungisha mimba kiasili pia faida Ni nyingi hasa katika kuchagua mbegu (mapacha,jinsia nk), na uboreshaji wa mbegu za kiume.

Wasisahau haya mambo yanaenda mabadiliko ya Sheria hasa uraia, kuasili watoto na mirathi.
 
mke wa obama hajawai beba mimba ko nae alitumia IVF tunakoelekea mabinti zetu wataingiwa na pepo la kutobeba mimba ili kuwavutia wanaume
Kwani hiyo ivf mimba inabebwa kwenye chupa mpaka mtoto anafikisha siku zake au
Maana sijakuelewa
 
Kwani hiyo ivf mimba inabebwa kwenye chupa mpaka mtoto anafikisha siku zake au
Maana sijakuelewa
Hii ni kali ivf ni njia ya kuaandaa mimba lkn mimba anabeba mwanamke uyo sijui anaelewaje iyo mambo ya IVF
 
Habarini wakuu je muhimbili washaanza kupandikiza? Mwenye kujua tunaomba atujuvye.. Walisema mwezi wa januar rasmi wanaanza.. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom