Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Hivi kwa nini tusipende vya kwetu? Shida ni nini iwapo na sisi watalam wetu wameona njia bora mojawapo kua ni hiyo? Kwani na sisi hadi tuige kwa kwingine? Naunga mkono msimamo wa Nchi yangu
 
hahaaaaaaaaaaaa this is funny,watu na taaluma zao kabisaa...
Hosipitali
IMG_20210304_173554.jpg
 
Hivi kwa nini tusipende vya kwetu? Shida ni nini iwapo na sisi watalam wetu wameona njia bora mojawapo kua ni hiyo? Kwani na sisi hadi tuige kwa kwingine? Naunga mkono msimamo wa Nchi yangu
Kupiga nyungu ilijaribiwa lini na wapi ikaonyesha mafanikio?Na hayo mafanikio yalikuwa ni asilimia ngapi?
 
Msiojua hii ni sauna ipo toka zamani, hakuna hoteli kubwa isiyokuwa nayo, kazi yake kutoa sumu mwilini nk, inasaidia sana hata magonjwa nyemelezi ngumu kupata anayefanya sauna
Pengine wewe unazisikia sauna tu. Mimi nimezitumia miaka mingi tu. Tena kule kwa wenyewe, wenye sauna. Tatizo la hiki ''kituko'' cha Muhimbili ni kuwa wao wanapigia debe inatibu corona wakati wenye sauna wanazitumia kwa burudani. Ingekuwa sauna inasaidia kwenye corona basi nchi zenye sauna karibu kila nyumba kama Finland wasingehangaika.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne za kujifukiza.

Wakati Muhimbili zikifungwa mashine tatu, Mloganzila imefungwa moja. Gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10.

Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.

“Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10,” Profesa Museru.

Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.


Mwananchi
 
Sauna za wazungu ni sawa sawa na nyungu ? Maana wao walisema hazifai katika kipindi hiki cha kovidi, labda wataalamu watakuwa wameweka vya ziada ili kuzifanya salama na tofauti na hizo za wazungu
Ngoja tuone huenda ina vitu vya ziada
 
Kupiga nyungu imejaribiwa lini na wapi ikaonyesha mafanikio?Na hayo mafanikio yalikuwa ni asilimia ngapi?
Haya ndiyo maswali ya kuuliza. Asante. Utapata majibu.
====

Soma post namba 226 ya uzi huu utapata majibu.

 
Back
Top Bottom