Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Muhimbili kuanza kupandikiza mimba mwaka 2020

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nchini Tanzania itaanza kutoa huduma ya kupandikiza mimba kuanzia Januari mwaka 2020.​

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya MNH tangu Rais John Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi.

“Tumeshapeleka wataalamu nchini India kuangalia namna ambavyo huduma ya upandikizaji mimba (IVF) inavyotolewa katika hospitali za umma, ni miundombinu na vifaa gani vinahitajika,” amesema Profesa Museru.

Amesema kwa sasa mainjinia wameanza kukarabati jengo katika hospitali hiyo litakaloanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kabla ya jipya litakalojengwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila.

“Ununuzi wa vifaa unafanyika na mipango imeanza, tayari wataalamu wameshatayarishwa, tunatarajia katika miezi miwili ijayo tutaanza rasmi kufanya upandikizaji,” amesema Profesa Museru.

Amesema huduma hiyo itakuwa ya kulipia, “tutataka watu wailipie hatujajua itagharimu kiasi gani, hiyo ni mpaka wataalamu watakapofanya maamuzi lakini asiyeweza kulipia pia tutaingia kwenye mfumo wa huduma za namna hiyo.”

Amesema katika kituo hicho zitatolewa huduma za kupandikiza figo, vifaa vya kusaidia kusikia, kupandikiza mimba, ini, uloto na maabara ya kujifunzia ujuzi.
Dah hiyo nifursa kwa bashite maana alikuwa anasumbuka kwenda China.. Najua anafurahia saana
 
Umesema 'naona wadada wanashangilia wanadhani unaenda na elfu kumi' dharau kubwa sana hii ututake radhi
Haaaaaahaaaaa sio dharau mdau anawaelekeza sio mnafurahia tu ile huduma sio 12,000 gharama yake!
 
Sijui biblia inasemaje kuhusu hiyo kitu ila kama si dhambi itabidi niende nikapandikize[emoji125][emoji125]
Kwa wanandoa haina shida, ni msaada mzuri kwa wanandoa ambao hawawezi kupata mtoto kwa njia ya kawaida,ila kwa masingle mpite tu kuna moto mkubwa huko mbinguni utakuwa unakusubiri hahahahaa!!!

Mambo vipi mdogo wangu? Nakusalimu katika jina la Bwana .......
 
Zen inaelekea wewe unapenda wenzako wasipate watoto.

Kupenda kwangu au kinyume chake haibadili kitu, bali mapenzi ya Mungu aliye juu muweza wa yote.... kwa kukusaidia tu success rate sio 100% na bado gharama zake sio kwa Watanzania wanyonge.
 
Kupenda kwangu au kinyume chake haibadili kitu, bali mapenzi ya Mungu aliye juu muweza wa yote.... kwa kukusaidia tu success rate sio 100% na bado gharama zake sio kwa Watanzania wanyonge.
Sawa ila mungu atupe pumzi mpaka 2030....tutaangalia gharama zitabaki kuwa juu au VP????
 
Ni vizuri sana ila waangalie na garama ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu (wanyonge kwa mujibu wa JPM), nina ndugu yangu alipandikizwa Nairobi yaani vipimo na upandikizwaji tu iligarimu karibia 40, milioni... na alibahatika kupata mapacha baada ya kukaa kwenye ndoa mika 21 bila mtoto. Mungu akampa wa kike na kiume kupitia IVF..ila pesa ni ndefu sana.
Mbona mikocheni pale m 10 tu.tulipata dogo hapo mwaka juzi
 
Kwa hiyo wanaoshika mimba na kujifungua kawaida success rate n 100%....ngoja nikupe mifano iliyo hai wiki iliyopita kuna shemeji yangu kajifungua kawaida mtoto kaish siku moja tumemzika,,,nyingine kunajirani yangu wakati wakujifungua mama na mtoto ikawa bahati mbaya wote tukawazika.
Kupenda kwangu au kinyume chake haibadili kitu, bali mapenzi ya Mungu aliye juu muweza wa yote.... kwa kukusaidia tu success rate sio 100% na bado gharama zake sio kwa Watanzania wanyonge.
 
Kwa hiyo wanaoshika mimba na kujifungua kawaida success rate n 100%....ngoja nikupe mifano iliyo hai wiki iliyopita kuna shemeji yangu kajifungua kawaida mtoto kaish siku moja tumemzika,,,nyingine kunajirani yangu wakati wakujifungua mama na mtoto ikawa bahati mbaya wote tukawazika.

Duuh..!!

We jamaa umekomaa na mifano bila kujali kuwa unahamisha magoli, nachelea kusema kuwa umehama kwenye hoja ya msingi.... mada inaongelea IVF sio Mortality Rate za mama na watoto.

Well, success rate hata kutia mimba kwa njia ya asili sio 100%.... ila kwani hapo unakuwa umetumia pesa kiasi gani kufanikisha lengo hilo..?

Poleni kwa msiba, kazi yake Mola haina makosa.... RIP them kids.
 
Asanteee

Sasa mtoto akifanya makosa shule akaambiwa kamlete mzazi wako wa kiume itakuwaje
 
Back
Top Bottom