Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne za kujifukiza.


Wakati Muhimbili zikifungwa mashine tatu, Mloganzila imefungwa moja. Gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10.

Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.

“Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10,” Profesa Museru

Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.


Mwananchi
 
Yaani kuvuta hayo mamivuke buku 5, kwamba kila mtu hawezi kutengeneza nyumbani kwake.....hivi mnauelewa kwamba mazingira ya humo ndani na idadi ya watu watakaoingia itachochea zaidi maambukizi ya korona na magonjwa mengine kama TB, hivi nchi hii wote wamegeuka waganga wa kienyeji?
 
hahaaaaaaaaaaaa this is funny,watu na taaluma zao kabisaa...
Wakisema steaming utakubali lakini wakisema nyungu unadharau. Waafrika tuna shida kwenye ubongo wetu hasa mnaojifanya mmesoma kumbe mmekariri hamkuelimika kabisa. Unajua kuwa virus wa corona ni inflammatory? Na kwamba virus wanauwawa na joto sasa steaming au nyungu ndiyo njia mwafaka ya kuwazuia.wasiendelee kuongezeka puani na njia za hewa mdomoni? Elimikeni kwanza then mpinge kwa akili basi nyinyi utopolo.
 
Safi sanaa MNH. Waliokuwa wakisema eti Tanzania hatuwezi kugundua chanjo ya korona wako wapi sasa!???
 
Hata nyumbani kwako unaweza jifanyia!

Unachemsha maji, unayawekea unachotaka kuweka, unachukua taulo, unaanza kuuvuta mvuke wake huku umejifunika na taulo lako.

Huhitaji kwenda kwenye kibanda cha Muhimbili...
Kumbuka kuna watu hawana uwezo kama wewe. Hivyo hiyo ni kwa ajili ya watu wakipato cha chini.
 
Yote hayo kumfuruhahisha mtu fulani

Wengi wa Watanzania wanaishi chini ya Dola 1 (Tsh 2300/- )

Kujifukiza ni karibia Dola 2 , Tsh 5000/-

Tano tena tumuongeze akae hata milele au nasema uongo ndugu zangu?
 
Yote hayo kumfuruhahisha mtu fulani

Wengi wa Watanzania wanaishi chini ya Dola 1 (Tsh 2300/- )

Kujifukiza ni karibia Dola 2 , Tsh 5000/-

Tano tena tumuongeze akae hata milele au nasema uongo ndugu zangu?
[emoji41]
 
Hivi kwa nini tusipende vya kwetu? Shida ni nini iwapo na sisi watalam wetu wameona njia bora mojawapo kua ni hiyo? Kwani na sisi hadi tuige kwa kwingine? Naunga mkono msimamo wa Nchi yangu
Hao walishagilimishwa ubongo (brain washed) kitambo tu; sampo za bongo zao zimehifadhiwa moseleum ya London & Washington. Ingekuwa Mzungu ndiye kaizindua hiyo nyungu, hawahawa mambweta wangeshindana fasta kuanzisha nyuzi hadi Mods wangechoshwa kuziunganisha.
 
Kupiga nyungu ilijaribiwa lini na wapi ikaonyesha mafanikio?Na hayo mafanikio yalikuwa ni asilimia ngapi?
Hiyo ni mashine au ni kibanda cha mlinzi.Kinagharimu shs.ngapi.Hiyo haisaidii chochote kwenye corona hii ya sasa.Naona waleeeeeee wanakuja taratibu.Hivi ukiingia humo kuna hewa ya kutosha au utazirai,hivi daktari anakupima kwanza kabla hujaingia humo au ikoje.

Ni kina nani hawaruhusiwi kuingia humo.

Naona tunafanya mambo ya ajabu wakati tulishaambiwa hakuna corona Tz.Juzi viongozi wa Dini Rc na KKKT tumewasikia vizuri.Tutatekeleza maelekezo yao. Haya ya shs.5000 mmmm?mmmmmmm?m???mmm?mm
 
Back
Top Bottom