mama chupaki
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 940
- 765
Kivipi iwe kinyume?Ni sehemu ya matibabu kama vile kupandikiza figo.Mbona hii ni kinyume na maagizo ya Allah (SAW)
BEI ZAKE TISHIOSio hatar kuna watu wanacancer ya uzazi hawez kumpa mimba mwanamke au maradhi kama hiv kuogopa kuambukizana unaenda pandikiza zinachukuliwa mbegu zako halafu zinaingizwa kwa mwanamke
Hata hiyo ni sehemu ya kuendeleza kizazi kwa wanandoa wenye shida kutunga mimba kwa njia ya asali,manii na yai la mama vinarutubishwa nje ya mfumo wa uzazi halafu vinarejeshwa kwenye mfuko wa mama na mimba inakuwa kama kawaida.... mimba halali ni ile inayotungwa kwa manii kuingia tumbo la uzazi baada ya uume kupenya ukeni; hiyo ndio njia pekee aliyoumba Mola wetu kuendeleza kizazi na sio vinginevyo.
Ivf haina uhusiano na kuolewa au upungufu wa nguvu za kiume.Basi wale ambao hawajabahatika kuolewa au kuoa na wenye upungufu wa nguvu za kiume Basi nafikili hii itawasaidia.
Habarini wakuu je muhimbili washaanza kupandikiza? Mwenye kujua tunaomba atujuvye.. Walisema mwezi wa januar rasmi wanaanza.. Asante
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ndugu ni mwendo wa punyeto then manii unaweka ktk test tube maalum baada ya hapo procedure ingine inaendelea.Mpandikiza mimba anapata utamu kweli!?
Ni kweli kabisa ngoja ije tu hiyo huduma tusikie kilio.Ni watu wachache sana wataweza gharamia ili kupata hiyo huduma.
Naona wadada wanashangilia wanadhani unaenda na elfu 10 yenye tembo unapanua unawekewa mbegu...
Its a long process, nitaelezea nikipata muda..
Hata dar kuna private hospital wanafanya mpaka unampatia mtoto siyo chini ya 20m za Tanzania.Ni vizuri sana ila waangalie na garama ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu (wanyonge kwa mujibu wa JPM), nina ndugu yangu alipandikizwa Nairobi yaani vipimo na upandikizwaji tu iligarimu karibia 40, milioni... na alibahatika kupata mapacha baada ya kukaa kwenye ndoa mika 21 bila mtoto. Mungu akampa wa kike na kiume kupitia IVF..ila pesa ni ndefu sana.
Tofautisha Ivf(upandikizaji) na sperm doner.Na sperm zipo tasa pia.Hii ajira itakuwa nzuri
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nchini Tanzania itaanza kutoa huduma ya kupandikiza mimba kuanzia Januari mwaka 2020.
Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya MNH tangu Rais John Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi.
“Tumeshapeleka wataalamu nchini India kuangalia namna ambavyo huduma ya upandikizaji mimba (IVF) inavyotolewa katika hospitali za umma, ni miundombinu na vifaa gani vinahitajika,” amesema Profesa Museru.
Amesema kwa sasa mainjinia wameanza kukarabati jengo katika hospitali hiyo litakaloanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kabla ya jipya litakalojengwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila.
“Ununuzi wa vifaa unafanyika na mipango imeanza, tayari wataalamu wameshatayarishwa, tunatarajia katika miezi miwili ijayo tutaanza rasmi kufanya upandikizaji,” amesema Profesa Museru.
Amesema huduma hiyo itakuwa ya kulipia, “tutataka watu wailipie hatujajua itagharimu kiasi gani, hiyo ni mpaka wataalamu watakapofanya maamuzi lakini asiyeweza kulipia pia tutaingia kwenye mfumo wa huduma za namna hiyo.”
Amesema katika kituo hicho zitatolewa huduma za kupandikiza figo, vifaa vya kusaidia kusikia, kupandikiza mimba, ini, uloto na maabara ya kujifunzia ujuzi.
Sorry mwanaume asiye na uwezo wa kutungisha mimbaKwa ukanjanja wangu kupandikiza mimba process yake ni very complex. Mimba inaweza kutungishwa kwa mwanamke mwingine na kupachikwa kwa mwanamke asiyeshika mimba. Au mwanauke asiye na uwezo au nguvu za kuzaa mbegu zake huchukuliwa na kupachikwa kwa mwanamke. Wataalamu humu toeni darasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo ilikuwa n siasa tuuu.Muhimbili wenyewe nazani bado hawajaanza sijui kwanini na walisema wangeanza tangu mwaka jana
Sent using Jamii Forums mobile app